Unawezaje kutokuwa na maelewano mazuri na wazazi wako kisa mke?

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,716
3,233
Nimepitia baadhi ya thread humu ndani zinazungumzia masuala ya ndoa na changamoto
zake , nimeshtushwa na jinsi baadhi ya vijana ambavyo kwa uchangiaji wao inaonekana kabisa wako tayari kutofautiana na wazazi wao kisa mke..na kwa upande wa wanawake wao wanaonesha waziwazi namna ambavyo wanaona ndugu wa mwanaume ni kama mzigo kwao. ni kweli mke anaweza kukutenganisha na wazazi wako?. Aisee sitaki kuamini kama kuna vijana wapo wa namna hii

Kiukweli Alikiba na Diamond pamoja na kuwa na madhaifu yao linapokuja suala la wazazi wao ni watu ambao napenda kujifunza kutoka kwao, Binafsi nimeoa huu ni mwaka wa tano, linapokuja suala la kifamilia na wazazi huwa sijiulizi mara mbili, ni lazma litatuliwe na kuhakikisha furaha ya wazazi na wadogo zangu inakuwepo mda wote, YES .. nampenda mke wangu nampenda sana tu na watoto wangu wawili tuliobarikiwa, na nafanya majukumu yote kama baba na nilishamwambia mke wangu kwamba " mimi sijaoa degree yako nimekuoa ili tujenge familia ambayo itatufanya kupata usalama na utulivu wa akili,nimekuoa kama mwenzi wa maisha ambaye tutaweza kushirikiana nawe katika furaha na huzuni" Lakini haimaanishi kuwa wazazi wangu watakuwa hawana nafasi kwangu.

Mke wangu nilimpata chuoni kipindi namaliza chuo yeye ndio anaanza, wote bado vijana tumepishana miaka 3.. ikiwa yeye ana 28 sasa, na tangu mwanzo wa mahusiano yetu nilimwambia wazi wazi kwamba ni bora usioneshe kunipenda mimi lakini uiipende familia yangu hapo tutaweza kuishi lakini ukinipenda na ukaichukia familia yangu wakiwemo wazazi haitatokea nikawa na wewe kama mke, na sitokuwa na sababu ya kukuoa

MKASA WA MKE WANGU ULIOPELEKEA KUTAKA KUMUACHA KAMA SI MAMA YANGU KUINGILIA.

Mimi ni engineer, majukumu ya kazi zangu yananifanya nakuwa nasafiri mikoani mara kwa mara hivyo mda mwingi nakuwa mbali na mke na watoto wangu. Katika maisha yetu ya ndoa wazazi na ndugu zake mke wangu nawapenda sana kama unavyojua ni mara chache mwanaume kuchukia ndugu wa kike wengi huwa tunataka sifa zetu ziwe nzuri upande huo, hata mimi pia nilijitahidi kusaidia pale nilipomudu na hakika tulishibana sana na mashemeji hata wazazi wake walinipenda sana, mke wangu naye alionesha kuwapenda wazazi wangu sana na dada zangu kiasi kwamba ni vigumu mgeni kuweza kujua kwamba kama ni mke ukiwakuta kwa pamoja unaweza kusema ni mtu na dada zake.. wazazi wangu nao walimpenda sana mke wangu, walimchukulia kama mtoto wa familia yetu hata kama mambo mengine alikuwa anashirikishwa hata bila mimi kufahamu.

