Undani wa Zitto Zubeir Kabwe

Undani wa Zitto Zubeir Kabwe

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
WanaJF

Nakumbuka ilikuwa ni mwezi Januari,2012 nilipoanza utaratibu wangu binafsi kuandika makala maalum kuhusu watu maalum hususan wanasiasa mashuhuri wa upinzani katika Tanzania.Nilianza na Freeman Mbowe mwanasiasa asiye na mfanowe katika bara hili,nikafuatia na Wilbroad Slaa(kabla hajasaliti wananchi) kisha nikamalizia kwa Tundu Lissu.Nilisimama kwa muda kuendeleza makala zile kwa sababu ambazo sitapenda kuziweka wazi.

Leo tarehe 04/11/2018 takriban miaka 7 baadaye nimeamua kurejea kuandika makala hizi na nitaanzia pale nilipoishia.

Naomba Leo nimlete kwenu mwanasiasa kijana,mahiri,mjanja na mwenye akili nyingi Zitto Zubeir Kabwe.

1.Zitto ni nani?

Jina la Zitto si geni masikioni mwa mamilioni ya watanzania.Ni wazi ukimuuliza mtu yeyote ataje wanasiasa mashuhuri watano katika Tanzania sina shaka kabisa jina la mwanasiasa huyu lazima liwe kati ya majina hayo.

Ila mimi nitajitahidi kuandika kwa uchache ninavyomfahamu

1.Zitto ni kati ya vijana walioibukia kutoka chuo kikuu cha DSM na kuamua kujipambanua katika kutetea maslahi ya wanafunzi wenzake na jamii ya Watanzania.

2.Zitto alijiunga na wapiganaji wa mageuzi wakiongozwa na Freeman Mbowe na kufanya kazi kubwa ya kuwafundisha Watanzania kuhusu elimu ya Uraia.

3.Zitto ndiye aliyewavuta vijana wengi kujiunga na Chadema hasa baada ya kufukuzwa Bungeni na Spika Sitta kuhusu Hoja ya Buzwagi.Niwe mkweli kabisa kwamba nami nilianza kupenda chama hiki kipindi hicho na nilikuwa mmoja wa vijana tulioenda kumlaki Zitto alipofukuzwa Bungeni na kuandamana naye hadi Jangwani na kuhutubia mkutano wa hadhara.Naweza kusema siku ile CDM ilizaliwa upya.

4.Zitto amekuwa mmoja wa wabunge machachari ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano kuanzia bunge la Samwel Sitta,Bunge la Anne Makinda na hata hili la sasa linaloonekana kutokuwa na mvuto kwa watu kutokana na kutokuwa na uongozi mzuri.

4.Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Zitto alisimama kidete kupigania maslahi ya wananchi na kuibua hoja mbalimbali za kuibana serikali kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.Ikumbukwe mawaziri kadhaa walijiuzulu katika bunge lililopita kutokana na Kamati ya Zitto.

5.Zitto ni kati ya wanasiasa wachache waliojitolea muda wao kusafiri maeneo mbalimbali ndani ya nchi akiwafundisha wananchi kuhusu elimu ya Uraia na kuwapa ujasiri wa kupigania maslahi yao.

6.Zitto ni mwanasiasa mjanja sana anayejua kutumia muda vizuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufanya siasa za nguvu ya Hoja.Mara nyingi watawala wameshindwa kupambana naye kwa Hoja kutokana na ukweli kwamba anapozungumza anakuwa amefanya utafiti wa kutosha na anakuwa na data za mkononi.

7.Zitto ni mwanasiasa asiyekata tamaa hasa anapokuwa anaamini katika jambo fulani.Ni muumini wa kutetea hoja na kuipigania mpaka dakika ya mwisho hata kama atabaki mwenyewe.

