Du!
Hii ni kali!
Unanikumbusha kipindi cha Tume ya Bei za Bidhaa, enzi za Mwalimu!
Hoja yako ni njema, nadhani unachopenda kueleza ni kuwa Serikali iwe na nguvu au mkono uliofichika katika uendeshaaji wa shughuli za biashara!
Kwa sasa mambo ni hoberahobera, kila mtu anajiamulia lake...aidha kuficha mazao na hivyo kusababisha aina fulani ya scarcity, kwa minajili ya kuuza kwa bei ya juu wakati wa mahitaji!
Kinachoshangaza ni kuwa mamlaka husika hazifuatilii matendo ya hivo, hadi waziri husika atoke ofisini na kwenda kutafuta maghala yalipo na kuuliza ni wapi mazao yameenda!....aibu!
Kwa hoja yako, ni ngumu sana kudhibiti bei za bidhaa kama maharage na sembe, maana wazalishaji ni wale petty producers ambao hakuna jinsi ya kuwafuatilia, hawalipi kodi, na wala hawawi supported kwa namna yoyote na serikali, hivyo wanajiamulia lolote!
Kwa maoni yangu, serikali inapoongea mambo ya kilimo kwanza iwe serious, na isiishie majukwani kuwafurahisha wapenda siasa...!
Turudishe enzi za matrekta ya Massey Ferguson, Ford na Valmet, na siyo hizi Power tillers!..Huku ni kurudi nyuma kwa -50% ya ukulima kwa kisasa!