Unaweza kudhibiti u.t.i mwenyewe..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaweza kudhibiti u.t.i mwenyewe..!

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jan 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I MWENYEWE..! U.T.I ni ugonjwa sugu unaosumbua sana watu wengi hivi sasa, wakubwa kwa wadogo. U.T.I (Urinary tract Infection) ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo na huweza kusababisha maumivu makali na unapojiimarisha mwilini kwa muda mrefu huathiri figo pia. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mtu kusikia haja ya kukojoa kila wakati na kusisimka wakati wa kujisaidia, kusikia maumivu, kutoa mkojo mchafu na hata kutoa haja ndogo iliyochanganyika na damu.

  Wataalamu wetu wa masuala ya tiba wanatueleza kuwa tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo inaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya.
  UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I KWA TIBA MBADALA
  Kwa kawaida kila ungonjwa una tiba mbadala, siyo lazima kwenda hospitali. Unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo utawahi kabla tatizo halijawa sugu.

  Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa. Aidha, njia nyingine ya kuudhibitibi ugonjwa huu ni kunywa maji mengi au kwenda haja ndogo mara baada ya kufanya tendo la ndoa, kitendo hiki husaidia kuwaondoa mapema bakteria wote ulioambukizwa wakati wa kujamiiana na mwenzio.

  Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka ndani ya siku tatu mara baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa maji mengi na juisi ya matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo baada ya siku hizo, hiyo itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na hivyo hauwezi kutibika kwa tiba hii ya nyumbani.

  Katika hali kama hii, utakuwa huna njia nyingine isipokuwa kwenda hospitalini na kuonana na daktari ambaye atakufanyia uchunguzi na kukupatia dozi sahihi ambayo utatakiwa kuizingatia bila kukosa. Uamuzi huu ni muhimu hasa kama unasikia maumivu makali ambayo yanaweza kuwa yanasababishwa na kuathirika kwa figo. Kwa kawaida tiba ya kidaktari kwa ugonjwa huu huhusisha matumizi ya dawa kali za ‘antibiotics’, ambazo watu wengi wanazikimbia kutokana na athari zake za baadae (side effects). Lakini ni muhimu kufuata ushauri wa dokta na kumaliza dozi ili kuepuka uwezekano wa kurejea kwa ugonjwa, tena kwa kasi kubwa.

  KUZUIA
  Ili kujiepusha na ugonjwa huu, suala la usafi na kuwa na tabia ya kunywa maji ya kutosha ni jambo muhimu sana. Hakikisha unajisafisha vizuri mara baada ya kwenda haja na kubadilisha mara kwa mara nguo yako ya ndani, hasa kwa akina mama.

  Vile vile usikae na haja ndogo kwa muda mrefu, nenda kajisaidie mara nyingi kadri unavyosikia kufanya hivyo. Kitu cha mwisho cha kuzingatia kwa mgonjwa wa UTI ni kupunguza unywaji wa pombe na vinywaji vingine vyenye sukari, kwa sababu sukari ni chakula cha bakteria hivyo kwa kuendelea kunywa kinywaji chenye sukari kutaifanya hali kuendelea kuwa mbaya. Ugonjwa huu ni rahisi kuepuka kwa mtu anayependa kunywa maji ya kutosha na kunywa juisi halisi kila siku.

  DAYATI MUHIMU KUDHIBITI UTI
  Katika kuudhibiti ugonjwa huu, pendelea kula vyakula ama vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo utakipata kwenye matunda ya aina mbalimbali yakiwemo machungwa, mboga za majani n.k. Jiepushe na ulaji wa vyakula vya ‘kupaki’ kama vile ‘chizi’, chokoleti na bidhaa nyingine zilizotengenezwa kutokana na maziwa. Pia jiepushe na ulaji wa vyakula vyenye viungo vingi kama pilau, epuka vyinywaji vyenye ‘caffeine’, kilevi na sigara na mwisho achana na vinywaji kama soda na vinavyofanana na soda.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,287
  Likes Received: 22,047
  Trophy Points: 280
  Safi sana, article yako nzuri sana.
  Nimeugua u t i kwa kujidai naujua sana usafi.
  Nilikuwa naosha uke wangu kwa sabuni kumbe naua bakteria wazuri wanaoulinda uke dhidi ya bakteria
   
 3. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Elimu ya bure hii, thanks
   
 4. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Safi sana mzizi mkavu elimu yaukweli mambo yote umeshaelezea vizuri sana kazi kwetu kuchukua hatua
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkuu safi sana maana siku hizi huu ugonjwa umekuwa tishio. ubarikiwe sana
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mzizimkavu asante kwa darsa murua.
   
 7. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Asante sana Dokta Mzizi.
   
 8. C

  Chiriku Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mungu akubariki
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  chocolate? Loh nimeumia.....
   
 10. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bonge ya darasa...ubarikiwe!!
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mtoto wa miaka 9 anatakiwa anywe kiasi gani cha maji kwa siku?
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  @Angel Msoffe inategemea afya yake ilivyo anaweza kunywa lita 2 za maji kwa siku.
   
 13. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  asante sana mkuu
   
 14. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mkuu, naweza kupata wapi Cranberry juice bongo?
   
 15. no9

  no9 Senior Member

  #15
  May 19, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  naona umeamua kutoa tiba asilia hongera
   
 16. n

  negger Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimetumia dozi tatu za u.t.i kila nikipima iko palepale 40/60 nifanyeje hapo maana naona kama hayo masindano hayatibu au ndo dawa feki hizo?
   
Loading...