UNAVYO JIHISI KIFO

UNAVYO JIHISI KIFO

lingindingi

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2016
Posts
218
Reaction score
123
Mtu huwa hatambui kuwa amekufa pale anapokufa. Yeye hujihisi anaota anakufa, anajihisi analia, anaoshwa, anafungwa na anateremshwa kaburini.
Bado anajihisi kuwa anaota anapofunikwa na mchanga. Kisha hulia kwa makelele na hakuna anae msikia.
Baadae kila mtu anapotawanyika na ameachwa pekee chini ya ardhi, Mungu huirudisha roho yake. Anafungua macho na kuamka kutoka "ndoto yake mbaya". Mwanzoni, hufurahi na kushukuru kuwa alikuwa anaota tu, na sasa ameamka kutoka usingizini. Kisha hujigusa mwili wake ambao utakuwa umefunikwa na kitambaa cheupe,na kwa mshangao hujiuliza "shati/gauni langu liko wapi?"
Kisha ana anza kujihisi "niko wapi?" "hii ni sehemu gani?" Mbona kuna harufu ya udongo kila mahali? Ni nini haswa ninacho kifanya hapa?
Hapo ndipo atakapo anza kugundua kuwa yuko chini ya ardhi na alicho kihisi haki kuwa ndoto!
Ndiyo, anagundua kuwa ni kweli yeye amekufa, na amezikwa.
Anapiga kelele kadri anavyoweza kuwaita watu waliokuwa karibu nae ambao wangeweza kumuokoa:
"baba"
"mama"
"kaka"
"dada"
"rafiki"

Hakuna anaemjibu. Kisha anagundua kuwa Allah ndio tegemeo lake pekee. Akilia na kumuita huku akimuomba msamaha :
"Yaa Allaaaaah...
Yaa Allaaaaaah...
Nisamehe mimi
Yaa Allaaaaaah!!!

Anaita akiwa na hofu kubwa,ambayo hakupata kuwa nayo alipokuwa hai .

Kama alikuwa mtu mwema na mcha Mungu, malaika wawili wakiwa na uso ulio na furaha watamkalisha na kumliwazana kumhudumia vizuri.

Kama alikuwa mtu mbaya na hakuwa mcha Mungu, malaika wawili watamwongozea hofu yake na kumpa mateso kufuatana na amali zake mbaya.

Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu, dhambi za baba yangu, mama yangu, mke/mume wangu na wanangu na jamaa zangu na marafiki.

C&p
 
Mtoa Mada ...Unalengo ...lakuwatisha watu...lakin kwa hii Generation ya sasa hiv ...utakuwa unatwanga maji kwenye kinu maana wengi wao hakuna anayeamin kama kuna ...Kifo ..na awaamini uwepo wa Mungu.
 
So..... wale wanaozikwa kwa kuchomwa moto (cremation) roho hua zinarudi wapi? Vipi wale wanaokufa kwa kuliwa na wanyama?
Dini zimefunga vichwa vya watu na minyororo ya ujinga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom