Unaweza kukaa mbali na matumizi ya smartphone kwa sasa?

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,109
2,511
Habari zenu wanajamvi?

Natumai shughuli zenu zinakwenda vizuri huko mlipo.

Leo nakuja na hii mada japo ni la kawaida lakini inaweza kutusaidia kutupa picha ya utofauti kati ya matumizi ndani ya simu za kawaida na hizi za kucharaza vidole simu za smartphone tuite hivyo.

Sasa je, unaweza kukaa mbali na matumizi ya smartphone angalau hata wiki moja au zaidi? Baada ya huo muda nini mabadiliko gani umeyapata kama ulijaribu kufanya hivyo wu kubahatika kufanya hivyo?

Kwangu mimi nilijaribu kukaa bila kutumia smart phone kwa muda wa takribani siku 11 na mabadiliko niliyoyaona ni haya:

1. Kichwa kinapumua au kupumzisha akili (stress)
2. Matumizi yanakuwa yako chini ya muda wa maongezi na vifurushi hasa za internet)
3. Unapata muda wa kuinteract sana na watu hasa mawasiliano ya uso kwa uso
4. Muda wa kucheza na watoto unakuwa mkubwa na wa kutosha

Kikwazo ni hizi kazi zetu za kujitafutia riziki zinatufanya tuwe karibu na hizi simu pamoja na aina ya maisha tunayoishi

Nini kwako umejifunza kukaa mbali na smartphone kama ulibahatika?

Karibu...
 
Mimi huwa napunguza matumizi na muda wa kutumia.

Kwanza nafuta apps zote ambazo naona zitatumia muda wangu mfano (social media apps).

Kitu pekee nabaki natumia ni texting and calling. Hapa nitapata muda wa kufanya mambo yangu mengine vizuri.

Na kupata muda wa kutosha kupumzika.
 
Back
Top Bottom