Unataka kuwa tajiri?(Desa hili hapa)

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,538
2,000
Kutoka Mtandaoni: MAMBO TISA IKIWA UNATAKA KUUKWAA UTAJIRI...KINYUME CHAKE NI MAMBO SABA IKIWA UNATAKA KUWA MASKINI/FUKARA:

1. Acha kuahirisha mambo

Ujinga wa vijana wengi ni kuamini kwamba wakati wote, kuna wakati mwingi/wa kutosha siku za hapo mbeleni kufanya jambo lolote watakalo...hivyo kila mara huahirisha mikakati ya kuchukua hatua wakijimabia "aah nitafanya kesho au mwezi ujao au mwakani"... Vijana wengi huamini kwamba wakati wa uzeeni au umri uliosonga sana ndipo mambo ya fedha yatatiki hivyo hawana mpango wa kujishughulisha saana na baadae,kwao LEO ndio inayomata. KOSA KUBWA. Mwandishi anasema kama unataka kuwa tajiri kupata mali/ukwasi nk anza sasa kwa hicho ulichonacho, iwe kwa kuwekeza akiba,kukuza mtaji,au kukuza matumizi sahihi ya vipawa vyako ambavyo ni mtaji tosha.

Kuahirisha mikakati kutakupelekea kupoteza au kuporomosha kiwango cha matarajio yako...kwa kadiri unavyoahirisha ndivyo ndoto hiyo ya KUWA TAJIRI inavyozidi kuyoyoma...Fikiria miaka Kumi iliyopita ulipanga kufanya nini ili kujiendeleza na je ulifaanya?...hebu fikiria sasa kama ungefanya ungekuwa wapi leo (Kwa mfano kama ulikuwa na fursa ya kununua shamba upande miti ya mbao inayokomaa kwa miaka kumi leo si ungekuwa tayari unazungumza hadithi nyingine?)

Japo kuweka akiba KUNATISHA lakini usiogope chukua hatua hiyo ngumu kabisa...hii ni njia ngumu kuianza lakini baadae huwa rahisi kama unapata 100 basi weka akiba ya shilingi 20 ili kufikia lengo.ANZA SASA.USIAHIRISHE!.


2. Tambua kwamba hakuna Uchawi kufikia hatima yako.
Hakuna muujiza utakaokufikisha kwenye hatima yako ya kuwa tajiri...iwe unaamini katika nguvu za asili(ushirikina/uganga/ulozi) au unaamini katika Mungu au miungu...hakuna njia ya kichawi kufikia hatima yako...kama ipo hiyo huwa ni nyongeza tu...yaani INGREDIENT(kikolezo) kwa zile juhudi ambazo tayari zimeshafanyika.

Mkakati ni rahisi tu kufikia hatima yako ya utajiri: Tengeneza/ingiza/weka akiba/tumia katika mradi wako kiasi kikubwa zaidi ya kile unachotumia kisha wekeza tena na tena uwiano wa matumizi na mapato uwe 80:20. Ni jinsi gani unawekeza kiasi hicho hiyo unaweza kuamua wewe lakini muhimu HAKIKISHA unachotumia ni kidogo kwa uwiano wa mbali na kile unachoingiza( TATIZO: Ni kwamba vijana wengi wanatumia zaidi ya mapato yao yaani kijana anapata mshahara wa shilingi 500,000 kwa mwezi matumizi yake kwa mwezi ni Tzs 800,000 au ana mtaji wa TZS 4,000,000 anatengeneza faida ya shilingi Laki Moja kwa siku matumizi yake kwa siku ni TZS 80,000 my friend kama ndio hivi sahau kuwa Bourgeoisie. INGIZA SANA;TOA KIDOGO). Kanuni hii inamvusha mtu anaefanya biashara au kazi yoyote yenye kipato.
DISADVANTAGE: Hapa Bongo utaitwa bahiri. Na jiandae kuishi maisha ya kawaida(low profile life) bata zipo sana kuanzia bata maji hadi bata mzinga huko mbele ukishakuwa ume make.3. Wekeza kwako mwenyewe.
Lengo lako jingine muhimu liwe kuwekeza kwako mwenyewe; WEWE ni rasilimali muhimu sana kupata ukwasi na utajiri(Hapa Tanzania tunao msemo usemao AFYA NI MTAJI-maana yake hasa ndio hii kwamba wewe ndio mtaji). Kuwekeza kwako mwenyewe ina maanisha kwamba uwekeze kiasi cha muda wa kutosha kujiongezea maarifa,kutafuta taarifa ya kile unafanya,kufanya utafiti wa masoko na fursa za kuongeza kipato zaidi,kutengeneza mtandao kwa kukutana na watu pamoja na fursa mpya kila uchao ili uweze kutanua mbawa zako za kuingiza mapato zaidi. Ubunifu si katika kutengeneza viwalo na masuala ya fasheni pekee...ubunifu unamata sana katika kujiongezea uwezo wewe mwenyewe kama tajiri wa kesho.


