Unataka kufanya uwekezaji basi wekeza huku

Unataka kufanya uwekezaji basi wekeza huku

Kuna baadhi ya sehemu ukiwekeza ni uhakika ila tulio wengi hatujui na hatufahamu kuhusu hili.mfano kuna kitu kinaitwa Samia Infrastructure Bonds ni hati fungani mahsusi inayotolewa na benki ya CRDB kwaajili ya kufadhili miradi muhimu ya miundombinu nchini Tanzania, hasa ujenzi wa barabara chini ya wakala wa barabara Vijijini na mjini (TARURA).

Miradi hii inaongeza mtandao usafiri nchini,ikiboresha Kwa kiasi kikubwa usafiri wa mjini na Vijijini. Bondi hii inalenga kukusanya Tzs bilioni mia hamsini. Tzs(150,000,000,000/=) na imepitiwa na kuidhinishwa na mamlaka ya masoko ya mtaji na dhamana CMSA. Hii inahusisha Kwa watu binafsi na makampuni.

Kwa watu binafsi,wanaotafuta UWEKEZAJI salama na wenye faida Kwa muda wa kati ya (miaka 5)huku pia wakichangia katika maendeleo ya taifa.

Kwa makampuni,biashra na taasisi zinazopendelea UWEKEZAJI salama unaougwa mkono na serikali unaendana na malengo ya uwajibikaji wa kijamii wa kampuni na ukuaji wa kifedha basi hii ni sehemu salama ya kuwekeza.

FAIDA NA GAWIO
Bondi hii inatoa riba ya asilimia 12 kwa mwaka,inayolipwa Kila robo ya mwaka ndani ya kipindi Cha miaka mitano.

Kwa mfano,
Ikiwa utawekeza TZS 1,000,000/= kwenye bondii ya miundombinu ya Samia yenye riba ya 12% Kwa mwaka utapata riba ya TZS 120,000 Kwa mwaka. Riba hii inalipwa Kila robo mwaka,kwa hivyo Kila miezi mitatu utapokea TZS 30,000/=

(NB) Faida inaongezeka kutoka na kiasi ulichowekeza

Jinsi ya kuwekeza Bondi
(1) Kwa wateja wa CRDB Bank
Pakua au fungua app ya simbanking chagua huduma>Samia bond >wekeza sasa > kisha endelea kufuata maelekezo .

(2) Kwa wateja wa banki zingine
Tembelea tawi lolote la banki ya CRDB kujaza fomu au pakua kutoka kwenye tovuti yetu ujaze kwa umakini,kisha peleka tawini watazipokea.

(NB) Kwa maelekezo zaidi ingia google andika (Samia Infrastructure Bonds)
(See You At the Top)
Kwamba mabulungutu ya wajomba yanakaribia kuisha?
 
Bado ni pesa ndogo,, kwa uwekezaji wa 5M either katika biashara faida utakayo kuwa unaipata haiwezi kabisa kulingana na hiyo yenu.
Alfu kumbuka biashara ni upate au ukose,sasa hapo ni kupata hakuna kupoteza
 
Alfu kumbuka biashara ni upate au ukose,sasa hapo ni kupata hakuna kupoteza
Pitia comments,, mmoja huko juu kasema what if Samia au ccm usirudi madarakani, na vipi kama kiongozi mpya atakaye ingia akabadili mfumo mzima??


Haujapoteza pesa zako kijinga hapo?
 
Hakuna investor makini atathubutu kuwekeza kwenye hati fungani kama hiyo. Imekaa kichawa chawa sana. What if umewekeza na Samia au CCM isirudi madarakani? Kwa ujumla hizo bond za serikakali kama serikali ikianguka au mapinduzi kutokea au akija mtawala mwingine anaweza akabadili mifumo na kuwachinjia baharini.

Pia hizo bond ni hasara sababu kunakuwa na inflation na thamani ya pesa inabadilika kwa kushuka.

Ukiona unaitwa kwenye fursa ujue wewe ndio fursa na ukipewa bidhaa ya bure utambue kuwa wewe ndio bidhaa.
Naomba unielimishe, mimi ngumbaru kwenye Uchumi
Kwa hiyo serikali iliyopo madarakani ikiondoka, waliowekeza kwenye hati fungani wanapoteza?
Je, thamani ya fedha inapungua kiasi cha 12% kwa mwaka mpaka uwekezaji usiwe na faida?
 
