Uncle, nitafanya maajabu ukweni

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,966
Kama mtakumbuka wiki ilopita ndo nimepeleka barua ukweni japo palitokea lapsha kidogo, wengi mmenishambulia na kunitisha nimekosa mke, dua la kuku.

Barua imejibiwa twende kupanga mahali, japo mke mtarajiwa kanitonya wamejiandaa kunibana kwenye mahali iwe kama faini, wanataka wanikamue milioni 3.

Kama ilivyo kawaida nimeamua kujipanga tena kwa kuandaa majembe ambayo yamefuzu katika nyanja nzima za bargaining, jana nikaongea na jembe moja ambalo ni uncle langu.

Jembe langu likaniambia maneno haya, "uncle ondoa shaka, nitafanya maajabu, nitawashangaza pale watakapopokea mahali ndogo kuliko kawaida, kwanza nitawaanzia mbali kama vile hatutaki. Halafu kwa ustadi wa hali ya juu kabisa tutapanda nao katika reducing balance, ikibidi tutapanda nao kwa elfu tano tano, huku tukiwapa maneno matamu, mwisho watachoka na tutajikuta tunaishia kwenye laki 3 au 4.....".

Niombeeni wakuu niikamilishe hii hatua tena bila jazba kama siku ya barua, nimejifunza na nimepokea ushauri wenu japo katika hatua hii lazima pia niibuke ili kuokoa jahazi kama litakuwa linazama.
 
Nasikia siku hizi wadada wanawapatia mahali wachumba zao ili wakalipe kwao, wadada wa namna hii ina maana wanajioa na hii yako ni aina hiyo hiyo. Sasa ukishamweka ndani inabidi utulie, siku ukimuudhi au ukichepuka, utasikia ningejua nisingiku............
 
mil. 3!? Kwanza suala la kulipa mahali inabidi lije lifutwe kabisa
 
hahhhahah unaenda kuoa mbuzi au ngombe.... laki tatu!??
 
Dude, we gonna put your a.ss in our prayers.
 
sawa si vibaya ukitupiamo na vipicha vya hapa na pale..

hiyo ngumu, hapa kila mtu kajificha, wewe mwenyewe avatar ya uongo, tuendeleeni hivi hivi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…