4. Tengeneza Bajeti.

Kumbuka Pointi ya hapo juu kwamba Ingiza fedha nyingi zaidi toa kidogo na wekeza kwa busara:

Kanuni hii ya Ingiza zaidi toa kidogo na wekeza kwa busara inakwenda sanjari/sambamba na upangaji mzuri wa bajeti...hakika!! hutaweza kuitekeleza kanuni hiyo hapo juu kama sio mtu wa kupanga bajeti....ni bahati mbaya kwamba hatupendi kabisa kutumia kalamu na daftari kuweka mipango yetu ya fedha...kutofanya hivyo kunatufelisha sana...fedha ni kanuni na kanuni ni fedha...Kanuni moja wapo ya fedha ambayo ni muhimu sana ni pamoja na hii ya kuweka bajeti.(Ule usemi wa mipango sio matumizi ni usemi ambao binafsi sikubaliani nao kwa sababu unachora picha ya mtu ambae huwa anaweka mipango lakini wakati wa kutumia hazingatii kile alichokipanga-kufanya hivi ni kukosa nidhamu ambako hakutakuwezesha kufikia lengo.)

Weka Bajeti kwa ajili ya shughuli zako na maisha yako kwa kuzingatia kiasi cha mapato unayoingiza na matumizi yako ya kawaida.

Ni lazima uweke kiwango ukomo cha matumizi...na pia uweke jicho lako ni eneo lipi linatumia fedha nyingi zaidi kwenye oroddha ya jumla ya matumizi yako yote (je ni michepuko? a bit of joke!) hapa usiruhusu nafsi na roho yako viendeshe tamaa zako za mahitaji ya mwili laah! hutafanikiwa.

Ili kutambua kwamba unatumia fedha nyingi katika matumizi ya kawaida ni lazima uwe na utaratibu wa kuandika mapato na matumizi vinginevyo hutaona wala kuhisi kama umekuwa unatumia fedha nyingi kwa matumizi yako ya kawaida kuliko kile unachoingiza.


5. Lipa Madeni.
Kabla hujaanza kufikiria kuweka akiba na kuwekeza fedha ili ulifikie lengo lako...ni muhimu sana kulipa madeni yoyote unayodaiwa. Madeni ya gari,kodi na bili mbalimbali nk hivi huwa vinyonya nguvu vikubwa katika kufikia azma yako ya kuwa tajiri...Epukana na madeni kwa kadri uwezavyo ili ulifikie lengo lako haraka...inapolazimu kukopa tumia hekima na busara kama utaweza kurejesha deni bila kupata hsara kwenye uwekezaji wako. KOPA KWA AKILI...Mkopo uhusike tu kuchagiza ukuaji wa biashara na si vinginevyo na ufanye hivyo inapobidi.


6. Usiogope kuchukua mzigo wa misumari(Take risks)
Wewe bado ni kijana. Unayo miaka mingi mbele. Huu ndio wakati wa kubeba mzigo wa misumari (take risks). Wekeza kwenye maeneo ambayo watu wanayaogopa ikiwa tu una uhakika ukokotozi wako wa marejesho ya faida utakuwa mkubwa ikiwa utafanikiwa,je waweza kununua hisa kwenye kampuni ambayo watu wengi wanadhani haifanyi vizuri kwa sasa? Je unaweza kufanya biashara ya daladala kwenye barabara mbovu ingawa kuna wateja wengi? je unaweza kununua nyanya za Ilula ukapeleka Mombasa ingawa uhakika wa kufika salama ni mdogo ingali huko Mombasa soko la nyanya liko juu?, je unaweza kununua na kusafirisha maua kupeleka London ingali wanasema biashara hiyo inalipa ila ikikukata inakukata kweli?....Je unaweza kuacha kazi baada ya kukusanya fedha za kutosha kukupatia mtaji au baada ya kuwekeza kiasi cha biashara kujisimamia yenyewe ili ukaisimamie kwa umakini zaidi?.CHUKUA MZIGO WA MISUMARI na tembea kwa stepu.


7. Fanya jitihada zako katika mtazamo mtambuka (Diversify)

Ingawa kuchukua hatari/risks ni mkakati unaoweza kukulipa hapo baadae ikiwa utafanikiwa ni muhimu ukahakikisha hauweki mayai yako yote kwenye kapu moja...zitawanye jitihada zako huku na kule ili ikishindikana hapa iwezekane pale,na ikiwa wastani pale ikawe vizuri sana hukoo!!...


Usijenge uzio kwenye maarifa uliyonayo sasa...ongeza maarifa zaidi...je unamiliki gereji na je unaweza kufungua video production company? je unauza chakula? unaweza kujaribu kuuza spea za pikipiki za miguu mitatu?....nk nk.....

Kamwe! usijiegemeze kwenye uwekezaji wa aina moja na wala usijaribu kamwe kuweka beti mtaji wako wote kwenye biashara moja...badala yake, jitahidi kutanua wigo wa uwekezaji wako katika maeneo tofauti tofauti....mfano Bakhresa Food,Bakhresa Marine,Bakhresa digital nk nk.

