Unataka kufanya uwekezaji basi wekeza huku

Pule

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
412
Reaction score
767
Kuna baadhi ya sehemu ukiwekeza ni uhakika ila tulio wengi hatujui na hatufahamu kuhusu hili.mfano kuna kitu kinaitwa Samia Infrastructure Bonds ni hati fungani mahsusi inayotolewa na benki ya CRDB kwaajili ya kufadhili miradi muhimu ya miundombinu nchini Tanzania, hasa ujenzi wa barabara chini ya wakala wa barabara Vijijini na mjini (TARURA).

Miradi hii inaongeza mtandao usafiri nchini,ikiboresha Kwa kiasi kikubwa usafiri wa mjini na Vijijini. Bondi hii inalenga kukusanya Tzs bilioni mia hamsini. Tzs(150,000,000,000/=) na imepitiwa na kuidhinishwa na mamlaka ya masoko ya mtaji na dhamana CMSA. Hii inahusisha Kwa watu binafsi na makampuni.

Kwa watu binafsi,wanaotafuta UWEKEZAJI salama na wenye faida Kwa muda wa kati ya (miaka 5)huku pia wakichangia katika maendeleo ya taifa.

Kwa makampuni,biashra na taasisi zinazopendelea UWEKEZAJI salama unaougwa mkono na serikali unaendana na malengo ya uwajibikaji wa kijamii wa kampuni na ukuaji wa kifedha basi hii ni sehemu salama ya kuwekeza.

FAIDA NA GAWIO
Bondi hii inatoa riba ya asilimia 12 kwa mwaka,inayolipwa Kila robo ya mwaka ndani ya kipindi Cha miaka mitano.

Kwa mfano,
Ikiwa utawekeza TZS 1,000,000/= kwenye bondii ya miundombinu ya Samia yenye riba ya 12% Kwa mwaka utapata riba ya TZS 120,000 Kwa mwaka. Riba hii inalipwa Kila robo mwaka,kwa hivyo Kila miezi mitatu utapokea TZS 30,000/=

(NB) Faida inaongezeka kutoka na kiasi ulichowekeza

Jinsi ya kuwekeza Bondi
(1) Kwa wateja wa CRDB Bank
Pakua au fungua app ya simbanking chagua huduma>Samia bond >wekeza sasa > kisha endelea kufuata maelekezo .

(2) Kwa wateja wa banki zingine
Tembelea tawi lolote la banki ya CRDB kujaza fomu au pakua kutoka kwenye tovuti yetu ujaze kwa umakini,kisha peleka tawini watazipokea.

(NB) Kwa maelekezo zaidi ingia google andika (Samia Infrastructure Bonds)
(See You At the Top)
 
Mmh jamani elf 10 per month? Hapana 🚮
 
Hakuna investor makini atathubutu kuwekeza kwenye hati fungani kama hiyo. Imekaa kichawa chawa sana. What if umewekeza na Samia au CCM isirudi madarakani? Kwa ujumla hizo bond za serikakali kama serikali ikianguka au mapinduzi kutokea au akija mtawala mwingine anaweza akabadili mifumo na kuwachinjia baharini.

Pia hizo bond ni hasara sababu kunakuwa na inflation na thamani ya pesa inabadilika kwa kushuka.

Ukiona unaitwa kwenye fursa ujue wewe ndio fursa na ukipewa bidhaa ya bure utambue kuwa wewe ndio bidhaa.
 
Kuna vitu Huwa vinabakia hata iweje mfano masuala ya treasure bond Huwa hayabadiliki na watu watalipwa stahiki zao Kama makubaliano yanavyosema
 
Ajabu sana nadhani watakuwa na Target zao , lakini kwa mtu unayepambana, kuwekeza hela yako huko ni kama kuizika tu 🤒
Hmna sio kuizika Fanya hesabu Kwa aliyewekeza 5m anapata shingpi? Kama faida
 
Back
Top Bottom