8.Zitto anaamini katika kusema kile anachoamini ni ukweli bila kuogopa na bila kujali anamweleza nani na wakati gani.Alimradi ni ukweli atasema

2.*Changamoto zinazomkabili*

Ni wazi mbali ya mafanikio kadhaa ya Zitto lakini ziko pia changamoto kadhaa zinazomkabili na ni vema akatizama na kushauriwa namna ya kukabiliana nazo

1.Moja ya Changamoto kubwa aliyonayo Zitto kwa sasa ni mtandao wa chama chake.ACT bado ni chama kichanga kinachohitaji kujitanua na kueneza sera zake nchini kote.Ila kwa sasa ukiitaja ACT maana yake umemtaja Zitto.Ni wazi Zitto anahitaji kuibua vipaji vingi zaidi kujiunga na chama hiki kama alivyompata Ado Shaibu kijana mahiri kabisa na anayeitendea haki nafasi yake.

2.Changamoto ya pili ni Imani ya wanamageuzi kwa Zitto.Ni ukweli ulio dhahiri katika kipindi cha kuanzia 2013/2014 Zitto alipatwa na mtihani mkubwa ndani ya Chama chake CDM.Sina haja kueleza yaliyotokea kwani kila mtu anajua hatima yake ilikuwa ni Zitto kuanzisha chama chake ACT.Kutokana na sababu hiyo kumekuwa na urafiki wa mashaka kati yake na baadhi ya magwiji wa siasa za upinzani.Kwa lugha nyingine kumekuwa na kutokuaminiana.Huu ni mtihani mkubwa kwa Zitto na anapaswa kutumia umahiri na akili zake nyingi kuhakikisha anaimarisha uhusiano wake na wanamageuzi wenzake hususan chama chake cha zamani akipendacho Chadema.

3.Changamoto ya tatu ni muungano wa Upinzani Tanzania.Ni wazi kutokana na utawala wa sasa njia pekee ya kuwaunganisha watu na kukabiliana na serikali hii ni kwa makundi kadhaa kuungana na kuwa na sauti moja.Kwa nafasi yake Zitto ni mtu muhimu sana katika kuunganisha makundi haya.Anapaswa kutafuta njia bora ya kushauriana na viongozi mahiri wa siasa za upinzani kama Freeman Mbowe,Tundu Lissu,James Mbatia,Maalim Seif Sharif Hamad na wengine.Wenzake walifika mbali na kuunda Ukawa ila kwa sasa inapaswa itafutwe njia ya kuunganisha makundi makubwa zaidi.

4.Changamoto ya nne inayomkabili Zitto ni Hulka yake.Ndiyo niseme Hulka yake.Jinsi Zitto anavyokabiliana na mambo.Zitto amekuwa ni mwepesi sana wa kuzungumza na kutenda.Wakati mwingine bila ya kupata muda wa kutosha kutafakari jambo na kushauriana kwa kina na watu.Kuna baadhi ya rafiki zake waliwahi kusema Zitto si rahisi sana kushaurika anapoamua jambo.Hii ni changamoto kubwa anayohitaji kuifanyia kazi kwa kina na kujirekebisha.Kuna wanaoamini kwamba hata yaliyotukia kipindi kile akiwa Chadema yasingetokea kama angetafakari kwa kina.

3.*Matarajio ya wengi*

1.Ni ukweli ulio wazi kwamba matarajio ya wanamageuzi na Watanzania wengi ni kwamba Zitto atatumia nafasi na ushawishi wake kuunganisha makundi kadhaa yakiwemo vyama vya siasa,wafanyakazi,makundi ya dini,Asasi zisizo za kiserikali nk katika kuunda umoja wenye nguvu kuelekea uchaguzi mkuu 2020 lengo na dhamiri kubwa ikiwa ni kupata katiba mpya itakayokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

2.Zitto anapaswa kuhakikisha kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2020 chama chake kitashirikiana na Ukawa katika kusimamisha mgombea mmoja wa Urais,mgombea mmoja wa Ubunge na mgombea mmoja wa udiwani nchini kote.

