Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

zethumb

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
610
Reaction score
137
Nilikuwa na mpenzi toka mwaka 2006 nimeishi nae nikiwa chuo na bahati nzuuri tukapata mtoto lakini si bahati akafa baada ya miezi michache!, nilibahatika siku moja kwenda mkoani kusalimia wakti wa likizo. Nikiwa home kama familia ya one parent tukawa tunajadili mambo ya kuoa, mimi kwa upande wangu nilikuwa simba mwenda pole na home walikuwa hawajawahi kuniona na demu, kwa hiyo siku hiyo nikabanwa kusema kuna nini ndo kusema kuhusu mausiano hayo, mamangu alisikitika sana na akaomba kusalimiana na mpenzi wangu nikampa namba wakaongea sana na ki ukweli mzazi wangu akatokea kumpenda walivyokuwa wanaoongea kwenye simu kwa muda wote niliyokuwa mkoa... nilivyo rudi dar baada ya siku kadhaa mzazi wangu akaniuliza..kama mwenzangu mzima maana ana siku nyingi hawajaongea na akimtafuta hampati, nikampa taarifa mpenz wangu... mzazi wangu baadae akaumwa sana na hata akiwa kitandan aliniambia nimsalimie mpenz wangu nikamuuliza kwani hawawasiliani akaniambia toka nimetoka mkoa hajawahi kumpata na mpenz wangu hajawai kumpigia simu..kwa kweli jambo hili liliniuzi sana, nikamwambia mzazi wangu huyu mtu HANIFAI na sina mpango nae tena na hivyo HASIMTAFUTE TENA! Mungu alimpenda mzazi wangu akamchukua...mpenz wangu hakuwa hewan nikamwambia mdogo wake kuwa nimepata msiba wa mzazi wangu!.... baada ya miwezi kadhaa kupita ndo mpenz wangu ananiuliza ..eti mama afarikije? nilikasirika sana na swali hili maana hata kunipa pole tu HAKUNIPA hali anajua nilifiwa! kuheshimu ahadi yangu kwa mamangu nikamuita mpenz wangu nikamwambia MIMI NA yeYE BASI! na kuachana nae si kwa sababu hiyo tuu, huyu mtu amekuwa akifanya mambo yako kunyume kabisa na tunavyokubaliana , na kila tukianza mazumgumzo ya maisha ya baadae anakwepa, ndugu marafiki zangu alikuwa hatki kukutana nao, ila kusalimiana kwenye simu ndo anakubali, anaweza hasipatikane wiki nzima, nimekuwa nikimpigia simu kwa mara moja moja, ila kila nikimpigia ananitumia sms ...nimsamehe anajua amekosa, eti na yeye ana mambo mazuri alinifanyia hivyo turudiane...na mambo mengine kibaoo! JAMAN katika mazingira haya maamuzi yangu ni kinyume kweli?
natanguliza shukrani zangu!
 
Kutokana na maelezo yako inaonyesha wazi kwamba mahusiano yenu sio mazuri. Kwanza nawashauri kama mnataka kuendelea mkapime afya zenu, mna historia ya kutatanisha. Mapenzi ya mbali mara nyingi ni ya kudanganyana, na uwezekano wa kuambukizana magonjwa kama bado hamjaambukizana ni mkubwa sana kwasababu wewe hata kondom hutumii na mwenzako pia hakuulizi, wote mnaonekana mnapenda kucheza pekupeku historia ya mapenzi yenu imethibitisha.
 
Pole sana kwakufiwa na Mzazi, kuhusu huyo mwanamke hakufai kwani mpenzi mwema ni yule unaekua nae pamoja kwenye raha na huzuni, kama umeachana nae kwa ridha yako mwenyewe umefanya jambo la maana sana sababu sie...
 
Bahati mbaya sioni hata cha kukushauri maana jibu unalo tayari.
 
Unaomba ushauri wa nini hapa wakati tayari ulishaamua kumpiga chini?
 
Mkuu achana kabisa na huyo kiumbe ni shetani,samahani kwa kutumia hilo neno.Ila uamuzi wa mwisho unao wewe.
 
Kutokana na maelezo yako inaonyesha wazi kwamba mahusiano yenu sio mazuri. Kwanza nawashauri kama mnataka kuendelea mkapime afya zenu, mna historia ya kutatanisha. Mapenzi ya mbali mara nyingi ni ya kudanganyana, na uwezekano wa kuambukizana magonjwa kama bado hamjaambukizana ni mkubwa sana kwasababu wewe hata kondom hutumii na mwenzako pia hakuulizi, wote mnaonekana mnapenda kucheza pekupeku historia ya mapenzi yenu imethibitisha.
nilitambua hilo nikaondoka mapema ndugu, pili sina mpango wa kuendelea nae maana sina desturi ya kuyarudi maneno yangu kimaamuzi! sio mapenzi ya mbali tulikuwa hapa na bado tupo hapa hapa darslam! kondom kweli niliacha zamani kutumia nae lakini naamini niko fiti!
 
Unaomba ushauri wa nini hapa wakati tayari ulishaamua kumpiga chini?

nilichotaka kupata kutoka kwenu wadau ni je maamuzi yangu ni haki kwa mtu wa namna hii ukizingatia maelezo niliyotoa, na je ungekuwa wewe ungechukua maamuz tofaut na haya, mimi niliona vema niachane nae na ni muda kitambo na sikutarajia kupost hii thread humu lakini sms zake za hivi karibun ndo zimenifanya kupost hiii thread, mfano anadai kwanini sitaki kumjulia hali, je yeye hanifai tena, na kwamba hana thamani tena kwangu na kuwa je haku fanya chochote kizuri kwangu mpaka nimfanyie hivyo....kwa hiyo ndugu nashindwa kumwelewa huyu mtoto ...
 
nilitambua hilo nikaondoka mapema ndugu, pili sina mpango wa kuendelea nae maana sina desturi ya kuyarudi maneno yangu kimaamuzi! sio mapenzi ya mbali tulikuwa hapa na bado tupo hapa hapa darslam! kondom kweli niliacha zamani kutumia nae lakini naamini niko fiti!

...Hapo kwenye maandishi mekundu, . Kama uamuzi wako ndo huo, ss unataka tukushauri nn tena jamani???????????
 
Mkuu achana kabisa na huyo kiumbe ni shetani,samahani kwa kutumia hilo neno.Ila uamuzi wa mwisho unao wewe.

uamuzi nilishachukua ila nilitaka kufahamu je ni haki ukizingatia nilishazaa nae lakini mtoto ndo hivyo alitutoka...
 
Bahati mbaya sioni hata cha kukushauri maana jibu unalo tayari.

i needed to know if i am being fair to her considering her recent counter attacks at me!
 
...Hapo kwenye maandishi mekundu, . Kama uamuzi wako ndo huo, ss unataka tukushauri nn tena jamani???????????

nilichotaka ni ushauri kama je nimefanya vema kuondoka au vipi? maaana unaweza kuamua kwa nafsi yako kumbe umekosea, na kila mtu anazo taratibu za kuishi na watu ndo ufanya abadilike kimtazamo!
 
i needed to know if i am being fair to her considering her recent counter attacks at me!
Hee!Umeamua sasa kutumia lugha ya kigeni?Mwenzako nilikimbia umande na natumia lugha yangu ya taifa,nitafsirie kwanza nielewe ndio tuendelee na habari hii.
 
Pole kwa kufiwa ila kwa huyo mupenzi wako mmmmh ngumu kumeza
 
kuna watu hawajali hata
piga chini
keshafulia huko aliko
 
Back
Top Bottom