Unataka kuagiza gari??... pitia hapa kwanza

dullymo

Senior Member
Joined
Aug 21, 2009
Posts
105
Reaction score
5
hello JF bros n sisz!
watu wengi wamekuwa wakitaka kuagiza magari kwa njia ya mtandao. ni njia rahisi na inayosave muda na gharama nyingine kama nauli nk na unapata gari kwa bei poa. mimi ni miongoni mwa wanaoleta magari kwa njia hiyo na nigependa niwape points muhimu ambazo zitawasaidia wale wanaotaka kuleta magari kwa njia hiyo.

WAKATI WA KUNUNUA
1. makampuni mengi siku hizi yanaweka picha za magari lakini magari hayo hayapo katika stock yao.
2. unaweza kulipia gari kisha ukaambiwa gari hilo limenunuliwa na mtu mwingine kwa hiyo wanakuletea gari linalofanana na lile. wanaweza wakakupa kwa bei ile ile, au kwa bei ndogo na wakakurudishia chenji au wakakwambia uongeze pesa zingine.
3. unaweza ukatuma pesa na huyo ulomtumia akaingia mitini. yaani ukaibiwa usipate chochote na hata ukimfuatilia unaweza kupoteza muda tu. mfano katika trdcarview kuna makampuni yamewekwa kwenye blacklist kwa makosa tofauti.

GARI KWENYE MELI.
4. unaweza ukanunua gari vizuri na meli ikaingia ila documents zikachelewa kufika then hapo unatakiwa ujiandae na storage kubwa.
5. meli inaweza kupata chochote wakati ipo kwneye maji so ni vyema iwapo utalipia na insurance yaani CIF na sio CNF.
6. sometimes meli inawahi kuingia kuliko ilivyotarajiwa na hii ni mbaya iwapo utakuwa hufuatilii movements za meli bandarini.
7. gari inaweza kucheleweshwa kutuma hata kwa zaidi ya mwezi mzima gari haijatoka japan.

GARI IKISHAFIKA BANDARINI
7. baadhi wameletewa gari zina sctratch na dent tofauti na walizoziona kwneye picha ambazo zimekuwa edited.
8. kuna washenzi wana tabia ya kuchomoa vitu muhimu ndani ya gari kama vile power windows, cd players, cd changers, screens nk.
9. gari inaweza kuchunwa au kukwanguliwa wakati ipo bandarini na huna wa kumlaumu.

KULIPIA USHURU TRA
10. mtandao wa TRA haupo stable kabisa na hiyo ndio sababu kubwa wanayoitumia siku hizi katika kuchelewesha kutoa documents za kulipia ushuru. yaani kukupa assesment.
11. TRA hawakupi ushuru kulingana na invoice yako uliyonunulia badala yake wanakupangia ushuru kwa bei wanayotaka wao. mfano umenunua gari kwa CIF $2500 wao wanaweza kukupigia ushuru wa bei ya USD 3500
13. registration ya gari huwa inachukua kati ya wiki 1 mpaka mwezi mzima otherwise utoe kidogodogo.

MUHIMU
- wakati unaagiza gari usisahau kuwaambi wakufanyie JAAI inspection ambayo inacost kama usd 200- 350. usipofanya huku watakuja kukufanyia kwa zaidi ya 700,000 na kukuongezea storage charge bure.
- ukiambiwa kwa mfano gari hilo linacost ml5 kuanzia kulinunua mpaka kulisajili ni vizuri ukajindaa na ml6 au zaidi maana baadhi ya vitu havina guarantee mfano ushuru wataokupa tra, storage charge, agent fees, shipping line agent fees nk.
- ni vizuri ulete gari isiyozidi miaka 10 na isiyozidi CC 2000 (exept magari ya mizigo na mabasi) maana haina kodi ya uchakavu na excess duty.

- unapolitoa gari lako bandarini hakikisha umeandikisha vibao vinavyoonyesha chasis namba, umekatia insurance angalau ya wiki 1, ina triangle na fire extinguisher ili kukwepa usumbufu wa askari barabarani nk.

wadau kama nimesahau kitu ni vizuri kuongezea mimi ni binadamu.
nategema hii itakuwa useful kwa wale wanaotaka kuanza kuimport magari.
 
Asante Dullymo kwa maelezo yaliyojitosheleza.

Kwa sala la vitu kuchomolewa bandarini, kuna mtu anayefanya kazi kwa C&F agent flani aliniambia kwamba una haki ya kuwadai bandari. Jamaa anadai usi-sign kuipokea gari kabla ya kuifanyia uchunguzi na kuahakikisha kila likichoko kwenye BOL kipo. Kama vitu vimeandikwa kwenye BOL, kwa mfano radio, na ukakuta imenyofolewa, una haki ya kuwadai bandari. Na watakulipa. Je, hii ina ukweli gani?