3.Ni dhahiri Zitto anatarajiwa kuendelea kusimama upande wa wenye haki na kamwe hatarubuniwa kujiunga na wanyonyaji.Na hii ilidhihirishwa na mbali ya watawala kujaribu kuivunja ACT kwa kuwachukua viongozi wake mahiri lakini Zitto ameendelea kupigana na kusimama upande wa wenye haki

4.*Imani kwa Wananchi*

Zitto amerejesha imani kwa wananchi kutokana na mambo 2 makubwa aliyofanya katika siku za karibuni

1.Kusimama kidete kupambana na utawala wa sasa wa CCM safari imbayo imeishia kwa kumpeleka mahabusu karibuni na kumfungulia mashtaka ya uchochezi.Tunaweza kusema Zitto amekuwa mwiba mkubwa kwa kuhoji utekwaji wa wananchi na kupotezwa,kupigwa risasi Tundu Lissu na ukandamizaji wa Demokrasia usio na mfano katika Taifa hili.

2.Zitto ameanza kuonyesha nia njema ya kuungana na wanamageuzi wenzake.Ni juzi tu aliunga mkono chana cha CDM kusimamisha mgombea mmoja wa Ubunge jimbo la Buyungu.Alishiriki kikamilifu kwenye kampeni ila wachunguzi wa mambo wanadai mgombea wa CDM alishinda ila aliporwa.Pia ameonekana kumtembelea na kuzungumza na mjumbe wa KK CDM Edward Lowassa kuhusu namna bora ya kukabiliana na utawala huu.Katika kuonyesha mshikamano Edward Lowassa alimtembelea Zitto alipokuwa kizuizini kituo cha polisi Mburahati ila polisi walikataa asimwone.Wachunguzi wanasema yalikuwa ni maagizo kutoka juu.

WanaJF karibuni kwa mjadala....
 
Kabla ya kuhitimisha mjadala wako hebu tupe majibu wa maswali mawili kuhusu Zitto. Moja, akiwa mwenyekiti wa PAC alikuwa analipwa milioni ngapi kila mwezi kutoka kwenye 'mashirika ya umma' yaliyokuwa yanasimamiwa na Kamati? na mbili, Sasa hivi anawajibika kwa nchi gani? Ukweli utakuweka huru.
 
Zitto kabwe ni mwansaisa kamili haswaa waliokuwa wanamuita msaliti walikuwa hawamuelwi au walikuwa wanasukumwa na utashi binafsi au ushawishi wa watu wanaowapenda na kila kukicha zitto anazidi kuwaproove wrong
 
Kabla ya kuhitimisha mjadala wako hebu tupe majibu wa maswali mawili kuhusu Zitto. Moja, akiwa mwenyekiti wa PAC alikuwa analipwa milioni ngapi kila mwezi kutoka kwenye 'mashirika ya umma' yaliyokuwa yanasimamiwa na Kamati? na mbili, Sasa hivi anawajibika kwa nchi gani? Ukweli utakuweka huru.
Onyesha ushahidi juu ya hilo Sio maneno tu ya mtaani wakt wa jakaya hata huyu magu was corrupt lkn Pima vzr ni wakati gani ambapo mwenyekt wa PAC ktk historia ya bunge la nchii hii alisimamia ipasavyo serikali na mashirika yake mpk kupelekea serikali kubadilisha mawaziri mara kadhaaa
 
Kabla ya kuhitimisha mjadala wako hebu tupe majibu wa maswali mawili kuhusu Zitto. Moja, akiwa mwenyekiti wa PAC alikuwa analipwa milioni ngapi kila mwezi kutoka kwenye 'mashirika ya umma' yaliyokuwa yanasimamiwa na Kamati? na mbili, Sasa hivi anawajibika kwa nchi gani? Ukweli utakuweka huru.
Molemo akilijibu hili najitoa JF muda huo huo!!
 
Kabla ya kuhitimisha mjadala wako hebu tupe majibu wa maswali mawili kuhusu Zitto. Moja, akiwa mwenyekiti wa PAC alikuwa analipwa milioni ngapi kila mwezi kutoka kwenye 'mashirika ya umma' yaliyokuwa yanasimamiwa na Kamati? na mbili, Sasa hivi anawajibika kwa nchi gani? Ukweli utakuweka huru.
Ebu na ww tuwekee salary slip yake aliyokua analipwa na ayo mashirika
 
