Wadau wenye uzoefu naombeni mnipe dondoo ili nipate ujasiri wa kupanda hii kitu, maana nishawahi kuikimbia sehemu.
Huwa unajisikiaje?
Kuna angalizo lolote kuhusiana na ubora wa afya?maana niliwahi kwenda sehemu na shemeji yenu tukapanda bembea moja kama kikombe ambacho kinazunguka halafu kinakwenda juu na chini, Wallah sitarudia kugusa hiyo kitu maana nilidhani wa ubani anakata roho na mimi mwenyewe nilikua hoooi bin taaban.
Tafadhali naombeni mnipe dondoo ya hii "roller coaster" sababu udadisi unanisukuma kutaka kuipanda siku moja.