Unatumia Infinix? Kuna maujanja yako hapa

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Kwenye simu nyingi za Infinix Kuna feature inaitwa ๐— ๐—ฒ๐—บ๐—ณ๐˜‚๐˜€๐—ถ๐—ผ๐—ป umeshawahi kutumia? Je unaijua inafanya Kazi gani ? Leo nitakujuza

Kama ๐—จ๐—ป๐—ฎ๐˜๐˜‚๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—œ๐—ป๐—ณ๐—ถ๐—ป๐—ถ๐˜… Kuna feature inaitwa Memfusion kazi yake ni kukusaidia kuongeza ufanisi kwenye simu yako.

Inaitwa Memfusion ni feature ambayo inafanya Kazi ya kuongeza nafasi kwenye kifaa chako na kuifanya simu yako iweze kufanya kazi kwa ufanisi Zaidi kwa kuongeza ram.

Tuchukulie simu yako imekuja na Ram 8Gb alafu ukaongezewa 8Gb inakua jumla 16Gb kwaiyo wakati unatumia simu kwenye kazi Zako ufanisi wake unaongeza na kuwa imara Zaidi ivyo kuifanya simu yako kutumia bila kuganda Ganda.

Kwaiyo unajikuta unafungua program nyingi kwa wakati mmoja, pia unaweza kucheza Game bila simu kuwa nzito na kufurahia mchezo mzima.

Je Memfusion unawezaje kuipata kwenye simu yako ? Fanya hivi chukua simu yako
โ€ข ingia setting
โ€ข chagua storage
โ€ข ingia kwenye Memfusion Kisha Enable

Utaweza kuongeza ufanisi kwenye simu yako ya Infinix na kufurahia performance wakati unatumia.

Umeshawahi kutumia hii feature au ndo unasikia Leo tuachie maoni yako?

#bongotech255
 
Nisaidie upande wa message, SMS nyingine hazionekani hasa za DAWASA, zinajificha wapi? Archive hazionekani! Nifanyeje?
Mwanzoni zilikua fresh tu zinatokea sio ?

Kama Yes basi fanya kwanza update ya app yako ya Message

Pili kama Bado inazingua insbidi uingie setting Kisha app alafu tafuta app ya message Kisha clear cache na force stopped ukimaliza itakua poa
 
Baada ya hapo simu inapandisha joto kama vile inaendeshwa na makaa ya mawe
Hayo ndo mambo ya infinix
Mimi huwa nawaambia watu ukiona mtu amenunua Tecno & Infixnix ya zaidi ya 120K huyu siyo hana hela ya kununua simu nzuri ila hajakutana na mtu wa kumshauri.

Namfahamu jamaa alinunua Tecno Tsh 635,000/= but kwa hela hiyo angepata simu bomba kama Oppo,Redmi&Vivo ila ndiyo hivyo akawa analalamika kwamba changamoto alizokutana nazo kwenye Tecno za 200K bado akawa ameanza kuziona baada ya muda mfupi kwenye hii simu aliyoamini ni nzuri na ya gharama.
 
Nice
But Virtual RAM ambazo zinakuja kwenye Chinese phones mara nyingi ni useless na hazina mchango mkubwa kwenye performance, maybe itasaidia kwenye multitasking kidogo tu lakini usitegemee improvement kwenye performance.
Virtual RAM sio sawa na built in RAM. Mara nyingi hutumika kama marketing strategy tu
 
Hii kitu hata Samsung wanayo inaitwa Ram Plus , naona naweza nikaongeza Gb nane so total ikawa 16 GB

Screenshot_20230605-231329_Device care.jpg


Screenshot_20230605-231249_Device care.jpg
 
Back
Top Bottom