Kwa suala la ushuru wa TRA, mbona kuna wengine kama kina Next Level wanadai wanatumia CIF yako unless kuna dalili za wewe kutaka kudanganya? Na hiyo bei wanayoitaka wao inaamuliwa vipi? Je, wana table za bei kwa kila aina ya gari? Kama sio, basi wao wanazitoa wapi hizo bei?

Na kama TRA wanapanga bei randomly kiasi hicho, inamaana watu wawili mnaweza kuagiza gari mbili zinazofanana kabisa halafu mkapangiwa bei tofauti? Kama ndio hivi, sasa huu sio uhuni tunaotakiwa tuutolee macho badala ya kukubali kwamba ndio utaratibu sahihi? Je, nikiagiza starlet CIF $3,000 wakiniambia ni $30,000 kwa sababu tu sura yangu mbaya inabidi nikubali tu imekula kwangu?

Ukweli hasa wa hii dhana ya TRA kujipangia bei uko wapi? Maana wengine wanasema hawafanyi hivyo wengine wanasema wanafanya? Na kama wanafanya hivyo, je, hii sio aina fulani ya ufisadi na wizi? Na, mbona watu (hasa madalali) wanalichukulia kama kitu cha kawaida?
 
Asante Dullymo kwa maelezo
hiyo BOL umemaanisha Bill OF lading? kama ni hiyo huwa hawaandiki options za gari zaidi ya chasisi no na mwaka tu. hata ukisema ubishane bandarini kwa kuibiwa dvd player ya laki 1 lakini ikasababisha ujiongezee storage huoni utakuwa unapoteza muda bure bila ya kupata chochote.
pia inawezekana kabisa kwa watu wawili kuleta gari sawasawa ila mkalipia ushuru tofauti. hayo yalinikuta mie mwenyewe nilinunua toyota raum 2 zote za mwaka 2000 ila moja walinipiga ushuru 1.7ml na nyingine walinipiga 2.2ml.
 
Hii imetulia mkuu. Nadhani ungeongezea mchakato wa ku calculate makato yote ya TRA - kama Dumping Fee, Import Duty, Exercise Duty, VAT etc. Hope Itakuwa reference nzuri hapa JF.

Pia, tungetengeneza listing ya online sites zote ambazo can be considered SAFE kutokana na uzoefu wa watu tofauti.

Hayo ndio maoni yangu mkuu.
 
Asante Dullymo kwa maelezo
hiyo BOL umemaanisha Bill OF lading? kama ni hiyo huwa hawaandiki options za gari zaidi ya chasisi no na mwaka tu. hata ukisema ubishane bandarini kwa kuibiwa dvd player ya laki 1 lakini ikasababisha ujiongezee storage huoni utakuwa unapoteza muda bure bila ya kupata chochote.
pia inawezekana kabisa kwa watu wawili kuleta gari sawasawa ila mkalipia ushuru tofauti. hayo yalinikuta mie mwenyewe nilinunua toyota raum 2 zote za mwaka 2000 ila moja walinipiga ushuru 1.7ml na nyingine walinipiga 2.2ml.

Niliasume ni BOL, lakini inawezekana nimekosea, itabidi nimtafute huyu jamaa anieleze kwa uhakika. Huyu jamaa anafanya kazi kwenye moja ya C&F agents. Na kazi yake ndiyo hiyo: ku clear magari pale. Na akanihakikishia kwamba kuna document (mimi nika-assume ni BOL) ambayo inasema nini kipo kwenye gari, na ni jukumu lako kuhakiki kwamba gari ipo hivyo. Na akaniambia ukigundua kwamba kunatofauti kuna jinsi ya ku-ripoti hiyo na ukawadai. Na akaniambia uki-sign kabla huja hakiki halafu ukarudi baadaye, ndio imekula kwako. Je, amenidanganya? Ila mimi sikuona kama ana sababu ya kunidanganya, na ukichukulia ni mshakaji tulikuwa naye long time.

Kuhusu kulipishwa tofauti kwa gari aina hiyo hiyo, kinachonichangaza hapa ni jinsi mzee unavyoona hiyo ni sawa, na jinsi watu wengine wanavyoona utaratibu huu ni sawa. Hivi hakuna jinsi ya ku-apeal? hata kama ni baada ya kulitoa gari? Usiniambia inachukua mda mrefu kufuatilia hiyo apeal, nataka nijue tu kama huo utaratibu upo niwe mtu wa kwanza kuufuata.
 
Asante Dullymo kwa maelezo

Niliasume ni BOL, lakini inawezekana nimekosea, itabidi nimtafute huyu QUOTE]
yup hiyo documents inayoonyesha vitu vilivyokuwepo kwneye gari ipo but sio B/L. ah mzee wao wameshika mpini mimi nimeshika makali so sikutaka hata kubishana nao as long as gari zangu nikawa nishazitoa. lakini cha ajabu mara ya kwanza nilinunua gari kwa bei rahisi nikalipia ushuru 2.2ml ila nikaleta gari nyingine ya model hiyo hiyo ila bei ilikuwa juu kidogo lakini maajabu yake ushuru ukawa mdogo 1.6ml. yaani ukifuatilia sana kichwa kinaweza kupasuka
 
Asante Dullymo kwa maelezo

Niliasume ni BOL, lakini inawezekana nimekosea, itabidi nimtafute huyu jamaa anieleze kwa uhakika. Huyu jamaa anafanya kazi kwenye moja ya C&F agents. Na kazi yake ndiyo hiyo: ku clear magari pale. Na akanihakikishia kwamba kuna document (mimi nika-assume ni BOL) ambayo inasema nini kipo kwenye gari, na ni jukumu lako kuhakiki kwamba gari ipo hivyo. Na akaniambia ukigundua kwamba kunatofauti kuna jinsi ya ku-ripoti hiyo na ukawadai. Na akaniambia uki-sign kabla huja hakiki halafu ukarudi baadaye, ndio imekula kwako. Je, amenidanganya? Ila mimi sikuona kama ana sababu ya kunidanganya, na ukichukulia ni mshakaji tulikuwa naye long time.

Kuhusu kulipishwa tofauti kwa gari aina hiyo hiyo, kinachonichangaza hapa ni jinsi mzee unavyoona hiyo ni sawa, na jinsi watu wengine wanavyoona utaratibu huu ni sawa. Hivi hakuna jinsi ya ku-apeal? hata kama ni baada ya kulitoa gari? Usiniambia inachukua mda mrefu kufuatilia hiyo apeal, nataka nijue tu kama huo utaratibu upo niwe mtu wa kwanza kuufuata.

Wakuu,

Kwa uzoefu wangu kila gari kabla ya kuteremshwa kutoka melini uwa linafanyiwa inspection. Bandari wanayo karatasi ambayo ina orodha ya vitu vyote vinavyopashwa kuwa kwenye gari la kawaida. Wanachofanya wao wakati wa inspection wana tick kila kitu walichokiona wakati gari linashuka. Hiyo karatasi anapewa agent aisome na kulinganisha na vitu vilivyomo kwenye gari against hiyo karatasi. Endapo utakuta walionyesha kwamba power window ipo halafu agent asiikute wakati wa kukabidhiwa gari, then Bandari wanapashwa wakulipe.

Tatizo ni kwamba hao wanaofanya hiyo inspection wakati gari linashuka ndio hao wanaochomoa hivyo vitu na kuweka X kwenye kisanduku husika kwamba hicho kitu kwa mfano radio haimo. Ukweli ni kwamba inakuwepo lakini wakiishaonyesha kwamba haikuwemo basi wanapokwenda kuweka gari kwenye maegesho wanatoa vitu vyote walivyoonyesha kwamba havimo. Agent akienda kupewa gari anaona kabisa kwamba radio hamna na karatasi ya Bandari inaonyesha kwamba wakati wanapokea gari radio haikuwemo. Wakati huo meli imeisha ondoka ukimuuliza supplier anakwambia kila kitu kilikuwemo.

Nimeyakubali maelezo ya aliyepost hii habari kuhusu some companies huko Japan ambao wameanza kufanya mchezo mchafu wa kuwaonyesha watu gari ambalo ni zuri na labda la mwaka 2003 halafu wanakuweka bei kidogo. Wanakwambia ukituma 50% wanakuwekea hilo gari mpaka utakapomalizia hizo nyingine. Ukituma pesa wanaconfirm kuzipokea lakini wanakwambia bahati mbaya kuna mtu alituma pesa ametangulia kwa hiyo wewe uchague gari nyingine. Hawa jamaa wa Japantradecar walijaribu kunifanyia mchezo huo nikawatolea nje na kuwataka warudishe pesa zangu. Pesa wamezirudisha lakini wamenikata USD 100 eti ni administration fee. Jihadhari kabisa na watu hao.

Tiba
 
MUHIMU
- wakati unaagiza gari usisahau kuwaambi wakufanyie JAAI inspection ambayo inacost kama usd 200- 350. usipofanya huku watakuja kukufanyia kwa zaidi ya 700,000 na kukuongezea storage charge bure.
- ukiambiwa kwa mfano gari hilo linacost ml5 kuanzia kulinunua mpaka kulisajili ni vizuri ukajindaa na ml6 au zaidi maana baadhi ya vitu havina guarantee mfano ushuru wataokupa tra, storage charge, agent fees, shipping line agent fees nk.
- ni vizuri ulete gari isiyozidi miaka 10 na isiyozidi CC 2000 (exept magari ya mizigo na mabasi) maana haina kodi ya uchakavu na excess duty.

