Unbeleivable!!!Jeshi la polisi kuingilia siasa

Unbeleivable!!!Jeshi la polisi kuingilia siasa

Ranks

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Posts
2,583
Reaction score
1,098
Gari za police zinapita mitaani Arusha zikitangaza marufuku ya maandamano ya CHADEMA kesho kwa mbwembwe na vitisho lakini cha ajabu hawaongelei marufuku ya maandamano ya CCM ambapo mwanzoni walisema zuio linahusiana na mwingiliano wa maombi ya maandamano.

UKWELI WANANCHI WAMEBAKI WANACHEKA NA KUSHANGAA WAKIULIZA"KWANI WANANCHI WAKIANDAMANA KISHA WAWAUE WOTE WATAKUA WANAWATUMIKIA NANI?KWA NINI WASIACHE HOJA ZIJIBIWE NA CHAMA TAWALA??TANGU LINI WAMESAHAU YA KWAMBA WAO NI WALINZI WA RAIA NA MALI ZAO SIO WALINZI WA CHAMA TAWALA???WANANCHI WANASEMA WATATOKA WAJIONEE HUKOHUKO.
 
Mbinu ya Kibanda imegonga mwamba na sasa wameamua kutumia nguvu, hawawezi zuia mwisho wa haya yote
 
Polisi ni Nigeria kwenye ile vita ya twiter kati ya Nigeria na Kenya. Too barbaric ptuu shame on you police iyowekwa JF
 
Wananchi wana uwezo wa kuzuia udhalimu huu pindi ifikapo 2015.
 
Nimeona gari za polisi pia Mbeya na ving'ora vyao bt sijaconfirm zinaenda wapi
 
Polisi wote ni failures kwa hiyo wanafurahia vijana kufeli, hawataki aliyefanikisha hilo abughudhiwe
 
Nilikuwa naongea na Polisi mmoja jirani yangu muda mfupi uliopita, na alikuwa anasema kuwa mdogo wake aliyekuwa form 4 alipata div.4 ya point 30 kinyume na matarajio kwani hata walimu wanashangaa, na mtoto wake alimaliza darasa la saba lakini hata hana pa kumpeleka kwani hajui hata kusoma wala kuandika. Akaniambia kuwa hata kama atavaa magwanda ya polisi kesho atakuwa anatimiza wajibu tu lakini anaunga mkono maandamano asilimia 100!
 
Wananchi wana uwezo wa kuzuia udhalimu huu pindi ifikapo 2015.

Yaani kuchagua magaidi ndiyo waingie Ikulu, Watanzania si wajinga kiasi hicho dogo. 2015 mrithi wa Kikwete hatoki kwenye genge la watesaji Lenye sura ya chama cha siasa.
 
Hao polisi wamekuwaje? mbona wanaanza kukata viuno wakati ngoma bado haijapigwa?? wasubiri mdundo wa ngoma ndo wajue watakatika kwa style gani, sio tu kurukia stage wakati ngoma haijaanza kupigwa. Hicho ndo yule mukulu wa magogoni anakiita KIHEREHERE
 
Gari za police zinapita mitaani Arusha zikitangaza marufuku ya maandamano ya chadema kesho kwa mbwembwe na vitisho lakini cha ajabu hawaongelei marufuku ya maandamano ya ccm ambapo mwanzoni walisema zuio linahusiana na mwingiliano wa maombi ya maandamano.UKWELI WANANCHI WAMEBAKI WANACHEKA NA KUSHANGAA WAKIULIZA"KWANI WANANCHI WAKIANDAMANA KISHA WAWAUE WOTE WATAKUA WANAWATUMIKIA NANI?KWA NINI WASIACHE HOJA ZIJIBIWE NA CHAMA TAWALA??TANGU LINI WAMESAHAU YA KWAMBA WAO NI WALINZI WA RAIA NA MALI ZAO SIO WALINZI WA CHAMA TAWALA???WANANCHI WANASEMA WATATOKA WAJIONEE HUKOHUKO.
sijawahi kusikia polis wakipinga maandamano ya kuipongeza serikali katika taifa letu. Polis wa tanzania wanaongozwa na maccm badala ya taratibu, kanuni na sheria!
 
Yaani kuchagua magaidi ndiyo waingie Ikulu, Watanzania si wajinga kiasi hicho dogo. 2015 mrithi wa Kikwete hatoki kwenye genge la watesaji Lenye sura ya chama cha siasa.

Sasa kuna genge la uhalifu zaidi ya hili lililopo madarakani sasa hivi?? Tembo wetu wanaangamia, migodi yetu wameuza, rasilimali zetu nyingi wamegawana, sasa kuna magaidi zaidi ya hawa??
 
Hawawezi na haitatoke hata siku moja ati Serikali kutumia vyombo vya dola kuwazibiti au kuizibiti nguvu ya umma,watatuuwa kama 3 au 2 lakini tutaendelea na mapambano hadi mwisho wa siku kitaeleweka wache watangaze hapo ni kwamba wanaipandisha Chadema hata kama kulikuwa na watu ambao hawaipendi Chadema watajiuliza iweje hawa watu wanaogopwa n hata na police the wananchi watafahamu ni kutokana na nguvu za hoja wanazotoa viongozi wa Chadema za kuwatetea wananchi.

Jamani wananchi tuamke 2015 sio mbali inakuwaje watu wachache waweza kufurahia maisha kana kwamba sie tuliowengi tu wakimbizi wa kutoka Kongo au Burundi na hatuna haki,Sasa tuseme enough is enough.

Maandamano ni haki ya raia Police hana haki ya kuzuia maandamano hata serikali wa kuzuia maandamano ni MaHAKAMA tu na wao Police na serikali wanatakiwa waende Mahakamani na ushahidi kama kuna hatari kwa nchi ndio wasitishe lakini sio kienyeji kama wafanyavyo
 
Yaani kuchagua magaidi ndiyo waingie Ikulu, Watanzania si wajinga kiasi hicho dogo. 2015 mrithi wa Kikwete hatoki kwenye genge la watesaji Lenye sura ya chama cha siasa.

Kila nikisoma maoni hayo sifahamu, umekusudia waislamu ni magaidi au ?
 
Yaani kuchagua magaidi ndiyo waingie Ikulu, Watanzania si wajinga kiasi hicho dogo. 2015 mrithi wa Kikwete hatoki kwenye genge la watesaji Lenye sura ya chama cha siasa.

hilo genge linajulikana mkuu,tangu policcm wamwangosi mwandishi Chanel Ten na kisha usalama wa taifa wakamlimboka mwenyekiti wa chama cha madaktari tz bila kusahau kumwakibanda kibanda,hakika genge hlo halitamrithi kamwe kikwete.
 
sijawahi kusikia polis wakipinga maandamano ya kuipongeza serikali katika taifa letu. Polis wa tanzania wanaongozwa na maccm badala ya taratibu, kanuni na sheria!

Kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya saa 1 jioni ch.ten kwamba uongozi wa juu wa cdm wamekutana na jeshi la police na kukubaliana kusitisha maandamano ya kesho.
 
Back
Top Bottom