Unemployment, layoff and redundancy advisory services

Unemployment, layoff and redundancy advisory services

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,953
Reaction score
6,727
Habari za wakati huu,

Wengi wetu tunaofanya kazi zakuajiriwa au hata biashara tunatambua kwamba kuna wakati mambo yanakuwa magumu.

Katika kipindi hiki tunajikuta tunakuwa na stress (Sonona na Msongo) huku tukihisi kwamba tunakaribia mwisho wa dunia.

Hali hii ina madhara sana na hupelekea wengine kukata tamaa na hata kujiua. Lakini pia wapo ambao kwa uwezo wa Mungu hufanikiwa kupita katika kipindi hiki kigumu na kujikuta wakiendelea na mapambano katika maisha ingawa bado hubaki na majeraha mioyoni mwao kutokana na maumivu waliyopitia katika kipindi hiki kigumu.

Kwa kutambua changamoto hio mwaka 2019 tulifanya utafiti kidogo wa kutaka kutambua iwapo kuna huduma za ushauri na unasihi wanazopewa watu wanaopitia katika kipindi kigumu hasa wakati wakiwa hawana ajira, wanaposimamisha kazi au wanapopoteza kazi.

Katika utafiti huo tuligundua kuwepo kwa uhaba mkubwa wa huduma hio huku waathirika wakiwa wengi. Tuligundua pia kwamba hata makampuni makubwa yanaposimamisha/kupunguza wafanya kazi kwa sababu yoyote ile hufanya uamuzi huo bila kujali matokeo ya maamuzi yao au kuwapa waathirika/au watakoathirika msaada wa kiushauri.

Katika utafiti huo tuligundua kwamba madhara yatokanayo na sononi/msongo wa kupoteza au kukosa ajira ni pamoja na ulevi uliokithiri, upweke, mawazo ya kujiua, maradhi ya moyo na matatizo mengine ya kiafya.

Tuligundua pia kwamba kiwango cha madhara anayopata mtu kunategemea pia nafasi yake katika kazi, kiwango cha mshahara wake, mtindo wake wa maisha, kiwango chake cha elimu, family support structure, kiwango cha unyanyapaa katika jamii yako, namna ambavyo amepoteza ajira yaka, idadi ya watu aliopoteza nao ajira n.k.

Vilevile tuligundua kwamba kutokana na sononi/msongo huo wengine hujikuta wakshinda kumudu kuendelea na maisha yao mfano hata wanapopata pesa za kufanya biashara hushindwa kufanya biashara vizuri, na hata wanapopata fursa za kupata ajira nyingine huwa wanakuwa na woga na hofu kubwa inayowapelekea kupoteza matumaini.

Kwa ujumla tuligundua kwamba idadi kubwa ya watanzania wanasumbuliwa na tatizo hili huku kukiwa hakuna mfumo wowote rasmi wa kuwapa usaidizi wa kitaalam katika kupindi hiki.

Katika utafiti huo pia tuligundua kwamba zipo namna mbalimbali za kusaidia aina hii ya watu ikiwamo ni kuwaanzishia support groups ambapo wanakutana kwa pamoja na kujadiliana na kuzungumzi changamoto zao na fursa zao ili wapate ahueni na kupeana faraja.

Katika hili ilithibitika kwamba idadi kubwa ya watu hupunguza msongo na kukataa tamaa kwa kati ya asilimia 45 hadi 75 kwa kushirika katika support groups meeting angalau mara moja kwa wiki. Namna ya pili ni kwa kuwapa pia mafunzo na taarifa za fursa za ajira na biashara kupitia katika hizo support groups. Support groups hizi zinaweza kukutanza sehemu fulani watakayochaguliwa na mratibu au hata katika makazi yao.

Namna nyingine ya kuwasaidia ni kwa kuwa na Individual private sessions na waathirika ambazo zikafanyika ama katika mfumo wa matembezi ya jioni (EVENING WALK au kwa njia ys SIMU, telephone support, au kwa mfumo wa Chat yaani messeji.

Pia unaweza kuwa na session ya kukaa kwenye eneo fulani na kuzungumza kwa kina kuhusu fursa na changamoto pamoja na matarajio.

Kwa kuwa tuliamni katika hitaji hili basi tulianza kutoa huduma hii kwa baadhi ya watu wa karibu na tumeona mafanikio makubwa. Mfumo wetu huu umesaidi baadhi ya watu kupata ajira mpya, kuendesha biashara zao vizuri na wengine kupata marafiki wapya na wanaowalewa zaidi.

Utajuaje kama una tatizo hili:

Dalili kubwa ya kuwa una tatizo hili ni tabia ya kutaka kukaa peke yako na kutokujichanganya. Unapoona umefikia hatua ya kukwepa watu, kujificha ndani muda mwingi, kulala muda mwingi, kupoteza hamu ya kula,tendo la ndoa, kuhisi watu wanakutenga na kujihisi kwamba huna thamani basi hizi ni dalili za hatari na unapaswa kutafuta msaada ili kuepuka kuingia katika hatua mbaya zaidi.

Dalili nyingini ni kuanza kuwa na mawazo ya kujiua, kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya sehemu nyingine, kuhisi umelogwa, kuanza kuchhukia watu wako wa karibu, kuanza kugombana na ndugu jamaa na marafi, kuanza kutumia vilevi na vileo, self neglection kama vile kutokuoga, kutokufua, kutokujali chochote. Hizi ni dalili mbaya zaidi na mdhara yake yanaweza kuwa makubwa kwako na kwa jamii inayokuzunguka.

Wengine hufikia hatua ya kuwa walevi chakari hasa wa vinywaji vikali kama gongo etc. Wengine hutelekeza familia zao, wengine huanza kuwa na tabia zisizokuwa salama na za hatari. Unapofikia hatua hii unahitaji msaada uchukuliwe na watu wako walioko karibu.

Pamoja na kwamba utafiti huu ulilenga zaidi katika eneo la kukosa ajira au kusimamishwa kazi lakini pili tuligundua kwamba wapo watu wengine hupata sononi kutokana na kutorodhika na aina ya kazi waliyo nayo, kiwango cha mafanikio, kiwango cha mshahara, kuyumba kwa biashara, mapenzi, na changamoto nyingine za kifamilia.

HIvyo basi kwa kutambua kwamba hili ni eneo ambalo lina athiri kwa kiasi kikubwa nguvu kazi ya taifa na kiwango cha furaha na maendelea tuko mbioni kuanzisha huduma hii ya ushauri ambayo itatolewa bure na kwa malipo kidogo kwa wale ambao wanahitaji kushirika katika support group, private session na hata mafunzo. I wapo ungependa kufahamu zaidi kuhusu huduma hii na maeneo ambapo inapatikana kwa sasa tafadhali wasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com au PM

Karibu tujadiliane kwa kina iwapo tumewahi kupitia katika kipindi kama hicho na namna ambavyo tuliathirika na kusaidika na iwapo bado tunapitia changamoto hizo.

Karibuni
 
Nimeshindwa kusoma kabisa,kama kuna mtaaramu wa kiswahili naomba anipe summary ya mile kilichoandikwa!
 
kwa ujumla ni huduma nzuri na umeielezea vizuri
ulipotaja mtu aliyepoteza ajira kwamba utamuhudumia kwa malipo kidogo hapo ndo ukakasi ulioanzia.
Najua nawe nawe hii ni ajira na yawezekana umesomea na umebobea lakini ni kama NGOMBE ALIKUWA JIKE, sasa bila kutegemea amegeuka dume, wewe unakuja na utaalamu kwamba kama unataka kuwa JIKE tena lazima unipe maziwa kwanza nikuhudumie.
USHAURI, hili ungelipenyeza vizuri kwa waajiri wangekeuwa na mfuko wa haua mambo ili mtu yakimfika anahudumiwa kwa michango iliyochango akiwa kazini
 
Back
Top Bottom