Unga wa Ubuyu unatibu nini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unga wa Ubuyu unatibu nini??

Discussion in 'JF Doctor' started by kidi kudi, Aug 20, 2012.

 1. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Wadau kuna rafiki yangu kanishauri niwe angalau kwa siku ninywe juisi ya unga wa ubuyu eti ni nzuri kiafya na hakuniambia kwa kina faida yake.

  Mwenye kujua tujuzane tafadhali faida ntakayoipata kiafya.

  Asanteni.
   
 2. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mwuulize, uwe na uhakika.
   
 3. b

  bidada Senior Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ina vitamin c nyingi kuliko machungwa
   
 4. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Watu wa nutrition tunaomba jibu.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Kila kitu mbona dawa...tuhamie porini tukaishi na matunda...
   
 6. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Pia ina boost imune
   
 7. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60

  Nimegundua kwamba kula vitu natural ndo ujanja! watu siku hizi wakikuona kila siku unaulizia matembele wanakuona kama uliefulia kumbe kwenye mboga za majani kuna utajiri wa afya zetu
   
 8. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mkuu kwa nini ulimuachia kabla hajakupa majibu ya kina?
  ona sasa tunakosa point hapa.
   
 9. b

  bidada Senior Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Husaidia kuongeza kumbukumbu, huongeza kinga za mwili, hutibu figo, hutibu magonjwa ya moyo, macho kuona vizur, huimarisha fizi na mifupa pia ngozi na misuli.
   
 10. b

  bidada Senior Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ila yakupasa unywe wenyewe usichanganye na kitu chochote. Kwa upande wangu imenisaidia sana kuni shape mwili japo imechukua muda kidogo
   
 11. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  wapi mzizi mkavu?? Au leo anasinzia??
   
 12. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Dah..!kumbe faida ni za kutosha tu..basi inabidi nianze kunywa kwa wingi maana niliona kama jamaa ananizingua
   
 13. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  mi nilijua ananitania tu coz siku hiyo tulikuwa wote nikamwambia naskia kiu nataka nipaje soda kupoza koo..ndipo akaniambia nibora niwe nakunywa juisi natural especially juisi ya ubuyu eti ni nzuri kiafya..nilichukulia ni utani tu
   
 14. b

  bidada Senior Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mi imenisaidia sana kwenye kupunguza uzito na kuumwa kichwa, nakushaur uitumie mkuu.
   
 15. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  nimeshaununua hapa ni kutendeneza juisi na kuanza kugonga mdogomdogo..
   
 16. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kweli nilipewa darasa hilo na mtaalamu mmoja.
   
 17. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wakuu,ni kweli ni tiba.Pia,kumbukeni kuwa ubuyu unatoa faida tele kupitia mafuta kutokana na mbegu zake;bila kusahau sabuni nk.
   
 18. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wakuu,kuweni makini kwenye bidhaa za ubuyu kwani kuna uchakachuaji mkubwa sasa;kwa sababu ya soko kupanuka hata nje ya nchi yetu !
   
 19. s

  sky_haf JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  vp kuhusu huu ubuyu unouzwa ambao ushatiwa rangi na sukari, kuna faida yoyote au hasara inayopatikana?
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu LEGE  [​IMG]


  [​IMG]


  Mungu ameumba miti na mimia kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

  UBUYU WENYEWE
  Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una Vitamin C nyingi kuliko hata machungwa na ina kiwango kingi cha madini ya kashiamu (Calcium) kuliko hata maziwa ya ng’ombe.
  Aidha, unga wa ubuyu ni chanzo kikubwa cha madini mengine aina ya chuma (iron), Potasiamu (Pottasium) na manganizi (magnesium). Inaelezwa kuwa kiwangao cha Potasiamu kilichomo kwenye unga wa ubuyu ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye ndizi. Ubuyu ni muhimu sana kwa watu wenye matatizo ya figo.
  Vile vile unga wa ubuyu una uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili (antioxidant) kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya kuongeza kinga mwilini dhidi ya magonjwa nyemelezi. Kiwango chake kinazidi hata kile kinachotolewa na matunda mengine kama vile Krenberi, bluberi na blakberi. Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha.

  MAFUTA YA UBUYU
  Mafuta ya ubuyu, ambayo hutengenezwa kutokana na mbegu zake, ni mazuri kwa kulainisha ngozi na kukarabati au kuponya ngozi iliyoathiriwa na magonjwa ya ngozi mbalimbali, ikiwemo fangasi, vipele na chunusi.
  Mafuta ya ubuyu yana uwezo wa kuifanya ngozi kuwa nyororo na laini kutokana na kuwa na kiasi kingi cha mafuta aina ya Omega 3 na Omega 6 na ina kiasi kingi cha Vitamin A, D na E ambazo zote ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa ngozi ya binadamu.
  Mafuta ya ubuyu yanaelezwa kuwa na virutubisho vinavyoweza kuondoa mikunjo ya ngozi, mabaka, michirizi na hata makunyazi na kuicha ngozi kuwa mpya. Hutoa kinga dhidi ya uharibifu wowote wa ngozi unaoweza kujitokeza baadaye.

  JINSI YA KUTUMIA MAFUTA
  Mafuta ya ubuyu unaweza kuyatumia kwa kupaka usoni au mwili mzima moja kwa moja. Unaweza kuyatumia mafuta haya kwa kupaka sehemu tu iliyoathiriwa kama dawa. Unaweza pia kuchanganya na mafuta au losheni unayotumia.
  Ili kupata matokeo unayotarajia, hakikisha unatumia mafuta halisi ya ubuyu ambayo hayajachanganywa na kitu kingine wakati wa kutengeneza.

  UPATIKANAJI WAKE
  Bidhaa za ubuyu zimeanza kujipatia umaarufu nchini Tanzania na hivi sasa kuna makampuni na wajasiriamali binafsi wanaojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na ubuyu, hivyo upatikanaji wake ni rahisi iwapo utaulizia maeneo unayoishi.
  Bidhaa zingine zinazoweza kutengenezwa kutokana na mti huu ni pamoja na majani yake ambayo hutumika kama dawa, mizizi na magamba yake pia. Kwa ujumla mti wote wa ubuyu una faida na hakuna kitu kinachotupwa kwenye mti huu ambao ni miongoni mwa miti yenye matunda bora yaliyopewa jina la ‘superfruit’.


   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...