Mwaka juzi mwezi december nikawa niko likizo, nikawaita mama yake na mama yangu waje watusalimie na kuwaona wajukuu wao, na kweli walikuja kwa bahati mbaya ikatokea dharula kazini nikapigiwa simu natakiwa kukatiza likizo nisafiri mikoani kwa mda wa wiki 2.. nikawajulisha wazazi wakanitakia safari njema na wakaniambia sitoweza kuwakuta kwamba walikuja kutujulia hali tu hivyo wanahitaji kurudi kuendelea na majukumu mengine, pamoja na kuwakatalia wakagoma, ilibidi kabla sijasafiri niangalie namna ya wale wazee watakavyorudi makwao... Nikamkabidhi mke wangu pesa za ticketi ya ndege kwa kila mmoja kipindi watakapoondoka wapande usafiri huo na kiasi taslimu cha pesa 3m wapewe kama zawadi yangu, sikuwa na mashaka na mke wangu nilijua atawagawanyishia sawasawa, kesho yake nikasafiri. nadhani mke wangu hapa alitaka kunipima upepo wakati mimi nilikuwa tayari nimeshamuamini na nilikuwa sijawahi kumkoromea tangu niwe nae.

Ilifika siku wakasifiri hawa wazazi wetu na nikawa nawasiliana nao mpaka walipofika airport, nilishtushwa pale mama yangu aliponipigia simu ya kunishuru katika maongezi yale ambayo alimsifia sana mke wangu na kuniambia nimepata mke haswa na kumshukuru sana kwamba alimpatia kiasi cha laki tisa ( Tsh 900,000/=) za ziada kwa ajili ya kuondoka nazo, nilishtuka japo sikutaka kumuonesha mama ajue mda ule niko tofauti.., baada ya kumaliza kuongea na mama kichwa kikawaka vibaya ina maana huyu mwanamke mama yake kampa 2.1m na lazma yeye atakuwa amemuongezea za kwake, mama yangu anampa laki tisa kweli..., ile kazi kule mikoani nikaona ngumu kwangu ilipoisha niliporudi nyumbani nikamkuta yupo na dada yake ambaye ni shemeji yangu, nikamuuliza ilitokea nini mpaka ikawa vile akawa hawana majibu zaidi ya kupanick na kunijibu majibu ya kishenzi kwa sauti ya jazba ... Ile siku dada yake hakuweza kuamini kwamba yule anayemuona mbele yake ni mimi aliyekuwa amenizoea siku zote nilikuwa zaidi ya kichaa , sikutaka hata walale kwangu yeye na dada yake usiku ule niliwafukuza niliwasha moto ambao ni vigumu kuuelezea hapa nikawapa nauli, sikujua walilala wapi usiku ule, kesho yake walipanda basi wakarudi kwao.

Wazazi wake wakanipigia sana simu kutaka kujua chanzo ni nini, niliwaambia wamuulize mwenyewe tena wala sikuwaonea aibu kama mwanzo na mimi kosa hili tu lilitosha kabisa kumfukuza huyu mwanamke, sikutaka tena kuishi nae. Haya yote niliyafanya bila wazazi wangu kufahamu na sikuwaambia chochote kinachoendelea. Baada ya wazazi wake huyu mwanamke kuona nimegoma kabisa hata kuitikia vikao vyao ikabidi wawaambie wazazi wangu, Ilibidi washtuke maana walijua naishi na mke wangu wakanipigia simu nilipopokea wakaanza kunitukana wakijua mimi lazma nitakuwa mkorofi maana mke wangu anaonekana mpole sana na kila waliponiuliza chanzo niliwaambia wamuulize mwenyewe, walijiongeza wao wazazi wakaandaa kikao kikafanyika nyumbani kwetu kwa wazazi akiwepo na mke wangu mimi sikuwepo akawaambia ukweli kilichotokea.

wazazi wakanipigia wakanielezea jinsi mke wangu alivyokiri kosa na kuomba msamaha, mama yangu akaniambia yule ndio mke anaemtambua ni lazma nimrudishe kwa vyovyote vile la sivyo nisimtambue yeye kama mama yangu ...nilimrudisha niko nae mpaka sasa cha kushangaza yale mazoea ya karibu yaliyokuwepo kati ya mimi na mashemeji zangu hayapo sasa wanakuwa kama wananiogopa vile, hata mama mkwe kawa muoga sana tofauti na zamani... but huwa sisiti kusaidia kwao ninapoweza.

