Unaweza kunisaidia hili?

OGOPASANA

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
262
144
Habari wadau,
Eti biashara gani halali (kwa kuorodhesha zote unazojua) zinaweza kuingiza kipato cha TSH 1,000,000.00 kwa mwezi hapa nchini? na kwa kila biashara inahitaji mtaji wa kiasi gani na mazingira/ vigezo gani kuzingatia?
With thanks in advance.
 
Sitegemei JF Senior Expert Member unaweza kumjibu mwenzio mwenye haja ya kujua kitu muhimu kama ulivyonijibu, nina kila imani tupo hapa kusaidiana.
 
OGOPA SANA acha uoga kwanza maana hata Avatar yako inakueleza ulivyo.Biashara ni nyingi sana rafiki yangu muhimu ni nidhamu ya kutunza hesabu tuu!!
 
ABEDNEGO be spesific najua biashara zipo nyingi, nahitaji kujua na kufahamu kutoka kwa wafanyabiashara na wadau wenye uzoefu na ujuzi wa biashara mbalimbali hapa nchini, specifically zinazoweza kuzalisha income ya milioni moja kwa mwezi.

''usimjudge mtu kwa muonekano wake'' Eg. Avatar
 
Mkuu Profit inategemea na:-
  • Demand
  • Profit Margin
Sasa hata kama unachouza kina faida ndogo sana ; mfano vouchers, mmpesa, soda lakini kama volume ni kubwa basi faida itakuwa kubwa tofauti na kitu labda biashara ya gari au vitu vya bei mbaya unaweza ukauza vitu viwili kwa miezi sita lakini vikakuingizia pesa nyingi

Kwahiyo kuuliza biashara gani inakuwa ngumu sababu inategemea upo wapi mfano biashara ya barafu huenda ikawa nzuri sana Dubai lakini usiweze kuuza kitu North Pole...

Au kiti moto huenda kikawa poa sana Dar lakini usiuze kitu Zanzibar; alafu biashara inategemea na product yako mimi naweza nikawa nauza Chakula naingiza 100,000/= kwa siku sababu ya chakula changu kizuri na wewe jirani yangu usiuze hata sahani moja labda kutokana na uchafu na poor customer care

By the Way SIASA inalipa kama unaweza kuingia mjengoni utakuwa na guarantee ya mshiko hata usipofanya kazi kwa miaka mitano.
 
Habari wadau,
Eti biashara gani halali (kwa kuorodhesha zote unazojua) zinaweza kuingiza kipato cha TSH 1,000,000.00 kwa mwezi hapa nchini? na kwa kila biashara inahitaji mtaji wa kiasi gani na mazingira/ vigezo gani kuzingatia?
With thanks in advance.

Jaribu dala dala, ukiagiza Japan used litakula kama 25m hadi 28m hivi kisha unaingiza 70,000 kwa siku ambayo ni kama milioni 2 kwa mwezi
 
Jaribu dala dala, ukiagiza Japan used litakula kama 25m hadi 28m hivi kisha unaingiza 70,000 kwa siku ambayo ni kama milioni 2 kwa mwezi
Mkuu vipi kuhusu Service ya Gari na kununua spea likiaanza kuharibika.. kwahiyo sio 2m net itabidi utoe na costs nyingine..

Sisemi kwamba ni biashara mbaya lakini inabidi mtu asiingie kichwa kichwa, na wajanja kwenye hii biashara huwa wanahakikisha wanauza gari kabla halijaanza kuharibika kwahiyo pesa yake ikirudi na faida kidogo analiuza gari na analeta jingine jipya kabla halijamzeekea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom