Unga na Maharage viwe na bei elekezi

bamwaiche

Member
Aug 30, 2011
50
8
Wadau inashangaza na inasikitisha kwa huyu maskini wa kitanzania kuendelea na maumivu makali ya maisha na hasa pale bei za chakula kukuu cha mtanzania kinapozidi kupanda bei siku hadi siku. Bei ya unga haishikiki, maharsge hayashikiki sisi wananchi wa hali ya kawaida tutakimbilia wapi na serikari yetu ndiyo hii. Ni kawaida kwa miaka ya 2005 kurudi nyuma bei za mazao haya zilikuwa zikishuka zenyewe wakati wavuno lakini sasa hivi haielleweki ni wakati upi ni mavuno na ni wakatai upi siyo wa mavuno. Ukweli tunaumia na hii inasabisaha taifa lenye njaa na hivyo watu hawawezi kufanya kazi kwa kiwango kianchotakiwa na kusabisha uzalishaji kupugua. taifa lenye watu wenye afya njema ndilo wakatai wote linaloendelea katika nyanja zote. Taifa na hasa JK na viongozi wake angalie namna ya kumkomboa Mtanzania. Jk ni msomi wa uchumi wa chuo kikuu cha kizalendo cha Manzese na washauri wake wa uchumi akae chini na kuangalia ni namna gani atalipatia ufumbuzi tatizo hili la kudorola kwa uchimi nchini.

Nchi yetu haina kundi la mafia ambao wanaweza kumiliki njia kuu za uchumi isipokuwa ni ulegevu wa viongozi wetu, kwani akina Mwl Nyerere hawapo tena akina Edward Moringe hawapo watetezi wa mtu wa chini.
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,208
8,686
Du!
Hii ni kali!
Unanikumbusha kipindi cha Tume ya Bei za Bidhaa, enzi za Mwalimu!

Hoja yako ni njema, nadhani unachopenda kueleza ni kuwa Serikali iwe na nguvu au mkono uliofichika katika uendeshaaji wa shughuli za biashara!
Kwa sasa mambo ni hoberahobera, kila mtu anajiamulia lake...aidha kuficha mazao na hivyo kusababisha aina fulani ya scarcity, kwa minajili ya kuuza kwa bei ya juu wakati wa mahitaji!

Kinachoshangaza ni kuwa mamlaka husika hazifuatilii matendo ya hivo, hadi waziri husika atoke ofisini na kwenda kutafuta maghala yalipo na kuuliza ni wapi mazao yameenda!....aibu!

Kwa hoja yako, ni ngumu sana kudhibiti bei za bidhaa kama maharage na sembe, maana wazalishaji ni wale petty producers ambao hakuna jinsi ya kuwafuatilia, hawalipi kodi, na wala hawawi supported kwa namna yoyote na serikali, hivyo wanajiamulia lolote!

Kwa maoni yangu, serikali inapoongea mambo ya kilimo kwanza iwe serious, na isiishie majukwani kuwafurahisha wapenda siasa...!
Turudishe enzi za matrekta ya Massey Ferguson, Ford na Valmet, na siyo hizi Power tillers!..Huku ni kurudi nyuma kwa -50% ya ukulima kwa kisasa!
 

Aza

JF-Expert Member
Feb 23, 2010
1,701
221
aisee ni kweli kabisa,ni chakula pekee nikipendacho
ila bei yake ss hivi jamani uwa najiuliza hivi tutafikia wapi na hizi bei za vyakula Tz?
izo mamlaka sijui TFDA,EWURA na nn wote ni wafu tu na nchi inaongozwa na wanandugu/mashsoti wachache
me nafikri zikizidi kupanda ivi ndipo itafikia hatua labda tutaamka na kuonyehsa kwa vitendo tumechoka
now kila mtu naona ka-relax tu,sijui wenzetu wanazo!!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom