Ungekuwa wewe ungefanyaje

dorcas1234

Senior Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
116
Reaction score
34
Habari wana jf,hebu tufurahi kidogo hapa ikiwa ni pamoja na kutafakari kama yanaweza kutufika sisi tungefanyaje.Kuna wanandoa fulani ambao wamedumu katika ndoa yao takribani miaka kumi,lakini katika miaka kumi hii kumbe mume hakuwa muaminifu,alikuwa anatembea na dada fulani kwa siri bila mke wa jamaa kujua,mpaka akafikia kumjengea huyu kimada nyumba ya kuishi,yaani mpaka hapo mke mtu hajui lolote.
Sasa kama ujuavyo wakina dada/mama akishachukua mume wa mtu tena akamfanyia kitu kikubwa kama hicho wengi huona jamaa hafurukuti,yule dada wakati ujenzi unaendelea akaanza kuwa na mdomo mdomo sana mara kuwafokea mafundi,kuwatukana bila sababu kitu ambacho mafundi kiliwaudhi sana kikapelekea fundi mmoja kujiapiza kuwa lazima akamueleze mama watoto wa jamaa,
Nyumba ilipoisha wakapanga siku ya kuhamia na walishirikisha mafundi kuwa siku hiyo wawepo hapo kwa ajili ya kusaidia kupangapanga mizigo mafundi wakakubali.Baada ya kujua tarehe fundi akaondoka mpaka kwa yule mke wa jamaa.akamweleza kila kitu mpaka tarehe yao ya kuhamia huko,mama akasema sawa wakapanga akaenda kupaona na hapo mahali wakati huo fundi alitoa copy ya funguo akampatia yule mke mtu.
Jioni ya siku hiyo Mume akarudi nakumuambia mkewe kuwa nimepata safari ya kikazi "hane kwa hivo nitakuwa mkoani kwa wiki mbili",mama akasema sawa lakini alikuwa tayari anajua nini kinaendelea.Asubuhi mume alipoondoka mama akatafuta dalali ampangishie ile nyumba ( wanayoishi sio mpya)akatafuta na vijana hapo mtaani wakamsaidia kufunga mizigo huyooooooo akahamia nyumba mpya ya hawara wa mumewe,huku alikotoka mpangaji akapatikana akahamia.
Baada ya siku 4 wakati mke mtu kashakuwa mwenyeji hapo nyumba mpya yule hawara na mume wa mwenzie ndio hao wanakuja wenyewe na fuso lao,mke akawa anachungulia dirishani,alipoona wameshuka akatoka na kwenda kumlaki mumewe,"karibu mume wangu" jamaa alitaka kuzimia akamwabia dereva wa fuso geuza gari, hao wakarudi walikotoka,mke mtu akabaki anacheka kwa ujasiri japo roho ilikuwa inamuuma.

kama ni wewe ni mwanamke au ni mwanaume ungefanyaje?
 
duh!!! kweli huyo mwanamke ana mipango!!! nimemkubali
 
Nice Story.
Mke amecheza kama "Mwanamke hodari aliyejawa na ujasiri wa hali ya juu".
 
"Ngoma ikilia sana haichelewi Kupasuka"
Nyumba ndogo ilijisahau sana ikaanza
kupayuka... . ........
 
Huyo mama yuko juu aisee.
ha haaa, kama namuona vile anavyojifaidia jasho lake.......
sijui huyo baba atarudi home baada ya safari ya kikazi ya wiki 2?
ila huyo baba alizidisha..... kaamua kuchukua na likizo kabisa ya wiki 2....
pole zake huyo kimada, maana najua baada ya hili fumanizi mume si wake tena
 
kisa kinasikitisha sana! Kidume lazima uwe mpole
 

ndivo inavokuwaga,unajua nini kiliendelea?vyombo vilikaa kwenye fuso wiki huku akitafuta nyumba nyingine ya kupanga.chezeya mwanamke na moyo wa simba weye?
 
ndivo inavokuwaga,unajua nini kiliendelea?vyombo vilikaa kwenye fuso wiki huku akitafuta nyumba nyingine ya kupanga.chezeya mwanamke na moyo wa simba weye?
ha haaa, huko walikotoka walishapangisha hiyo nyumba?
baba naye alibaki kwenye fuso hiyo wiki nzima au alirudi kwa mkewe?
mpaka muda huu baba yuko wapi?
Nimempenda sana huyo mama, yaani hata ningekuwa mimi ningefanya hivyo hivyo
 
hiki kisa ni cha kweli na mume ni mwajiriwa serikalini kwa mama Ti.ba.i.ju.ka
aaahhhhh! wale wanakuwaga na viwanja vingi tu....
huyo kimada asubiri kidogo tu ataporomoshewa mjengo mwingine wa kisasa....
ila mimi ningekuwa ndo mke, masikio yangefunguka mara tatu.....
na kama bado nampenda huyo mume, ningemwambia arudi home nimemsamehe, huyo dada sasa angemsikia kwa jirani, maana ningejitolea kuwa dereva wake
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…