Kabla ya kuhitimisha mjadala wako hebu tupe majibu wa maswali mawili kuhusu Zitto. Moja, akiwa mwenyekiti wa PAC alikuwa analipwa milioni ngapi kila mwezi kutoka kwenye 'mashirika ya umma' yaliyokuwa yanasimamiwa na Kamati? na mbili, Sasa hivi anawajibika kwa nchi gani? Ukweli utakuweka huru.
Nashangaa anamuelezea zitto wakati hamjui..historia ya zitto inaanzia sakata la buzwagi..kufukuzwa bungeni..mijadala aliyoifanya sehemu mbalimbali nchini kuhusu machimbo yakiwemo north mara, tulawaka,buzwagi na bulyanhulu..kuingizwa kwenye kamati ya madini na jk na kuacha kabisa kupiga kelele kuhusu madini..urafiki wake na kina mary yule mama wa nishati na madini aliyehongwa milioni 100 na tanpower resources hadi kufikia kuombana hela..
Kuwa mwenyekiti wa mashirika ya uma hadi kufungua kampuni ya lekadutigite na kuchukua fedha nssf.
Kuacha kwenda ufipa na kutoshiriki vikao halali vya chadema...na hatimaye kutengeneza makundi bavicha kabla hajatangaza kugombea uenyekiti..
Safari binafsi alizofanya nchi mbalimbali na jk..
IMG_20171024_145004.jpg
 
Nashangaa anamuelezea zitto wakati hamjui..historia ya zitto inaanzia sakata la buzwagi..kufukuzwa bungeni..mijadala aliyoifanya sehemu mbalimbali nchini kuhusu machimbo yakiwemo north mara, tulawaka,buzwagi na bulyanhulu..kuingizwa kwenye kamati ya madini na jk na kuacha kabisa kupiga kelele kuhusu madini..urafiki wake na kina mary yule mama wa nishati na madini aliyehongwa milioni 100 na tanpower resources hadi kufikia kuombana hela..
Kuwa mwenyekiti wa mashirika ya uma hadi kufungua kampuni ya lekadutigite na kuchukua fedha nssf.
Kuacha kwenda ufipa na kutoshiriki vikao halali vya chadema...na hatimaye kutengeneza makundi bavicha kabla hajatangaza kugombea uenyekiti..
Safari binafsi alizofanya nchi mbalimbali na jk..View attachment 921075
Kwenye hii picha Zitto he was young and Innocent!
 
Kabla ya kuhitimisha mjadala wako hebu tupe majibu wa maswali mawili kuhusu Zitto. Moja, akiwa mwenyekiti wa PAC alikuwa analipwa milioni ngapi kila mwezi kutoka kwenye 'mashirika ya umma' yaliyokuwa yanasimamiwa na Kamati? na mbili, Sasa hivi anawajibika kwa nchi gani? Ukweli utakuweka huru.
Yeye ametaja yale anayoyafahamu! Unaonaje basi wewe ukisema alikuwa analipwa shillingi ngapi?
 
Nasimamia kauli yake mwenyewe zito kuwa wanasiasa sio watu wakuamini siami mwanasiasa yoyote yule
 
Namfananisha na kiongozi mkuu wa taifa la Iran anayeihangaisha marekani na ulaya ameifanya Iran kuwa Taifa lenye nguvu kijeshi,kiuchumi,na kiteknologia,marekani hivi sasa inahangaika na vikwazo visivyotekeleka kwa ajili ya kuizuia Iran isisonge mbele,bahati mbaya imechelewa pia imesahau kama Iran toka mwaka 1979 mpaka leo inaishi na vikwazo ilivyowekewa na USA lakini bado inasonga .namuona zito kama rais baada ya raid wa kweli magufuri
 
Kabla ya kuhitimisha mjadala wako hebu tupe majibu wa maswali mawili kuhusu Zitto. Moja, akiwa mwenyekiti wa PAC alikuwa analipwa milioni ngapi kila mwezi kutoka kwenye 'mashirika ya umma' yaliyokuwa yanasimamiwa na Kamati? na mbili, Sasa hivi anawajibika kwa nchi gani? Ukweli utakuweka huru.
Kielelezo cha ujinga!
 
Back
Top Bottom