Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Author

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
1,709
8,007
UNGEKUWA NI WEWE UNGECHUKUA UAMUZI GANI?
Siku zote mke wangu amekuwa akiniambia kuwa ananipenda sana. Kitu kizuri zaidi amekuwa akinionyesha upendo huo, jambo ambalo limenifanya nijivunie kuwa naye siku zote.

Siku moja nikaamua kumtania kwani tumezoea kutaniana, na siku zote amekuwa akifurahia utani wangu.

Nikamtania, ‘mke wangu, nimefukuzwa kazi. Na kibaya zaidi wamesema nitafirisiwa nyumba pamoja na gari zangu ili kufidia hasara ya kampuni’.

Mke wangu aliniangalia kwa ukali, kitu ambacho hakijawahi kutokea hata siku moja, kisha akanifyonya. Kwanza kabisa nilishangaa, mke wangu ananifyonya! Haijawahi tokea tangu tuanze mahusiano yetu, ila nikaona huenda tu ame-panick kwa sababu ya taarifa niliyompa.

Basi akaenda zake kulala na usiku mzima hakutaka kuniongelesha kabisa.

Asubuhi kulipokucha nilishangaa kuona mke wangu amekusanya vitu vyake nje, nikamuuliza mbona anatoa vitu nje? Akanijibu hawezi tena kuishi na mimi kwani hawezi kuishi na mwanaume ambaye hana kazi, pesa, nyumba wala gari.

Nikamwambia naomba uniachie mwanangu basi, akanijibu kwa ukali, huyu sio mwanao na hapa unaponiona nataka kuelekea kuishi kwa baba wa mtoto wangu.

Kichwa changu kilichanganyikiwa, sikutegemea kama utani ule ungeweza kuzua yote yale. Nikaamua kumuita mke wangu niongee naye kumjulisha kuwa nilikuwa namtania tu.

Nikamwambia, ‘mke wangu, pole sana nilikuwa nakutania tu. Ukweli ni kwamba nimepandishwa cheo kazini, na pia nimepewa nyumba nyingine kubwa zaidi ya hii pamoja na gari zuri zaidi la kutembelea, hivyo kesho tunahamia nyumba nyingine ambayo ni nzuri sana’.

Huwezi amini, mke wangu aliruka juu kwa furaha akanikumbatia na kunipa mabusu tele huku akisema, ‘nakupenda sana mume wangu kipenzi, siku zote za maisha yangu sijawahi kujuta kuwa nawe. Naomba unisaidie kurudisha vitu ndani’.

Nikamsaidia kuingiza vitu vyote ambavyo alikuwa ametoa. Tulipomaliza, nikamuuliza kwa upole, mke wangu ina maana kweli ndio ulikuwa unaondoka?

Akanijibu, ‘hapana mume wangu, nilikuwa nakutania tu. Kwa namna ninavyokupenda nisingeweza kukuacha peke yako’.

Tayari tumehamia nyumba mpya, na maisha yamekuwa bora zaidi kuliko mwanzoni kutokana na kupandishwa cheo. Lakini akili yangu bado inafikiria kitendo kile na pia maneno aliyoniambia juu ya mtoto.

Hivi hapa kuna upendo kweli? Na ungekuwa ni wewe ungefanyaje? Tupia comment yako hapo chini...!
 
Kama in kweli kile alichoonyesha mwanzo ndio uhalisia, na alishindwa kuzuia hisia na ukweli uliopo na wewe ulitakiwa umuache upate majibu yote then uamue vizr, Ila huna mke kama ni mchumba muage mapema maana hili likitokea utaakimbiwa!
 
UNGEKUWA NI WEWE UNGECHUKUA UAMUZI GANI?
Siku zote mke wangu amekuwa akiniambia kuwa ananipenda sana. Kitu kizuri zaidi amekuwa akinionyesha upendo huo, jambo ambalo limenifanya nijivunie kuwa naye siku zote.

Siku moja nikaamua kumtania kwani tumezoea kutaniana, na siku zote amekuwa akifurahia utani wangu.

