Ungekuwa wewe ungeamuaje?

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,989
Reaction score
5,069
Una mchumba ambaye mmeshatambulishana pande zote kwamba mtaoana. Mko pamoja kwa miaka miwili na kipindi chote mmekuwa mkifanya mapenzi kwa condom na kipindi chote mmekuwa waaminifu kwa kila mmoja. Mnajadiliana na kukubaliana kuzaa mtoto. Siku moja mwenzako anakuambia aliamua kwenda kupima vvu ili isitokee ajali ya kumuambukiza mtoto. Bahati mbaya kakutwa ameathirika, wewe unapima na kukutwa mzima. Mwenzako anakuambia ameamua kuwa muwazi ili muweze kujadiliana pamoja. Kaka, dada ungeamuajae hapo? Unamuacha? Unaendelea naye? Kwa kila uamuzi ni kwa nini unaamua hivyo? Karibuni kwa mchango wenu wa mawazo.
 
Kwa kuwa nikifa niatazikwa peke yangu, nampiga kibuti ili na yeye aanze kujiandaa kisaikolojia, akifa azikwe peke yake......
 
Dah! huyo kama huku vaa soksi nenda kapime tuu mkuu wala nisikufariji manaake maneno yake yana maanisha..
 
Kujipiga kisu mpaka kujiua ni zambi, jamhuri inatakiwa kukushitaki... kuishi na kisu jikoni ni kitu cha faraja kinakupunguzia msongo wa mawazo pale utakapo hitaji kukata nyama.
 
Kujipiga kisu mpaka kujiua ni zambi, jamhuri inatakiwa kukushitaki... kuishi na kisu jikoni ni kitu cha faraja kinakupunguzia msongo wa mawazo pale utakapo hitaji kukata nyama.

Duh! Nimetoka kapa hapa!
 
Hivi kumbe watu huwa wanaanza kufanya mapenzi kwa kondomu halafu baadaye wanaenda kupima...mmmh!!!
 
Kwa kuwa nikifa niatazikwa peke yangu, nampiga kibuti ili na yeye aanze kujiandaa kisaikolojia, akifa azikwe peke yake......

Imagine ndo wewe unapigwa chini utajisikiaje? Ungependa ufanyiwe nini?
 
Hivi kumbe watu huwa wanaanza kufanya mapenzi kwa kondomu halafu baadaye wanaenda kupima...mmmh!!!

Na wengine wanaanza na condom baada ya miezi miwili wanaacha hata hizo condom bila kupima. Wanaoenda kupima mwanzo kabisa ni wachache sana.!
 
mh ngumu kumeza mpe faraja yako ili aweze kuishi miaka ming zaidi
 
Life goes on and I will move on.... Nitamsaidia tu kuweza kukubaliana na hali halisi mpaka atakapokuwa ready to be alone..may be
 
Na wengine wanaanza na condom baada ya miezi miwili wanaacha hata hizo condom bila kupima. Wanaoenda kupima mwanzo kabisa ni wachache sana.!

Basi hatari sana mkuu...
 
ahahah....ndom two yrs!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mbado...
 
Life goes on and I will move on.... Nitamsaidia tu kuweza kukubaliana na hali halisi mpaka atakapokuwa ready to be alone..may be

Mtaendelea kupeana mchezo? Nimependa ushauri wako lakini.
 
ahahah....ndom two yrs!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mbado...

Mkuu inawezekana kabisa. Ni tamaa tu ndo zinatufanyaga tuhatarishe afya zetu. Imagine mnakaa mikoa tofauti na kukutana ni kila baada ya miezi mitatu. Hutakiwi kumuamini mwenzio mpaka mtakapooana ambapo assumption ya kujicomit kwa mwenzio inakuwepo. Kipindi cha uchumba kila mtu anakuwa akibahatisha sehemu ya kuoa/kuolewa. Usiamini kwamba mmepima na kukutwa mko safi.! Kuna window period ndio inayotuangamiza wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…