Aidha, kumbuka mara zote unapotaka kuongeza wigo wako wa uwekezaji usiwasikilize watu wasio sahihi jitahidi kwa uri na thim upate taarifa sahihi za biashara au shughuli mpya unayotaka kuwekeza ili kutanua mbawa zako za kipato...kama unaweza kufungua tuition center, ukawa na duka la nguo za ndani za kike,,,ukawa na duka la spea za magari unaweza pia ukalima matikiti kama umejiridhisha kila upande unaweza kuongeza tija kwenye mapato yako katika kuifikia azma yako ya kuwa Tajiri.8. Matumizi sahihi ya muda
Ikiwa utafeli kutumia muda wako vizuri ni vigumu sana kuifikia ndoto hiyo; muda ni fedha na fedha ni muda. Fursa yoyote iliyopo mbele yako inapoachwa kwa sekunde moja kuna mtu anaifikiria na kuitekeleza na inamtoa na kumbuka akiingia yeye kwenye fursa yako tayari wewe umepoteza pointi. Kwa hiyo amua fanya sasa na huo ndio utumizi sahihi wa muda.

9. Ishi Kibepari
Tumekuzwa na mfumo wa kijamaa familia mtambuka zile za ndugu na jamaa yaani extended family na tumeishi kwa kubebana sana unaweza kuwa na kipato kikubwa na wajibu wako ukawa ni kutunza almost ukoo mzima...my friend if that is the style zile kanuni za kule mwanzo hazitaweza kufanya kazi hapa...kwa hiyo ishi kibepari haswaa wakati ukitafuta kufikia lengo huu ujamaa ulete huko baadae sana wakati umesha kuwa stable.
Hebu tujikumbushe zile sifa za kibepari nakumbuka shule zilikuwa zinaitwa Features of Capitalism/Capitalist economy.
i) Mali Binafsi(Private property)- Hapa changu ni changu-haihitaji ufafanuzi sana.

ii) Mipango ya Bei (Price Mechanism) - Ubepari ambao ndio utajiri haswaa huchagizwa na mipango ya bei yaani thamani na mtoe na muingize ambavyo haswa vinaangalia mahitaji ya soko; kwa hiyo ili ukuze himaya yako ya mapesa angalia soko na bei vinasemaje na wewe cheza na upepo huo...na upepo huu anaeuvumisha mara zote ni Bepari hasa kwenye uchumi huria kama wetu.

iii) Uhuru wa biashara- tafuta mazingira hayo ya uhuru wa kufanya biashara yako na uhakikishe hakuna kikwazo chochote kutoka ndani yako mwenyewe na familia yako au nje...hakikisha biashara yako inakuwa huru kweli kweli...na uhuru hapa unaweza hata kumaanisha kuwa muwazi kwa mamlaka za serikali ili usibanwe banwe na hatimae kutofurahia unachokifanya...altenatively utatumia njia haramu ambayo haitakupa uhuru wa kutanuka kwa sababu mara zote utakuwa mtu wa kujificha.

iv) Uhuru wa wateja wako (Sovereignty of that consumer)- kanuni hii mabepari wanaitumia kuwin soko 'kushindwa kutekeleza matakwa ya mteja wako ni kushindwa kufanikiwa'

v) Msukumo wa faida- biashara au shughuli yoyote ya capitalist lazima izae 'faida' kila unalofanya ufanye kwa lengo la kupata faida hata kama mchakato wake watu wanaweza wasiuelewe...usishangae hata matajiri wakubwa wanajipambanua kama philanthropists(watu wanaojitolea kwa makundi ya wasiojiweza) lengo lao huwa ni kutengeneza faida kwa namna ambayo mtu wa kawaida hataielewa vizuri...mkakati mmoja wapo huwa ni 'be a philanthropist to win consumer's sympathy in business'

v) Kusiwe na uingiliwaji wa serikali kwenye biashara

Kanuni hizi nimezinyaka mtandaoni nikazifasili...ili tushee pamoja nanyi wanabodi...tulenge kutoboa jamani haya maisha mbona yanawezekana na kwa tunaoamini Mungu, ameweka ardhi kama mtaji na sisi wenyewe kama mtaji...twendeni guys tubadilishe kizazi na historia ya taifa.
WE ARE/I AM RICH.
 

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,311
2,000
Ukiweza kuzika fahari ya Leo kwa faida ya kesho na Mungu akakusaidia ukaiona kesho yako , hakika unafaa kuitwa shujaa
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,538
2,000
Ukiweza kuzika fahari ya Leo kwa faida ya kesho na Mungu akakusaidia ukaiona kesho yako , hakika unafaa kuitwa shujaa
Kabisa.Tatizo huo udiriki ndio hatuna wengi tunaishi kwa ajili ya leo. Utasikia 'kesho unaijua?'
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,538
2,000
Safi sana mkuu kutuletea hizi mbinu tushindwe wenyewe.
Kabisa.Kuwa na utajiri wa mali inawezekana sana hapahapa Tanzania. Kwenda kutafuta mali nje ya mipaka kwa kisingizio cha hapa kwetu hakuna kitu binafsi sikubaliani. Tukiacha uvivu wa akili,nafsi,na mwili tutavuka kuwa angalau kama Singapore ambao sio muda sana tulikuwa na uchumi sawa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom