unawakumbuka wacheza disco walisumbua enzi hizo?

Noma mkuu jamaa alikuwa anatisha alichukua ubingwa wa disco wa Africa mashariki kwa macho yangu naona pale silent inn

Na yule kijana alikuwa anacheza ngoma za asili za west africa, anachezea moto na wadada na anamwigiza shaba ranks alipotelea wapi yule?????
 
Home boys wa sinza members banza mchafu,jesca ongala,dogodogo kadoda na dancers wengine wa enzi hizo
Digadiga,dogodogo nyamwela,sammy cool,janet jackson R.I.P,

kiongozi ni ras D (bugaloow)
elvis danger ( michael jackson)
jeska ongala (maddona)
Queen cloud( shala mwana )
banza stone (mubaraka mweshehe)
mandingo
kuna yule dada alikuwa hasikii vzr
kadoda
ukumbi wetu SUNDOWN (sinza makaburini)
DJ steve
n;b sina uhakika kama wote wapo hai wale waliotangulia mbele ya haki R.I.P
 
Yaani nikiwakumbukaga hawa jamaa simini kama dunia Ile ndio hii ya leo....baadhi ya hawa madansa walikuwa malafiki zangu sana...nilishawahi kuandaa show mmoja ambayo sitokuja kusahau katika maisha yangu ilifanyika RUAHA GALAXY KIMARA huyu black Moses alionyesha maajabu makubwa sana sidhani kama kuna kiumbe atakuja kumfikia huyu jamaa.....Dah! Huzuni sana

heshima kwa madansa wote but Black Moses atabakia kwenye vitabu vya kumbukumbu.
 
kuna jamaa alikuwa anaitwa Oswald Kasambala a.k.a Bongoman kule mbeya especially MTC miaka ya tisini mwanzoni
 
Habari za jioni wana jamvi,naami ijumaa ya Leo ipo shwari.Leo nimeona tujikumbushe kidogo wacheza disco waliwahi kutamba sana enzi hizo kabla ya kuja hiki kizazi cha bongofleva na Si vibaya tukiwataja kwa majina ili kuwapa heshima...
1.BLACK MOSESS(RIP)
2.BOB KASSIM
3.BOSCO COOL J
4.KELLY JOHN
5.ALI BAUCHA
6.DIGA DIGA
7.KID FRASH(RIP)
8.MAX
haya mdau na wewe endelea....na Si vibaya ukataja hata ukumbi ulikokuwa unashuhudia baadhi ya mashindano ya hawa jamaa.
nawakilisha.
Salama mkuu.....Kama hautojali pitia bandiko hili hapa chini........

https://www.jamiiforums.com/entertainment/148004-karibuni-mtaa-wa-mangoma-music-boulaverd-d.html
 
Ukizungumzia madansa bongo unamzungumzia Musa Simba aka Black Moses, huyu jamaa alikua hana mpinzani. Kwa wenzangu wazee wa yenu, Super Nyamwela namkubali kwa ubunifu.
 
Back
Top Bottom