Mlimazunzu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2010
- 415
- 53
Duu Umenikumbusha mbali sana. Hata kampuni ya Posta walikuwa wanatudangaya - wanatuuzia airform (karatasi ya kuandikia barua ambayo ni bahasha hiyohiyo) halafu imeandikwa " ukiweka kitu chochote ndani, haitasafirishwa kwa ndege" sasa sijui vijijini ndege zilikuwa zinatua wapi?
Halafu kwenye barua unaandika ' salaam zikufikie hapo ulipo, ama baada ya salaam je u hali gani? Upendapo kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya njema hofu na mashaka ni kwako uliye mbali na upeo wa macho yangu! haa haa haa du.
mi hizo barua nakumbuka zilivyokuwa zinanizingua,
mshiko unaisha, unatuma barua nyumbani kuomba pesa wanajifanya kama hawajaipata vile dah...
demu wangu alikuwa hanitumii barua na mm simtumii tunakutana mwezi wa6 na disemba kitaa.
Halafu zilikuwepo zile Telegramu hizi zimeuwawa pia na mobile phones. shule unafundishwa kuandiha msg fupi maana kila neno linalipiwa
Masapo kunawa
Box 10
Kiwanja
Mbwa wetu mgonjwa sana
jibaba
barua zilikuwa zina raha sana nakumbuka nilikuwa najifungua masaa mawili kuandika barua na baada ya kuifunga ukishenda kuiposti unahakikisha imeingia vizuri kwenye kile kibox ili mtu hasije kusema hajaipata. Na ukishaituma tu unakuwa makini kusikiliza barua zinaposomwa shuleni na ukitajwa unafurahi kupita maelezo. Nakumbuka kuna dada mmoja alikuwa anasoma Kibosho Girls enzi hizo kibosho girls kibosho girls kweli unaambiwa nilikuwa nikipata barua yake naoga kabisa napanda kwenye double decker juu shuleni naisoma mara kumi. Kuna siku alinitumia picha yake kavaa kishati kitovu kinaonekana unaambia nilidata sikusoma siku tatu kila mwalimu akiingia darasani akiwa anaandika ubaoni mie naichungulia ile picha mpaka ukachakaa kabisa ndani ya wiki
Mnakumbuka stempu za kufoji, mtu unasugua stempu kichwani kuondoa ule muhuri wa posta halafu unaitumia stempu hiyo hiyo kumwandikia barua mtu mwingine, halafu posta wakiishtukia inarudishwa kupitia address uliyoondika
hapa naona mnasema tu, ebu mmoja atuandikie barua anayoikumbuka, iwe ameituma au ametumiwa ili angalau tukumbukie, mm kama nimesahau! ebu tumwagieni jamani
Ngoja niandike barua hapa mara moja...mhusika akiiona atajua inamhusu!!
Lizzy
AYT(anuani ya tovuti) JF
Tanzania
Mpendwa MM,
Dhumuni la barua hii ni kutaka kukupa jibu la ombi lako ulilonifikishia takiribani mwezi sasa.Ila kwanza naomba unijulie hali yako ili nipate amani na furaha moyoni kusikia u mzima wa afya.Binafsi si mgonjwa ila upweke unanitawala kwa kutoweza kukutia machoni kila uwapo mawazoni mwangu.
Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.Siwezi kusema nilikupenda ghafla maana ntakua nakudanganya na ninajidanganya pia.Lakini kadiri siku zinavyokimbia ndivyo moyo wangu hua unaongezeka mapigo pale nisikiapo kutoka kwako.Naomba nikwambie ukweli kwamba uliponitamkia mara ya kwamba wanipenda nilishangaa sana maana sikutegemea maneno yale ndani ya kipindi kifupi tu ulichopata kunifahamu.Taratibu nilianza kukuelewa na kuamini kwamba inawezekana maana mapenzi hayapangiliwi.
Baada ya kuchukua muda wangu kukusoma na kukufahamu nimeamua na ningependa kuwa wako mpenzi au hata mkeo huko mbeleni kama nia yako ni thabiti.Nakubali kwasababu nimegundua u mwanaume mzuri mwenye heshima kwa watu na pia mwenye kujiheshimu...mwenye mapenzi na mwenye kujali...mwenye sauti ya kuremba masikio yangu kama kinanda kinachopigwa kwa ujuzi na pia mwenye kujituma.Naahidi ntakua nawe bega kwa bega iwe kwa shida na raha...ntakupenda kwa moyo wangu wote bila kusahau kukuheshimu wewe na mawazo yako.
Natumai barua hii itakuacha mwenye furaha hata kama ilikukuta na huzuni.Naomba utabasamu kwaajili yangu japo sikuoni furaha yako ni yangu pia.Nakupenda sana ewe mfalme wa moyo wangu na ninatumai nitabaki kua malkia na mtawala pekee wa moyo wako.
Wako akupendae Lizzy!
PS
Asante sana kwa nauli ntajitahidi pindi nipatapo nafasi nije mjini kukuona.Natamani sana kuhisi joto lako na mikono yako ikinizunguka.Niyaone macho yako ukiniambia unanipenda pia kuninongoneza yaliyo moyoni mwako.ALAFU JIANDAE KULA CHAKULA KIZURI NTAKAPOKUJA...NDIZI UZIPENDAZO NTAKUJA NAZO MWENYEWE.
Kwaheri kwa sasa!
Enzi zile ilikuwa raha sana, ajabu siku hizi wanafanya watoto wetu wa miaka chini ya kumi, ndio utakuta kaandika kibarua kakamatwa shuleni mzazi eti unaitw a ukamkanye mtotoBarua unalala nayo unaamka usiku wa manane unasoma tena, wenye machozi ya karibu linakutoka tu bila sababu
kama nakuona enzi hizo migombani, hii lazima pages 5 zinaisha na ukiwa unaandika shingo umeilazia pembeni kwa jinsi unavojisikiaNgoja niandike barua hapa mara moja...mhusika akiiona atajua inamhusu!!
Lizzy
AYT(anuani ya tovuti) JF
Tanzania
Mpendwa MM,
Dhumuni la barua hii ni kutaka kukupa jibu la ombi lako ulilonifikishia takiribani mwezi sasa.Ila kwanza naomba unijulie hali yako ili nipate amani na furaha moyoni kusikia u mzima wa afya.Binafsi si mgonjwa ila upweke unanitawala kwa kutoweza kukutia machoni kila uwapo mawazoni mwangu.
Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.Siwezi kusema nilikupenda ghafla maana ntakua nakudanganya na ninajidanganya pia.Lakini kadiri siku zinavyokimbia ndivyo moyo wangu hua unaongezeka mapigo pale nisikiapo kutoka kwako.Naomba nikwambie ukweli kwamba uliponitamkia mara ya kwamba wanipenda nilishangaa sana maana sikutegemea maneno yale ndani ya kipindi kifupi tu ulichopata kunifahamu.Taratibu nilianza kukuelewa na kuamini kwamba inawezekana maana mapenzi hayapangiliwi.
Baada ya kuchukua muda wangu kukusoma na kukufahamu nimeamua na ningependa kuwa wako mpenzi au hata mkeo huko mbeleni kama nia yako ni thabiti.Nakubali kwasababu nimegundua u mwanaume mzuri mwenye heshima kwa watu na pia mwenye kujiheshimu...mwenye mapenzi na mwenye kujali...mwenye sauti ya kuremba masikio yangu kama kinanda kinachopigwa kwa ujuzi na pia mwenye kujituma.Naahidi ntakua nawe bega kwa bega iwe kwa shida na raha...ntakupenda kwa moyo wangu wote bila kusahau kukuheshimu wewe na mawazo yako.
Natumai barua hii itakuacha mwenye furaha hata kama ilikukuta na huzuni.Naomba utabasamu kwaajili yangu japo sikuoni furaha yako ni yangu pia.Nakupenda sana ewe mfalme wa moyo wangu na ninatumai nitabaki kua malkia na mtawala pekee wa moyo wako.
Wako akupendae Lizzy!
PS
Asante sana kwa nauli ntajitahidi pindi nipatapo nafasi nije mjini kukuona.Natamani sana kuhisi joto lako na mikono yako ikinizunguka.Niyaone macho yako ukiniambia unanipenda pia kuninong‘oneza yaliyo moyoni mwako.ALAFU JIANDAE KULA CHAKULA KIZURI NTAKAPOKUJA...NDIZI UZIPENDAZO NTAKUJA NAZO MWENYEWE.
Kwaheri kwa sasa!
kama nakuona enzi hizo migombani, hii lazima pages 5 zinaisha na ukiwa unaandika shingo umeilazia pembeni kwa jinsi unavojisikiaNgoja niandike barua hapa mara moja...mhusika akiiona atajua inamhusu!!
Lizzy
AYT(anuani ya tovuti) JF
Tanzania
Mpendwa MM,
Dhumuni la barua hii ni kutaka kukupa jibu la ombi lako ulilonifikishia takiribani mwezi sasa.Ila kwanza naomba unijulie hali yako ili nipate amani na furaha moyoni kusikia u mzima wa afya.Binafsi si mgonjwa ila upweke unanitawala kwa kutoweza kukutia machoni kila uwapo mawazoni mwangu.
Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.Siwezi kusema nilikupenda ghafla maana ntakua nakudanganya na ninajidanganya pia.Lakini kadiri siku zinavyokimbia ndivyo moyo wangu hua unaongezeka mapigo pale nisikiapo kutoka kwako.Naomba nikwambie ukweli kwamba uliponitamkia mara ya kwamba wanipenda nilishangaa sana maana sikutegemea maneno yale ndani ya kipindi kifupi tu ulichopata kunifahamu.Taratibu nilianza kukuelewa na kuamini kwamba inawezekana maana mapenzi hayapangiliwi.
Baada ya kuchukua muda wangu kukusoma na kukufahamu nimeamua na ningependa kuwa wako mpenzi au hata mkeo huko mbeleni kama nia yako ni thabiti.Nakubali kwasababu nimegundua u mwanaume mzuri mwenye heshima kwa watu na pia mwenye kujiheshimu...mwenye mapenzi na mwenye kujali...mwenye sauti ya kuremba masikio yangu kama kinanda kinachopigwa kwa ujuzi na pia mwenye kujituma.Naahidi ntakua nawe bega kwa bega iwe kwa shida na raha...ntakupenda kwa moyo wangu wote bila kusahau kukuheshimu wewe na mawazo yako.
Natumai barua hii itakuacha mwenye furaha hata kama ilikukuta na huzuni.Naomba utabasamu kwaajili yangu japo sikuoni furaha yako ni yangu pia.Nakupenda sana ewe mfalme wa moyo wangu na ninatumai nitabaki kua malkia na mtawala pekee wa moyo wako.
Wako akupendae Lizzy!
PS
Asante sana kwa nauli ntajitahidi pindi nipatapo nafasi nije mjini kukuona.Natamani sana kuhisi joto lako na mikono yako ikinizunguka.Niyaone macho yako ukiniambia unanipenda pia kuninongoneza yaliyo moyoni mwako.ALAFU JIANDAE KULA CHAKULA KIZURI NTAKAPOKUJA...NDIZI UZIPENDAZO NTAKUJA NAZO MWENYEWE.
Kwaheri kwa sasa!
Hahaha bahati mbaya sikupata hiyo bahati....ndo nimelipazia hapa!kama nakuona enzi hizo migombani, hii lazima pages 5 zinaisha na ukiwa unaandika shingo ueilazia pembeni kwa jinsi unavojisikia