Kuna vitu Huwa vinabakia hata iweje mfano masuala ya treasure bond Huwa hayabadiliki na watu watalipwa stahiki zao Kama makubaliano yanavyosema
Mkuu ukweli unafichwa ila upo wazi kwa wanaochimba kwa kina na kuutafuta. Sio guarantee asilimia mia kuwa watalipwa stahiki zao.

Government bonds na treasury bills zilikuwa na uhakika na salama miaka kumi iliyopita. Sasa hivi hadi unaona zinatangazwa na kuhamasisha wastaafu wanunue bond maana yake Kuna kitu hakipo sawa.
 
Kwa watu binafsi,wanaotafuta UWEKEZAJI salama na wenye faida Kwa muda wa kati ya (miaka 5)huku pia wakichangia katika maendeleo ya taifa.

Hii scheme bado inaendelea kuruhusu watu kuwekeza?

Sio kwamba walisitisha watu kuongeza au kuanza kuwekeza?
 
Naomba unielimishe, mimi ngumbaru kwenye Uchumi
Kwa hiyo serikali iliyopo madarakani ikiondoka, waliowekeza kwenye hati fungani wanapoteza?
Je, thamani ya fedha inapungua kiasi cha 12% kwa mwaka mpaka uwekezaji usiwe na faida?
Mkuu mimi si mtaalamu wa uchumi. Pia sijasema kama waliowekeza watapoteza kama serikali ikiondoka.

Lengo la bond ni kuwekeza kwenye uchumi. Yaani unaikopesha fedha serikali halafu serikali inatumia fedha zilizowekezwa kwa maendeleo kama barabara, afya n.k.

Issue inakuja, kama serikali iliyopi inatumia ndivyo sivyo pesa hizo kinyume na matarajio yaliyokusudiwa na ikitokea serikali au kiongozi mwingine akaingia madarakani nakugundua pesa za bond zilitumika vibaya anaweza akafanya maamuzi magumu na msimfanye chochote hii ndio ilikuwa point yangu.

Kuhusu kushuka thamani kwa fedha au mfumuko wa bei ni jambo rahisi tu kuelewa halihitaji kujua uchumi. Mfano mfuko wa cement kwa sasa ni elfu 15 ukitaka kujenga, au tofali ni shiling I elfu Moja ila baada ya miaka mitano au kumi mfuko huo huo utaununua kwa shiling 25, 000/ na tofali kitakuwa shilingi elfu tatu kwa hiyo hata kama utapata ongezeko la faida ya asilimia 10 bado haitakusaidia.
 
Nsekela kajipambanua kuwa chawa wa mtu hata ufanisi wa hiyo bond hautakuwepo!

Kuna uzi wa malalamiko humu kutoka kwa member kuhusu kutopata gawio lake!

Ni suala la muda tu,serikali ina uzoefu wa dhulma,watu watalizwa very soon.
 
Mnaokosoa hebu fikirieni kidogo. Mjue pale unaikopesha serikali sasa unataka uikopeshe alafu ikupe return 40% vipi miradi yao ikichemka, ujue lazima wakulipe hata mambo yakienda kombo maana kwao huo ni mkopo. Think about it like unamkopesha rafiki ako pesa na lazima tu akulipe baada ya muda ila atakuwa anakupa riba ya 12% kila mwaka. Mtu unaweka savings bank hadi milioni 2 kwa interest ndogo sana. Sasa kuliko usevu bank why usiwekeze hapa ukapa hizo 12% per anum.
Kuna mtu anasema bora akafuge kuku it's okay. Lakini ukumbuke bonds low risk au pengine ni 0% risk na baada ya bond kumature unapata pesa yako kamili so inaweza kuwa mbinu ya kusave pesa kwa ajili ya malengo yako ya baadae huku ukiendelea kupata interest.
Toa pesa bank savings ilete huku. Hii haihusiani na zile issue za politics sijui utekaji najua watu hapa wanaponda kwa sababu wanaona jina la ( ) hilo ni jina tu wakuu.
Sema mama nae aache kuteka watu bwana heee natania bhn.
Anyway mapenzi yafutwe.
 
Back
Top Bottom