tena mie nilivyo na hasira, naweza kumfungulia kesi kwa kunidhalilisha.Hapo mbona simple tuu.? Kwa mfano ulioutoa kama hana silaha kwa maana ya kuwa si jambazi na ninammudu kisawasawa, namchukua na kuelekea naye kituo cha polisi na kila mtu aandikiwe maelezo yake, ikibidi tutaenda hata hospitali kuthibitisha kama anachokidai ni kweli. Nitakuwa tayari kupoteza pesa na muda ili iwe fundisho kwake na kwa watu wa aina yake.
Naenda nae Sinza kuna masela wangu kule wanapenda sana Sinema hizi. Watamfundisha adabu!
Hapo mbona simple tuu.? Kwa mfano ulioutoa kama hana silaha kwa maana ya kuwa si jambazi na ninammudu kisawasawa, namchukua na kuelekea naye kituo cha polisi na kila mtu aandikiwe maelezo yake, ikibidi tutaenda hata hospitali kuthibitisha kama anachokidai ni kweli. Nitakuwa tayari kupoteza pesa na muda ili iwe fundisho kwake na kwa watu wa aina yake.
Ungelifanyaje? Mchana kweupe, ukiwa na gari lako kwa mwendo si wa kasi sana, mitaa ya sayansi anakupiga mkono binti. Unajiuliza ni nini? Unataka kupitiliza lakini hisani inakujia na kuamua kusimama. Anakusarimu binti mzuri tu, anakuomba samahani kwa kukusimamisha kisha anakuambia anaomba lifti kama unaelekea posta umsaidie. Unamwambia mimi naelekea maeneo ya agakhani, sifiki posta. Anakwambia basi nisogeze hata mbele utakuwa umenisaidia. Unamchukua, bila kumsemesha chochote kuhusu mapenzi isipokuwa maongezi tu ya kawaida.
Unafika karibu na unakoelekea unamwambia, kwa kuwa mi naelekea kushoto basi nikuache hapa. Mara unasikia, umwache nani? ndo utanijua mi nani, nilipe elfu hamsini yangu, kama haunilipi napiga kelele. Na muda huo sauti anayotumia ni ya juu tayari tena ya hamaki. Ungelikuwa wewe ungelifanya nini?