Nikamtania, ‘mke wangu, nimefukuzwa kazi. Na kibaya zaidi wamesema nitafirisiwa nyumba pamoja na gari zangu ili kufidia hasara ya kampuni’.

Mke wangu aliniangalia kwa ukali, kitu ambacho hakijawahi kutokea hata siku moja, kisha akanifyonya. Kwanza kabisa nilishangaa, mke wangu ananifyonya! Haijawahi tokea tangu tuanze mahusiano yetu, ila nikaona huenda tu ame-panick kwa sababu ya taarifa niliyompa.

Basi akaenda zake kulala na usiku mzima hakutaka kuniongelesha kabisa.

Asubuhi kulipokucha nilishangaa kuona mke wangu amekusanya vitu vyake nje, nikamuuliza mbona anatoa vitu nje? Akanijibu hawezi tena kuishi na mimi kwani hawezi kuishi na mwanaume ambaye hana kazi, pesa, nyumba wala gari.

Nikamwambia naomba uniachie mwanangu basi, akanijibu kwa ukali, huyu sio mwanao na hapa unaponiona nataka kuelekea kuishi kwa baba wa mtoto wangu.

Kichwa changu kilichanganyikiwa, sikutegemea kama utani ule ungeweza kuzua yote yale. Nikaamua kumuita mke wangu niongee naye kumjulisha kuwa nilikuwa namtania tu.

Nikamwambia, ‘mke wangu, pole sana nilikuwa nakutania tu. Ukweli ni kwamba nimepandishwa cheo kazini, na pia nimepewa nyumba nyingine kubwa zaidi ya hii pamoja na gari zuri zaidi la kutembelea, hivyo kesho tunahamia nyumba nyingine ambayo ni nzuri sana’.

Huwezi amini, mke wangu aliruka juu kwa furaha akanikumbatia na kunipa mabusu tele huku akisema, ‘nakupenda sana mume wangu kipenzi, siku zote za maisha yangu sijawahi kujuta kuwa nawe. Naomba unisaidie kurudisha vitu ndani’.

Nikamsaidia kuingiza vitu vyote ambavyo alikuwa ametoa. Tulipomaliza, nikamuuliza kwa upole, mke wangu ina maana kweli ndio ulikuwa unaondoka?

Akanijibu, ‘hapana mume wangu, nilikuwa nakutania tu. Kwa namna ninavyokupenda nisingeweza kukuacha peke yako’.

Tayari tumehamia nyumba mpya, na maisha yamekuwa bora zaidi kuliko mwanzoni kutokana na kupandishwa cheo. Lakini akili yangu bado inafikiria kitendo kile na pia maneno aliyoniambia juu ya mtoto.

Hivi hapa kuna upendo kweli? Na ungekuwa ni wewe ungefanyaje? Tupia comment yako hapo chini...!
We endelea kulea sperm za mwanamme mwenzio
 
Japo story ya kutunga nimekuelewa ila ingekuwa ni ya kweli hayo uliyo andika huyo mke hafai ni chui unayeishi nae.
 
Hii "hadisi" hata Shigongo hawezi kukubali kuichapisha kwenye magazeti yake ya udaku.
 
Mungu alikuonyesha mbinu nzur ya kumjua mnafiki sa umeshajua bila kutumia nguvua alfu bdo unaamua kuwa fala du ww ni jinga miaka yote ijayao
 
Kama kweli kwanza nawashangaa hao waliokupandisha cheo maana sikuoni ukiitumia akili ya kisomi zaidi nakuona kama zezeta tu!

Mwanaume timamu hapo hapo pa kuambiwa “hata huyu mtoto siyo wako" angechukua hatua kali kufatilia hiyo issue,awe alitania au hakutania DNA lazima ingepimika na hata kama ikasoma mtoto ni wako kuna advantage kubwa mkeo ana bwana anambandua na alishamdanganya kipindi akiwa na mimba ya huyo mwanao kwamba mimba ni yake ila wewe anakupiga changa la macho tu.
 
Halafu baadaye mnakuja kuanza kuilaumu serikali kwa kutowaamini vijana na kuwaajiri katika sekta muhimu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom