Unawajua BeForward Co. LTD Japan

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,563
2,000
Habari za asubuhi wakuu!

Naomba msaada wenu, nataka kununua gari, na nimefanya mawasiliano na Beforward Co. LTD Japan kwa mtandao wao, na asubuhi hii nimekuta Pro forma Invoice kwa E-mail yangu, wakinitaka nikalipie ndani ya 48 hrs. Naomba msaada kujua uhalali na uwepo wa kampuni tajwa, mi huwa naona bango lao pale Jangwani, hivi vijihela nimevunja kibubu jana, na wabongo wamekuwa watu hatari sana, wasije niingiza mjini!

Natanguliza shukrani, ruksa kupita kimya kimya!
 
Borro

Member
Nov 29, 2011
97
125
Mkubwa wala usiwe na shaka kuhusu beforward we nenda kalipie. Angalizo kama vip ingia kwenye web yao kwanza check zile hatua jins ya kuagiza gari hadi kufanya malipo.

Wana namba nyingi za account ambazo pia kuna kuwa sales manager responsible kwa kila namba. So kama namba ya account kwenye proforma ipo ndani ya zile kwenye web yao basi hapo hakuna shida.

Lakin kwanza ingia kwenye hiyo web utapata details kibao kuhusu kulipia na vitu vingine kabla hujaamua kwenda benk.
 
QuadKabaku

Member
Sep 7, 2013
35
125
Kwa ushauri nenda tu kwa branch yao hapo Dar, ufanye malipo hapo then wao wataleta hiyo gari.

Mimi nimeshafanya order online kuagiza magari mara nne tofauti na yalifika salama tu. Hivyo ili uwe na amani tumia branch yao hapo Dar.Maana wao wanafanya delivery hata mpaka nchi za jirani
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,563
2,000
Kwa ushauri nenda tu kwa branch yao hapo Dar, ufanye malipo hapo then wao wataleta hiyo gari.

Mimi nimeshafanya order online kuagiza magari mara nne tofauti na yalifika salama tu.Hivyo ili uwe na amani tumia branch yao hapo Dar.Maana wao wanafanya delivery hata mpaka nchi za jirani

Nashukuru sana! Ipo wapi ofisi yao kwa hapa dsm?
 
mlimbwende

Member
Jul 15, 2011
72
95
Befoward Japan ni Kampuni nzuri ila nakupa tahadhari usije ukatumia agents wa BEFOWARD Tanzania ni wasumbufu na awajui kazi sisi hapa tumeagiza magari yameingia bandari Dar es salaam sasa ni mwezi wa pili lakini wameshindwa kuyatoa bandarini kila siku tunaacha kazi tunashinda ofisini kufuatilia bila mafanikio,

ila kuna tetesi ni kwamba agents wa BEFOWARD Tanzania wanawapa kipaumbele wafanya biashara wakubwa wenye magari mengi, wewe kama una magari mawili au matatu jiandae kusubiri miezi mitatu utazungushwa na hadithi za uongo uongo na file awataki kuachilia, kwakweli hawa agents wao Tanzania ni wababaishaji kweli na wanaharibu sifa ya BEFOWARD JAPAN
 
RR

JF-Expert Member
Mar 17, 2007
6,885
2,000
Habari za asubuhi wakuu!

Naomba msaada wenu, nataka kununua gari, na nimefanya mawasiliano na Beforward Co. LTD Japan kwa mtandao wao, na asubuhi hii nimekuta Pro forma Invoice kwa E-mail yangu, wakinitaka nikalipie ndani ya 48 hrs. Naomba msaada kujua uhalali na uwepo wa kampuni tajwa, mi huwa naona bango lao pale Jangwani, hivi vijihela nimevunja kibubu jana, na wabongo wamekuwa watu hatari sana, wasije niingiza mjini!

Natanguliza shukrani, ruksa kupita kimya kimya!

Ingia hapa ....then uwe na amani!
Ni waaminifu sana!
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,563
2,000
[Befoward Japan ni Kampuni nzuri ila nakupa tahadhari usije ukatumia agents wa BEFOWARD Tanzania ni wasumbufu na awajui kazi sisi hapa tumeagiza magari yameingia bandari Dar es salaam sasa ni mwezi wa pili lakini wameshindwa kuyatoa bandarini kila siku tunaacha kazi tunashinda ofisini kufuatilia bila mafanikio,

ila kuna tetesi ni kwamba agents wa BEFOWARD Tanzania wanawapa kipaumbele wafanya biashara wakubwa wenye magari mengi, wewe kama una magari mawili au matatu jiandae kusubiri miezi mitatu utazungushwa na hadithi za uongo uongo na file awataki kuachilia, kwakweli hawa agents wao Tanzania ni wababaishaji kweli na wanaharibu sifa ya BEFOWARD JAPAN

Nashukuru kwa kunishtua, nilitaka kuwatumia km agents! Nitatafuta agent tofauti
 
Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
2,378
2,000
Befoward Japan ni Kampuni nzuri ila nakupa tahadhari usije ukatumia agents wa BEFOWARD Tanzania ni wasumbufu na awajui kazi sisi hapa tumeagiza magari yameingia bandari Dar es salaam sasa ni mwezi wa pili lakini wameshindwa kuyatoa bandarini kila siku tunaacha kazi tunashinda ofisini kufuatilia bila mafanikio,

ila kuna tetesi ni kwamba agents wa BEFOWARD Tanzania wanawapa kipaumbele wafanya biashara wakubwa wenye magari mengi, wewe kama una magari mawili au matatu jiandae kusubiri miezi mitatu utazungushwa na hadithi za uongo uongo na file awataki kuachilia, kwakweli hawa agents wao Tanzania ni wababaishaji kweli na wanaharibu sifa ya BEFOWARD JAPAN

Naunga mkono hoja. Ukitaka kujuta tumia Be forward Tanzania kama agents. Pengine wana hisa kwenye yard zinazohifadhi magari manake lazima ukutane na storage charge kubwa unaweza ukazimia kama wewe sio ngangari. Kifupi agiza gari Be forward Japan document zikifika waambie wakupatie then tafuta agent mwaminifu utapata gari lako kwa wakati bila gharama za ziada. Achana kabisa na Be forward Tanzania.
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,534
2,000
acha woga minimetoka kutuma hela asubui namnunulia wifi yako ndinga maana ananikosha sana kipindi hiki cha baridi amejituma sana ...ngoja nimtunuku Noah
 
Dec 22, 2013
6
0
Samahani nilikua nauliza vp kuhu ushuru wake mpaka kuitoa gari maanake nimeona magari rahisi kwenye ushuru inakuaje asanteni

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
mwantui

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
1,624
2,000
acha woga minimetoka kutuma hela asubui namnunulia wifi yako ndinga maana ananikosha sana kipindi hiki cha baridi amejituma sana ...ngoja nimtunuku Noah

hapo lazima aongezee bidii akiamini utamnunulia helicopter kabisa..
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,563
2,000
Naunga mkono hoja. Ukitaka kujuta tumia Be forward Tanzania kama agents. Pengine wana hisa kwenye yard zinazohifadhi magari manake lazima ukutane na storage charge kubwa unaweza ukazimia kama wewe sio ngangari. Kifupi agiza gari Be forward Japan document zikifika waambie wakupatie then tafuta agent mwaminifu utapata gari lako kwa wakati bila gharama za ziada. Achana kabisa na Be forward Tanzania.

Nashukuru sana mkuu! Naomba msaada wako kama unaijua kampuni nzuri ya clearing agent!
 
Juma salehe

Member
Jan 13, 2014
40
0
Mcheki huyu jamaa anaitwa JACOB 0754_267097 , AVALON BLD , NEAR AZAM MARINE POSTA, mwambie umepewa namba na DR JUMA, meli ukifika cku ya tatu au nne anatoa gar, keshanitolea c chini ya gar 50 within 4 yrs of my business
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom