Ungefanya nini kama hii ingekutokea wewe?

Ungefanya nini kama hii ingekutokea wewe?

Moo Click

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Posts
3,495
Reaction score
3,261
Umemkopesha rafiki yako wa karibu Tshs 400,000 mwaka jana, lakini tokea wakati huo amekuwa mgumu kulipa deni hilo, kitu kilichochangia kudorora kwa urafiki wenu. Unamuomba akulipe basi walau Tshs 200,000 tu alafu umsamehe hiyo nyingine kwakuwa kwa sasa una ukata na matatizo na una uhitaji na hiyo hela.

Rafiki yako huyo anakuambia anaweza kukupatia tu Tshs 150,000 kwasababu ndio kiasi alichonacho. Unaona huna namna zaidi ya kukubali tu kiasi hicho. Unampatia details zako za benki na account namba akutumbukizie humo.

Kuamka asubuhi unatizama kwenye account yako unakuta kuna Tshs 1,500,000[emoji15][emoji15] Unatizama tena kwa makini huamini unachokiona lakini bado kweli ni Tshs 1,500,000.

Unatizama vizuri simu yako unakuta missed calls 53 na meseji 27 akiomba umrudishie Tshs 1,350,000 kwasababu alitaka kutuma tu Tshs 150,000 lakini akakosea akaongeza 0 moja.

Wewe ungechukua maamuzi gani?

1. Utamrudishia kiasi anachoomba urudishe Tshs 1,350,000?
2. Utachukua zile zako unazomdai Tshs 400,000?
3. Utachukua zote Tshs 1,500,000?
 
Hapo hairudi hata ile senti 20 ya mbuni

"ᴺᵒ ⁱᵐᵖᵒˢˢⁱᵇˡᵉ ᵗʰᵉ ʷᵒʳᵈ ⁱᵗˢᵉˡᶠ ˢᵃʸˢ ᴵ'ᵐ ᵖᵒˢˢⁱᵇˡᵉ"
Haha kwa nini?
 
Haha kwa nini?
Binafsi huwa sipendi mtu anitese kwa changu nilokitolea jasho na ikitokea hivyo atajuta tu siku nikipata pa kukamatia.

"ᴺᵒ ⁱᵐᵖᵒˢˢⁱᵇˡᵉ ᵗʰᵉ ʷᵒʳᵈ ⁱᵗˢᵉˡᶠ ˢᵃʸˢ ᴵ'ᵐ ᵖᵒˢˢⁱᵇˡᵉ"
 
Mkuu huo Ni mfano au ishu ambayo ipo serious

Ila Kama Ni kweli usirudishe hata Mia,haiwezekani akutese muda wote huo na Mali yako na Kama urafiki ufe hapo hapo
 
Nadhani namba 2 kwangu inanifaa zaidii



Wanangu wa A town inakuaje??
 
Hapo ni kuchukua tu 400k yako basi nyingine ile unarudisha kiroho safi! Sababu shida ilikuwa ni deni lako tu! Na atimaye limerudi kwa nguvu za ajabu!
 
Chukua tu kilicho haki yako, yaani ile fedha unayomdai
Kisha inayobakia (ambayo ni yakwake), mrejeshee . Kisha mshukuru Mungu
 
[emoji23][emoji23]
Mkuu huo Ni mfano au ishu ambayo ipo serious

Ila Kama Ni kweli usirudishe hata Mia,haiwezekani akutese muda wote huo na Mali yako na Kama urafiki ufe hapo hapo
Mkuu unalipiza kisasi ni mfano tu nimekutana nao mahali nikaamua kushare na ma GT maana hii hali inatokea sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom