Unawezaje kutokuwa na maelewano mazuri na wazazi wako kisa mke?

Hadi hapo kwenye 3mil nikajua uongo huu.
Wazazi wana sehemu zao
Wake wana sehemu zao katika kujenga familia yako. Familia yako ni yako na yenu haikuhusu sana. Ile ni familia ina kiongozi wake. Wewe ukiruhusu ile familia iingilie yako hutafanikiwa kupata familia bora.
 
Mama na baba yangu, kweli itokee mwanamke afanye nisielewane na nyie? umbali wangu kwenu haizidi km20 lakini mnanipigia kila mara kutaka kujua naendeleaje zaidi ya mimi ninavyowapigia.... nakumbuka mlivyopigika kunisomesha hata hamkutaka nisome kayumba school kuanza chekechea mpaka form six na chuo hamkataka kusikia nasoma kwa mkopo wa serikali ......MUNGU AWAPE MAISHA MAREFU MY HEROES
Nasema kama sitompata mwanamke wa kuendana na wazazi na familia yangu bora nipige tu then nibaki bachela
Baba lina
Mbona unanikumbushia huu wajibu kila siku😢
 
Pande zote mbili za wazazi pamoja na ndugu huweza kukosea pia..

Binafsi Navyomjua mama yangu jinsi alivyo mpole asiye na makuu na alivyo mcha mungu siku zote namuombea a pate mkwe wa kufanana nae ikiwa hakijatimia kile nikiombacho basi daima nitasimama na mama hata hvyo sioni kama wazazi wanaweza ruhusu mgongano kati yao na mkwe wao.
 
Mimi hawa watu wanaoendekeza undugu sijawahi wakubali. Wanachukulia wwnawake ka accessories wakati hata mama zao nao walikuwa wanawake.
Mimi siku zote naamini mke ana sehemu yake na mama a nayo yake. Sitaki waingiliane kwenye maamuzi. Mke asinishauri kuhusu Mama na Mama asinishauri kuhusu Mke.
Yupo sahihi machoni kwako tuu au machoni mwa kila mtu?
 
Tatizo kila mtu anataka ingilia sehemu ya mwenzake
Mama anataka ingilia sehemu ya Mke na Mke anataka ingilia sehemu ya Mama. Wanatakiwa wajue majukumu yao.
Mama alizaa
Mke ananizalia kutengeneza familia.
Mungu alisema tuongozane na wake zetu
 
Nimepitia baadhi ya thread humu ndani zinazungumzia masuala ya ndoa na changamoto
zake , nimeshtushwa na jinsi baadhi ya vijana ambavyo kwa uchangiaji wao inaonekana kabisa wako tayari kutofautiana na wazazi wao kisa mke..na kwa upande wa wanawake wao wanaonesha waziwazi namna ambavyo wanaona ndugu wa mwanaume ni kama mzigo kwao. ni kweli mke anaweza kukutenganisha na wazazi wako?. Aisee sitaki kuamini kama kuna vijana wapo wa namna hii

Kiukweli Alikiba na Diamond pamoja na kuwa na madhaifu yao linapokuja suala la wazazi wao ni watu ambao napenda kujifunza kutoka kwao, Binafsi nimeoa huu ni mwaka wa tano, linapokuja suala la kifamilia na wazazi huwa sijiulizi mara mbili, ni lazma litatuliwe na kuhakikisha furaha ya wazazi na wadogo zangu inakuwepo mda wote, YES .. nampenda mke wangu nampenda sana tu na watoto wangu wawili tuliobarikiwa, na nafanya majukumu yote kama baba na nilishamwambia mke wangu kwamba " mimi sijaoa degree yako nimekuoa ili tujenge familia ambayo itatufanya kupata usalama na utulivu wa akili,nimekuoa kama mwenzi wa maisha ambaye tutaweza kushirikiana nawe katika furaha na huzuni" Lakini haimaanishi kuwa wazazi wangu watakuwa hawana nafasi kwangu.

Mke wangu nilimpata chuoni kipindi namaliza chuo yeye ndio anaanza, wote bado vijana tumepishana miaka 3.. ikiwa yeye ana 28 sasa, na tangu mwanzo wa mahusiano yetu nilimwambia wazi wazi kwamba ni bora usioneshe kunipenda mimi lakini uiipende familia yangu hapo tutaweza kuishi lakini ukinipenda na ukaichukia familia yangu wakiwemo wazazi haitatokea nikawa na wewe kama mke, na sitokuwa na sababu ya kukuoa

MKASA WA MKE WANGU ULIOPELEKEA KUTAKA KUMUACHA KAMA SI MAMA YANGU KUINGILIA.

Mimi ni engineer, majukumu ya kazi zangu yananifanya nakuwa nasafiri mikoani mara kwa mara hivyo mda mwingi nakuwa mbali na mke na watoto wangu. Katika maisha yetu ya ndoa wazazi na ndugu zake mke wangu nawapenda sana kama unavyojua ni mara chache mwanaume kuchukia ndugu wa kike wengi huwa tunataka sifa zetu ziwe nzuri upande huo, hata mimi pia nilijitahidi kusaidia pale nilipomudu na hakika tulishibana sana na mashemeji hata wazazi wake walinipenda sana, mke wangu naye alionesha kuwapenda wazazi wangu sana na dada zangu kiasi kwamba ni vigumu mgeni kuweza kujua kwamba kama ni mke ukiwakuta kwa pamoja unaweza kusema ni mtu na dada zake.. wazazi wangu nao walimpenda sana mke wangu, walimchukulia kama mtoto wa familia yetu hata kama mambo mengine alikuwa anashirikishwa hata bila mimi kufahamu.

Mwaka juzi mwezi december nikawa niko likizo, nikawaita mama yake na mama yangu waje watusalimie na kuwaona wajukuu wao, na kweli walikuja kwa bahati mbaya ikatokea dharula kazini nikapigiwa simu natakiwa kukatiza likizo nisafiri mikoani kwa mda wa wiki 2.. nikawajulisha wazazi wakanitakia safari njema na wakaniambia sitoweza kuwakuta kwamba walikuja kutujulia hali tu hivyo wanahitaji kurudi kuendelea na majukumu mengine, pamoja na kuwakatalia wakagoma, ilibidi kabla sijasafiri niangalie namna ya wale wazee watakavyorudi makwao... Nikamkabidhi mke wangu pesa za ticketi ya ndege kwa kila mmoja kipindi watakapoondoka wapande usafiri huo na kiasi taslimu cha pesa 3m wapewe kama zawadi yangu, sikuwa na mashaka na mke wangu nilijua atawagawanyishia sawasawa, kesho yake nikasafiri. nadhani mke wangu hapa alitaka kunipima upepo wakati mimi nilikuwa tayari nimeshamuamini na nilikuwa sijawahi kumkoromea tangu niwe nae.

Ilifika siku wakasifiri hawa wazazi wetu na nikawa nawasiliana nao mpaka walipofika airport, nilishtushwa pale mama yangu aliponipigia simu ya kunishuru katika maongezi yale ambayo alimsifia sana mke wangu na kuniambia nimepata mke haswa na kumshukuru sana kwamba alimpatia kiasi cha laki tisa ( Tsh 900,000/=) za ziada kwa ajili ya kuondoka nazo, nilishtuka japo sikutaka kumuonesha mama ajue mda ule niko tofauti.., baada ya kumaliza kuongea na mama kichwa kikawaka vibaya ina maana huyu mwanamke mama yake kampa 2.1m na lazma yeye atakuwa amemuongezea za kwake, mama yangu anampa laki tisa kweli..., ile kazi kule mikoani nikaona ngumu kwangu ilipoisha niliporudi nyumbani nikamkuta yupo na dada yake ambaye ni shemeji yangu,... Ile siku dada yake hakuweza kuamini kwamba yule anayemuona mbele yake ni mimi aliyekuwa amenizoea siku zote nilikuwa zaidi ya kichaa , sikutaka hata walale kwangu yeye na dada yake usiku ule niliwafukuza niliwasha moto ambao ni vigumu kuuelezea hapa nikawapa nauli, sikujua walilala wapi usiku ule, kesho yake walipanda basi wakarudi kwao.

Wazazi wake wakanipigia sana simu kutaka kujua chanzo ni nini, niliwaambia wamuulize mwenyewe tena wala sikuwaonea aibu kama mwanzo na mimi kosa hili tu lilitosha kabisa kumfukuza huyu mwanamke, sikutaka tena kuishi nae. Haya yote niliyafanya bila wazazi wangu kufahamu na sikuwaambia chochote kinachoendelea. Baada ya wazazi wake huyu mwanamke kuona nimegoma kabisa hata kuitikia vikao vyao ikabidi wawaambie wazazi wangu, Ilibidi washtuke maana walijua naishi na mke wangu wakanipigia simu nilipopokea wakaanza kunitukana wakijua mimi lazma nitakuwa mkorofi maana mke wangu anaonekana mpole sana na kila waliponiuliza chanzo niliwaambia wamuulize mwenyewe, walijiongeza wao wazazi wakaandaa kikao kikafanyika nyumbani kwetu kwa wazazi akiwepo na mke wangu mimi sikuwepo akawaambia ukweli kilichotokea.

wazazi wakanipigia wakanielezea jinsi mke wangu alivyokiri kosa na kuomba msamaha, mama yangu akaniambia yule ndio mke anaemtambua ni lazma nimrudishe kwa vyovyote vile la sivyo nisimtambue yeye kama mama yangu ...nilimrudisha niko nae mpaka sasa cha kushangaza yale mazoea ya karibu yaliyokuwepo kati ya mimi na mashemeji zangu hayapo sasa wanakuwa kama wananiogopa vile, hata mama mkwe kawa muoga sana tofauti na zamani... but huwa sisiti kusaidia kwao ninapoweza.

Pamoja na kwamba Baba yangu ana matatzo yake lakini sihitaji mke wangu kwa namna yeyote adharau familia yangu niliyotoka.
ukiona unakubali kutengana na familia yako kwa sababu ya mke wewe ni zaidi ya MUME BWEGE, na mke wako akishajua hivi atakuendesha anavyotaka ,.. Utabaki jina tu kwamba ni mume ila maamuzi atakuwa nayo yeye
wewe mwenyewe ulizingua. Hakukuwa na sababu ya kuzipitisha hizo hela kwa mke wako. Ulishindwa nini kuwapa mwenyewe.
 
Pande zote mbili za wazazi pamoja na ndugu huweza kukosea pia..

Binafsi Navyomjua mama yangu jinsi alivyo mpole asiye na makuu na alivyo mcha mungu siku zote namuombea a pate mkwe wa kufanana nae ikiwa hakijatimia kile nikiombacho basi daima nitasimama na mama hata hvyo sioni kama wazazi wanaweza ruhusu mgongano kati yao na mkwe wao.
Sasa ukisema apate mkwe wa kufanana nae inamana mkeo na mama yako watakua wanaishi pamoja.Mi naona kila mmoja aishi nafasi yake.Wazazi wapewe heshima wanayostahili kama wazazi.
 
Duuh,nikweli hakufuata masharti yako na tunawapenda Mama zetu hasa sisi ambao tuna Baba-mama (single parent family) ambao wametutoa mbali sana

Kwa akili yangu na elimu yangu ya Ngumbalu,nadhani ungeongea na mkewako Private room angeweza kukiri na kukwambia mume wangu halitajirudia tena na angekupa sababu maybe maana si shida zote za familia yake atakwambia na angepata confidence zaidi kushare nawewe mambo mengi kwasiku za usoni

Kumfukuza,kwanza ulimdhalilisha mtu anayekuzalia watoto,ulimdharau mkeo,mkeo hukumthamini tena na inaonyesha vile vimesaada unavyowasaidia ulitumia kama fimbo ya kuwachapia yeye nadada yake wakati unahasira jambo ambalo nikosa kubwa sana.

Madhara.
Umesema ile intimacy iliyokuwepo imepungua toka kwa shemeji zako,nikweli nikutokana na maneno uliyosema wakati na Dada yake yupo,so aliwaambia ndugu zake hawana hamu nawewe tena

Mkeo atakuwa anakuogopa hana amani tena maana hukumlinda (ulitakiwa uongee naye)

Hana mapenzi tena kwako inatakiwa update upya,siyo umuombe radhi ila onyesha kuwa unajutia namna ulivyomtimua kama mbwa koko.

Ushauri.
Jaribu kila jambo kufikiria kwa muda kabla ya kuchukua hatua

Mfanye mkeo rafiki,awe huru nawewe,akiwa stressed akimbilie kwako kupata ushauri bora

Mwisho
Muombeni sana Mungu ataendelea kuibariki ndoa yenu
 
Kama asipouelewa huu ushauri ndo basi tena. Ndo maana mama yake jamaa kaona kosa la kidwanzi.
Duuh,nikweli hakufuata masharti yako na tunawapenda Mama zetu hasa sisi ambao tuna Baba-mama ambao wametutoa mbali sana

Kwa akili yangu na elimu yangu ya Ngumbalu,nadhani ungeongea na mkewako Private room angeweza kukiri na kukwambia mume wangu halitajirudia tena na angekupa sababu maybe maana si shida zote za familia yake atakwambia na angepata confidence zaidi kushare nawewe mambo mengi kwasiku za usoni

Kumfukuza,kwanza ulimdhalilisha mtu anayekuzalia watoto,ulimdharau mkeo,mkeo hukumthamini tena na inaonyesha vile vimesaada unavyowasaidia ulitumia kama fimbo ya kuwachapia yeye nadada yake wakati unahasira jambo ambalo nikosa kubwa sana.

Madhara.
Umesema ile intimacy iliyokuwepo imepungua toka kwa shemeji zako,nikweli nikutokana na maneno uliyosema wakati na Dada yake yupo,so aliwaambia ndugu zake hawana hamu nawewe tena

Mkeo atakuwa anakuogopa hana amani tena maana hukumlinda (ulitakiwa uongee naye)

Hana mapenzi tena kwako inatakiwa update upya,siyo umuombe radhi ila onyesha kuwa unajutia namna ulivyomtimua kama mbwa koko.

Ushauri.
Jaribu kila jambo kufikiria kwa muda kabla ya kuchukua hatua

Mfanye mkeo rafiki,awe huru nawewe,akiwa stressed akimbilie kwako kupata ushauri bora

Mwisho
Muombeni sana Mungu ataendelea kuibariki ndoa yako
 
Sasa ukisema apate mkwe wa kufanana nae inamana mkeo na mama yako watakua wanaishi pamoja.Mi naona kila mmoja aishi nafasi yake.Wazazi wapewe heshima wanayostahili kama wazazi.
Hakuna mahali niliposema wataishi pamoja unajua wanaweza wasiwe wanaishi pamoja lakini tofauti ikawepo pia..
 
Ila wanawake tuna taabu jamani. Hatutakiwi kukosea, tukikosea tunasimwangwa na dunia nzima.

Kuna msemo wao wanaupenda hawa viumbe "mke sio ndugu yako" ila cha ajabu wao wanataka uwafanye wao wawe zaidi ya ndugu na ni lazima kuwapenda ndugu zake hata kama wana matatizo.

Ndoa zimekuwa kitu cha ajabu kweli siku hizi
 
Mamii nimekumbuka ule uzi wa mwananke mfanya kazi ulipoongelea kuhusu kuwasaidia wazazi na ndugu zako ulivyovamiwa na comments za povu. Ila hapa naona mambo ni toauti
Hapa ni tofauti kabisa.
Niliambiwa nikishaolewa nisahau habari za kuwasaidia wazazi wangu nideal na mume wangu na watoto. .

Kumbe kuna watu ili wakuoe kigezo cha kwanza ni lazima kupenda wazazi na ndugu wa mume.
 
Back
Top Bottom