Unawandaa watoto wako kumiliki au kutumia?

Unawandaa watoto wako kumiliki au kutumia?

Bwege2030

Member
Joined
May 10, 2025
Posts
82
Reaction score
152
Wazazi wazazi siri ya matajiri kama Mohammed Dewji (MO) na baba yake, mzee Gulam Dewji, si kiasi cha fedha walichorithishana, bali ni MIFUMO na ELIMU ya kifedha tangu udogo.

Utajiri haurithishwi, unafundishwa.
Matajiri hawawapi watoto pesa za matumizi; wanawafundisha kuzifanya pesa ziwatumikie.

Pesa ni Mfumo, si Kazi: Matajiri hufundisha watoto kuwa pesa inapaswa kuwatumikia kupitia uwekezaji (kama masoko ya hisa) bila wao kuwepo kila siku.

Nguvu ya "HAPANA": Maskini huogopa kusema hapana, lakini matajiri hutumia neno "Hapana" kulinda utajiri dhidi ya matumizi yasiyo na tija au lazima.

Mkopo ni Silaha: Matajiri hutumia mikopo kuzalisha na kumiliki mali (Hisa, Ardhi, Biashara), siyo kununua anasa.

Uvumilivu & Akiba: Mfundishe mtoto "Delayed Gratification". Akiba na budget si mateso, ni nidhamu ya kuelekea utajiri wa kudumu.

Umiliki vs Ajira: Lengo liwe kumiliki mifumo itakayodumu vizazi na vizazi (Legacy), na si kutafuta ajira ya muda.

Ukimwachia mtoto gari, ataliendesha; ukimwachia nidhamu ya kifedha, atanunua kiwanda cha magari.
Tuwafundishe watoto wetu kuwa Wamiliki ili kurithisha utajiri kwa tija!.

IMG-20260126-WA0000.jpg
1769165288390.jpg

 
Mtoto alelewe, apewe maarifa sahihi, atafute chake. Hi ndio falsafa yangu.

Sio akae akijua atarithi au kupewa, hamna hiyo kwangu. Atawanyike akajenge legacy yake.
Hiyo Ndiyo maana ya nakala hii..mtoto kurithishwa elimu na maarifa ya kufanya pesa imtumikie...
Asante sana
 
Sisi wengine hatuna cha kurithi,ni kujipambania.
Hiyo ni bahati Ndugu yangu! Mtu anayejipambania anakuwa na ujuzi wa kufanikiwa haraka mapema sana,utachelewa kufanikiwa Lakini lazima ufanikiwe... tofauti na mtoto wa tajiri ambaye hajafundishwa,anasubiri kurithishwa
 
Kwahiyo mkuu watanzania milioni 47 wanaoishi kwenye umasikini wote hawana nidhamu ya fedha?
Asilimia 99% hatuna nidhamu ya pesa... Tuko busy na dini,Imani za zamani,Imani potofu pia ya'ani kiufupi unazaliwa unarithi mzazi wako alichokuwanacho ..na wazazi waliowengi wameanza kujua utajiri ,kuwa na hela.. kuanzia mwaka 2000 ...ila hawajui nidhamu ya pesa na Hiyo elimu ni adimu sana kwa bongo
 
Sawa, familia ya Dewji wamewarithisha watoto wao nidhamu ya kutumia pesa walizokuwa nazo tayari.
Vipi kwa sisi ambao hatuna? tutarithishwa nidhamu ya kutumia nini na pesa hatuna?
Hata TSH 10000 unayopata kwa shida, ukiwa na nidhamu ya pesa,na kuelekezwa namna ya kuizalisha inatosha kabisa...mfano
>>>>>>>>>>> >>>>>>>>>>>>>
MWEZI WA 11,mtandao wa vodacom ulikuwa unauza HISA ZA VODACOM (umiliki wa voda) kipande TSh 500 ,aya nambie hiyo 10000 utakuwa na vipande vingapi?
Mpaka sasa HISA ZA VODA zimefika TSH 750 ..je,hapo una sh ngapi?
 
Sawa, familia ya Dewji wamewarithisha watoto wao nidhamu ya kutumia pesa walizokuwa nazo tayari.
Vipi kwa sisi ambao hatuna? tutarithishwa nidhamu ya kutumia nini na pesa hatuna?
Elimu ya fedha ndio msingi mkuu... Nidhamu ni kijisehemu cha elimu ya fedha. There are many parts to explore
 
Nidhamu ipi mwenye nazo anazo , kina Mo wananunua maHonda kila siku new model, kila mtu aishi daraja lake
 
Mtoto alelewe, apewe maarifa sahihi, atafute chake. Hi ndio falsafa yangu.

Sio akae akijua atarithi au kupewa, hamna hiyo kwangu. Atawanyike akajenge legacy yake.
Mchezajshaji makamari Tarimba Abbas wa CCM anasema wototo walazimishwe kuwalea wazazi wao!
 
Matajiri wanarithisha biashara na elimu zote kwa pamoja kwa watoto wao, sisi masikini kwa kuwa hatuna cha kuwarithisha, tunajikita tu kwenye kuwapatia elimu waje wapambane na soko la ajira.
 
Back
Top Bottom