Undugu bandia ulivyonikosesha wife material

Undugu bandia ulivyonikosesha wife material

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,108
Nakumbuka wakati nimetoka nchi za mabeberu miaka kadhaa iliyopita basi kufika home kwa bi mkubwa nakutana na totozi sio mkali ni Wa kawaida fulani sema plate namba kidogo ipo, baada ya muda mchache kama miezi kadhaa nikagundua kuwa yule ni [emoji817] wife material kwa vile nilimkuta ni kama beki tatu pale kwa bi mkubwa ikapidi nimuulize vizuri bi mkubwa kwamba yule ni nani na ametokea wapi!

Nilipomuuliza bi mkubwa akanijibu yule ni ndugu yetu kabisa wa damu,kwa vile alikuwa na haraka kidogo basi mazungumzo yakaishia hapo!

Sasa ikawa kila nikijaribu kufanya u FBI kwa yule binti majibu yanakuja tu negative na mwenyewe kila nikifika home ananiita kaka kaka mara ananiomba nimsindikize dukani mara sijui nini!,lakini sema kweli nilimkubali sana alikuwa na umri mdogo lakini kichwani alikuwa vizuri kweli kweli yaani ukikaa nae muda mfupi unaenjoy!

Kwa vile muda haukua rafiki ikatokea nikaondoka tena na nilirudi baada ya miaka miwili sasa cha ajabu sikumkuta home!
Kwa vile niliambiwa ni mdogo wangu ikabidi nimuulize bi mkubwa vipi mdogo wangu ameenda wapi mbona simuoni?Bi mkubwa akaanza unajua hata sijui alienda wapi kwanza yule bibi yake walikuwa wanaishi jirani na bibi yako sasa baba yake ndio aliyemuuzia kiwanja mjomba yako sana mama yake ndio alikuwa na urafiki na bibi yako sasa mama yako mdogo ndio alikuwa anamfahamu halafu mdogo wako wa mwisho alikuwa classmate wake sasa halafu bibi yako akaniomba nije nikae nae na mjomba wako ndio anafaamiana na ndugu zake!

Yaani hadi kwa kifupi sikuelewa chochote nikaona hapa undugu hakuna nimepoteza wife material bure sasa wakati naendelea na kauchunguzi kangu cha ki FBI nakuta picha kwenye mitandao ya kijamii mshkaji kashavuta jiko tena ndoa kweli kweli na kwa sasa huyo mwanamke ni mwalimu na wamebahatika kupata mtoto mmoja!najua jamaa kapata mke kweli kweli sio bora mwanamke
 
Mtafute mwambie akuunganishe na nduguye wa kike ambaye hajaolewa...ndugu wengine huambukizana u wife material

"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
Mtafute mwambie akuunganishe na nduguye wa kike ambaye hajaolewa...ndugu wengine huambukizana u wife material

"corona ipo tuchukue tahadhari"

Maisha hayapo hivyo mkuu


Sent using IPhone X
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom