JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 9,058
- 9,660
natumaini wadau mmeshasikia au kuathirika na vikundi hivi vya vijana waliokuwa wanafanya uhalifu kwa pamoja. kuna kiboko msheli, komandoo yosso, begi bovu, mbwa mwitu. wakati nakaa maeneo ya mwananyamala dsm hao jamaa wa begi bovu walikuwa wananilazimisha mpaka saa nne usiku niwe nimesharudi nyumbani maana wakikutana nawe inabidi uwakabidhi ulichonacho kisha wanaweka kwenye hilo limfuko au libegi lao. hao mbwa mwitu nimesikia uhalifu wao wanautekeleza hasa maeneo ya beach hususan kule coco. wadau, vipi kuhusu kumbukumbu zenu kuhusiana na hawa jamaaa?