Pamoja na kwamba Baba yangu ana matatzo yake lakini sihitaji mke wangu kwa namna yeyote adharau familia yangu niliyotoka.
ukiona unakubali kutengana na familia yako kwa sababu ya mke wewe ni zaidi ya MUME BWEGE, na mke wako akishajua hivi atakuendesha anavyotaka ,.. Utabaki jina tu kwamba ni mume ila maamuzi atakuwa nayo yeye
 
Alitoa sababu gani kwenye huo mgawanyisho wa fedha?
Yawezekana hakumpa mama yake 2.1M.
Yawezekana alispend kwa matumizi mengine pengine na hao hao wazazi japo hayakuwa makubaliano.
Amefanya makosa hata hivo.
.
NYONGEZA.
Nitapate mwanaume wa kunipiga mkwara wa kipuuzi kama wewe ''eti usipowapenda wazazi wangu sijui nini...." Siwezi kukubali kuolewa nae.
Si kwa sababu sitowapenda wazazi wake bali ni kwa sababu anaonekana kuitanguliza familia yake mbele zaidi ya familia ambayo naenda kuanzisha nae.
.
Atakuwa tayari ana silaha yake ya "usipompenda mama yangu ondoka" kupishana kwenye maisha ipo sana, mtu anapishana na mama yake mzazi hata mwaka hawana maelewano sembuse "mama mkwe"?.
Nitampenda mama yako kama ninavyowapenda wazazi wangu , nitamheshimu kama wazazi wangu ila kuwekewa hiyo kama sheria ya kuishi na wewe ni kuniona nina uchungu wa kuolewa na wewe sana.
 
nilitoa pesa zote za matumizi muhimu, hii ilikuwa pembeni kabisa kwa ajili ya pesa zao za kuanzia huko kijijini na ni ukweli alimpa mama yake zaidi ya 2.1m, na mimi sio lazma nioe kama wewe unatafuta unaowamudu,.. Kwangu usipoipenda familia yangu huna nafasi kwangu
 
nilitoa pesa zote za matumizi muhimu, hii ilikuwa pembeni kabisa kwa ajili ya pesa zao za kuanzia huko kijijini na ni ukweli alimpa mama yake zaidi ya 2.1m, na mimi sio lazma nioe kama wewe unatafuta unaowamudu
Alifanya makosa basi.
Endelea kutumia familia yako kama kipimo cha kumpima mke wako na usahau kabisa mke wako anatakiwa akupende wewe na sio familia yako.
 
unaweza kuwa umenipita umri au ukawa mdogo kwangu lakini kwa ulichokifanya kama ni kweli then unakuja kijisifia nbelw ya watu wala hukufanya jambo zuri hata kwani lilikuwa ni jambo la kumwita tu mkeo chumbani na kuyamaliza,wanau.e wengi tunashindwa kuwaelewa wanawake, ili uishi na mwanamke kwa salama na upendo wa dhati zingatia sana mambo haya mawili

1. usimfanye akakosa amani na wewe(kumuumiza) au kumfanyia kitu cha kuumiza asichotarajia.
wanawake ni viumbe wa ajabu sana but kitu kidogo sana kinaweza kikamtoa upendo wake wote kwako but still asionyeshe tofauti na ukaona yuko vile vile kumbe kuna kitu kizito anasubiria tu muda alipe huenda ukajiona shujaa kwa hicho kiasi kidogo alichozidisha mpka kumfukuza na kutokujua alilala wapi na yeye huwezi jua atafanya lipi endapo na wewe ukienda kushoto au aliamua nini mpka kujifanya mjinga na kujirudi.

2.Kumfanya ajione peke yake
Hili ni kosa kubwa ambalo wanaume wengi huwa tunashindwa sana na ndiyo sababu kubwa sana inayowafanya wanawake wakimbie wanaume zao,unakuta baada ya ndoa mapenzi yote mwanaume unayaondoa bussy na wewe hata mda na mkeo huna akigusa simu yako ndo balaa mostly imifika hatua hiyo huwa anajiona hayuko safe sasa na yeye anaanza kutafuta kwake ili hata siku ukimwaga ugali na yeye aambulie mboga

Hitimisho
ili uishi vizuri na familia zote 2 ya mkeo na yako,endapo kama familia hazitokuwa vizuri na nyie kidogo mmebarikiwa hakikisheni mnawajengea uwezo wa kujitegemea kwa kuwafungulia japo vimiradi vitavyowaingizia chochote kitu kwa siku zaidi kumbuka kuwa nature ya wanawake ni kwamba hawapendani so haijalishi mtata ni mama au mkeo

Refer to my refference ni ndugu yangu ambae anaishi na mama yake mpka now alishaoa wanawake zaidi ya 9 na ote alishaachana nao hpo siwezi kutoa hukumu but nature ya nani mkorofi ushaipata
 
Kama huipendi familia yangu automatically hata mimi hunipendi utakuwa kwangu kimaslahi tu
Ndio imani ambayo unayo.
Mwanamke anatakiwa awaheshimu wazazi/familia yako na kuijali na sio kuipenda.
Upendo ni kitu kingine hauwezi kukurupuka tuu unampenda mtu ili umfurahishe mtu.
.
Kwa mfano nikikuambia "kama hauwezi kuipenda familia yangu usiolewe na mimi" utalichukuliaje hili? Kuwa honest tuu.
Utafurahia kuwekewa condition ya namna hiyo na mwanamke unayetaka kumuoa?
 
ni vigumu mwanaume kutopenda au kutoa madhaifu upande wa kike
 
unaweza kuwa umenipita umri au ukawa mdogo kwangu lakini kwa ulichokifanya kama ni kweli then unakuja kijisifia nbelw ya watu wala hukufanya jambo zuri hata kwani lilikuwa ni jambo la kumwita tu mkeo chumbani na kuyamaliza,wanau.e wengi tunashindwa kuwaelewa wanawake, ili uishi na mwanamke kwa salama na upendo wa dhati zingatia sana mambo haya mawili

1. usimfanye akakosa amani na wewe(kumuumiza) au kumfanyia kitu cha kuumiza asichotarajia.
wanawake ni viumbe wa ajabu sana but kitu kidogo sana kinaweza kikamtoa upendo wake wote kwako but still asionyeshe tofauti na ukaona yuko vile vile kumbe kuna kitu kizito anasubiria tu muda alipe huenda ukajiona shujaa kwa hicho kiasi kidogo alichozidisha mpka kumfukuza na kutokujua alilala wapi na yeye huwezi jua atafanya lipi endapo na wewe ukienda kushoto au aliamua nini mpka kujifanya mjinga na kujirudi.

2.Kumfanya ajione peke yake
Hili ni kosa kubwa ambalo wanaume wengi huwa tunashindwa sana na ndiyo sababu kubwa sana inayowafanya wanawake wakimbie wanaume zao,unakuta baada ya ndoa mapenzi yote mwanaume unayaondoa bussy na wewe hata mda na mkeo huna akigusa simu yako ndo balaa mostly imifika hatua hiyo huwa anajiona hayuko safe sasa na yeye anaanza kutafuta kwake ili hata siku ukimwaga ugali na yeye aambulie mboga

Hitimisho
ili uishi vizuri na familia zote 2 ya mkeo na yako,endapo kama familia hazitokuwa vizuri na nyie kidogo mmebarikiwa hakikisheni mnawajengea uwezo wa kujitegemea kwa kuwafungulia japo vimiradi vitavyowaingizia chochote kitu kwa siku zaidi kumbuka kuwa nature ya wanawake ni kwamba hawapendani so haijalishi mtata ni mama au mkeo

Refer to my refference ni ndugu yangu ambae anaishi na mama yake mpka now alishaoa wanawake zaidi ya 9 na ote alishaachana nao hpo siwezi kutoa hukumu but nature ya nani mkorofi ushaipata
mimi sihitaji ushauri, unaweza kuutumia wewe ukimpata mwenzako wako
 
Similar Discussions

91 Reactions
Reply
Back
Top Bottom