Unga umepanda bei, mshahara ni ule ule

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,983
1,574
Wanabodi, salaam.

Wakati mawaziri wakiendelea kutoa kauli zisizoeleweka kuhusu takwa la kisheria la kupanda mshahara mtaani hali inazidi kuwa mbaya.

Unga umepanda bei sana. mwezi january unga wa sembe kilo 25 ulikuwa ukiuzwa 14,500/= kwa bei ya jumla. Leo unga ule ule unauzwa 27,000/= kwa bei ya jumla.

Hii ni kwa bidhaa mbalimbali hata nyanya zimepanda bei, hii hupelekea watumishi kutomudu gharama za kawaida za maisha.

Kupanda kwa bei ya unga kwa zaidi ya 50% kuna uhusiano wowote wa kupanda kwa bei ya mkate Sudani? Au kuna uhusiano na kuzorota kwa uchumi tunaoelezwa na IMF?
 
Hii hoja ya mishahara naona inataka kuwa ajenda kuu. Hii ajenda ni hatari sana ,kama upinzani utaamua kuitumia vizuri inaweza kuleta shida kubwa.
 
Uzuri bia na Konyagi bei ni ile ile. Nyie endeleeni kula unga tu. Halafu tukishalewa tukiulizwa tunajibu Ndiyooooooooooooooooooo!!!!!
Nyie mnajibu Ndiooo!!
Halafu nyie mnashinda. Maisha yanasonga.
 
Mkuu kama huwezi kununua unga sio lazima ule ugali, vyakula viko vingi. Mshahara tutaongeza nchi ikishaendelea, tukiwa tuna barabara za juu, madege, matrain ya umeme nk sasa tufanye kazi kwa bidii tuzarishe kwanza tutaongezeana tu mishahara baadaye huko sio lazima uwe wewe hata mjuu wako..

Hapa kazi tu..
Kenge hasikii mpaka atoke damu masikioni.
CCM oyeee..
 
Uzuri bia na Konyagi bei ni ile ile. Nyie endeleeni kula unga tu. Halafu tukishalewa tukiulizwa tunajibu Ndiyooooooooooooooooooo!!!!!
Nyie mnajibu Ndiooo!!
Halafu nyie mnashinda. Maisha yanasonga.
Wee mrombooo wewe
Tukaribishane nyama choma nyie hii hali ya vyuma kukosa griss haijawagusa Sana.
 
Eti kwa sasa tufanye kwanza maendeleo....ningeona uzalendo ingekuwa Rais na balaza lake wakatangaza kupunguza kiwngo cha mshahara wao na stahiki nyingine ili wote tuchangie maendeleo
 
Mkuu kama huwezi kununua unga sio lazima ule ugali, vyakula viko vingi. Mshahara tutaongeza nchi ikishaendelea, tukiwa tuna barabara za juu, madege, matrain ya umeme nk sasa tufanye kazi kwa bidii tuzarishe kwanza tutaongezeana tu mishahara baadaye huko sio lazima uwe wewe hata mjuu wako..

Hapa kazi tu..
Kenge hasikii mpaka atoke damu masikioni.
CCM oyeee..
kipi ambacho hakijapanda chini ya jiwe?
 
Ndugu mshahara huwa hautoshi sikuzotee fanya mishe ata ki mpesa utaishia kumlaum rais wetu mpedwa
Ndugai mbona ametumia mabilioni ya pesa wakati mshahara wa kutosha anao yeye hafanyi mishemishe? huu mshahara wangu mdogo usiotosha hata matumizi ya kawaida unatosha kufungua biashara?
 
Back
Top Bottom