Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
3,303
4,564
Mfumo ni muundo unaotumika kutofautisha, kutekeleza au kuonesha majukumu ya kikazi au majukumu, mfumo ni Mchakato wa Mda mrefu ambao huendesha taasisi fulani ni kwamba bila ya Mfumo hakuna Taasisi.

Mtu hua ni mtumwa/zao/kiungo katika mfumo hivyo mfumo unamuhitaji mtu ili kujiendeleza kuwepo kwa taasisi.

Pia soma: Sio lazima uende CHADEMA ili kuwa mpinzani, jipenyeze kwenye mifumo yao kama Magufuli halafu badili uliyokuwa unaona si sawa

Swali langu, tunaweza kutofautisha kati ya mfumo na mtu/tabia/wadhifa/majukumu?

Nilimnukuu Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa kuna Askari Polisi alisema kuwa wapo miongoni mwao wanasikitishwa na mambo yanayoendelea, je ni kweli mtu mwenye akili anaweza kuishi katika mfumo mbovu?

Pili, political system (mazingira ya kisiasa) ni jumla ya mfumo mzima wa siasa ikiwemo taasisi binafsi, serikali, vyama, shughuli za kiuchumi na watu je, tunaweza kutofautisha hizi taasisi moja moja dhidi ya mfumo wa kisiasa?

Je, tunawezaje kuwa na Mfumo wa kijamaa na kibepari kwa wakati mmoja, vilevile tunawezaje kuwa na mfumo wa kijamaa na asili ya watu wa kibepari?

JE CCM wanaendesha mfumo ni Mabepari ila CHAMA ni cha kijamaa? Tunaweza kukomesha Rushwa, Wizi na Tabia Chafu kwa muundo huu uliyopo?
 
Mfumo ni muundo unaotumika kutofautisha,kutekeleza au kuonesha majukumu ya kikazi au majukumu,Mfumo ni Mchakato wa Mda mrefu ambao huendesha taasisi fulani ni kwamba bila ya Mfumo hakuna Taasisi.

Mtu hua ni mtumwa/zao/kiungo katika mfumo hivyo mfumo unamuhitaji mtu ili kujiendeleza kuwepo kwa taasisi.

Swali langu,tunaweza kutofautisha kati ya mfumo na mtu/tabia/wadhifa/majukumu?

Nilimnukuu Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa kuna Askari Polisi alisema kuwa wapo Miongoni mwao wanasikitishwa na mambo yanayoendelea,je ni kweli mtu mwenye akili anaweza kuishi katika mfumo mbovu?

Pili,Political system(mazingira ya kisiasa) ni jumla ya mfumo mzima wa siasa ikiwemo taasisi binafsi,serikali,vyama,shughuli za kiuchumi na watu je,tunaweza kutofautisha hizi taasisi moja moja dhidi ya mfumo wa kisiasa?

Je,tunawezaje kuwa na Mfumo wa kijamaa na kibepari kwa wakati mmoja,vilevile tunawezaje kuwa na mfumo wa kijamaa na asili ya watu wa kibepari?JE CCM wanaendesha mfumo ni Mabepari ila CHAMA ni cha kijamaa?Tunaweza kukomesha Rushwa.Wizi na Tabia chafu Kwa muundo huu uliyopo?
Nadhani kiingereza hakijakaa sawa kwenye heading! consult your grammar reference book!
 
Back
Top Bottom