- unapolitoa gari lako bandarini hakikisha umeandikisha vibao vinavyoonyesha chasis namba, umekatia insurance angalau ya wiki 1, ina triangle na fire extinguisher ili kukwepa usumbufu wa askari barabarani nk.

wadau kama nimesahau kitu ni vizuri kuongezea mimi ni binadamu.
nategema hii itakuwa useful kwa wale wanaotaka kuanza kuimport magari.

Mkuu asante kwa hili. Hapa penye nyukundu mimi mbona sijaelewa. Maana nilileta gari toka UK sikuambiwa hili au ni kwa ajili ya magari yanayoagizwa toka Japan?
 
Wakuu,

Kwa uzoefu wangu kila gari kabla ya kuteremshwa kutoka melini uwa linafanyiwa inspection. Bandari wanayo karatasi ambayo ina orodha ya vitu vyote vinavyopashwa kuwa kwenye gari la kawaida. Wanachofanya wao wakati wa inspection wana tick kila kitu walichokiona wakati gari linashuka. Hiyo karatasi anapewa agent aisome na kulinganisha na vitu vilivyomo kwenye gari against hiyo karatasi. Endapo utakuta walionyesha kwamba power window ipo halafu agent asiikute wakati wa kukabidhiwa gari, then Bandari wanapashwa wakulipe.

Tatizo ni kwamba hao wanaofanya hiyo inspection wakati gari linashuka ndio hao wanaochomoa hivyo vitu na kuweka X kwenye kisanduku husika kwamba hicho kitu kwa mfano radio haimo. Ukweli ni kwamba inakuwepo lakini wakiishaonyesha kwamba haikuwemo basi wanapokwenda kuweka gari kwenye maegesho wanatoa vitu vyote walivyoonyesha kwamba havimo. Agent akienda kupewa gari anaona kabisa kwamba radio hamna na karatasi ya Bandari inaonyesha kwamba wakati wanapokea gari radio haikuwemo. Wakati huo meli imeisha ondoka ukimuuliza supplier anakwambia kila kitu kilikuwemo.

Nimeyakubali maelezo ya aliyepost hii habari kuhusu some companies huko Japan ambao wameanza kufanya mchezo mchafu wa kuwaonyesha watu gari ambalo ni zuri na labda la mwaka 2003 halafu wanakuweka bei kidogo. Wanakwambia ukituma 50% wanakuwekea hilo gari mpaka utakapomalizia hizo nyingine. Ukituma pesa wanaconfirm kuzipokea lakini wanakwambia bahati mbaya kuna mtu alituma pesa ametangulia kwa hiyo wewe uchague gari nyingine. Hawa jamaa wa Japantradecar walijaribu kunifanyia mchezo huo nikawatolea nje na kuwataka warudishe pesa zangu. Pesa wamezirudisha lakini wamenikata USD 100 eti ni administration fee. Jihadhari kabisa na watu hao.

Tiba

Asante kwa maelezo mazuri, kidogo naanza kupata picha.

Sasa jamani kama wezi wadogo wanatushinda akili hivi, mafisadi papa tutawaweza kweli? tehetehe

Mimi nadhani kuna kitu tunakiruka hapa, sidhani kama taratibu zina holes hivyo kiasi kwamba ni rahisi hivyo mtu kuibiwa bila kuwa na la kufanya. Na kutokujua kwetu ndio kunawapa nafasi hawa wezi kufanya wanachofanya.

Kama huo ndio ungekuwa ukweli wote then maana yake gari ikiwa kwenye meli, mbaharia wanaweza kufanya chochote, na huna la kufanya. Kitu ambacho si kweli. Je, hakuna makabidhiano kati ya meli na bandari? Inamaana mwenye meli anaweza akaiharibu gari na usiwe na cha kufanya?
 
Last edited:
Asante sana mheshimiwa nikipata mshiko wa kununua gari nitayafanyia kazi mie
 
Dullymo,
ebu tusaidie kuhusu tradecarview Maana hawa watu wanauza magari kwa bei poa sana na kuna makampuni mengi saana, sasa hayo ambayo wameyawekea lable kwamba ni ya kitapeli ni yapi???????????? Msaada kaka.
 
Asante Dullymo kwa maelezo yaliyojitosheleza.

Kwa sala la vitu kuchomolewa bandarini, kuna mtu anayefanya kazi kwa C&F agent flani aliniambia kwamba una haki ya kuwadai bandari. Jamaa anadai usi-sign kuipokea gari kabla ya kuifanyia uchunguzi na kuahakikisha kila likichoko kwenye BOL kipo. Kama vitu vimeandikwa kwenye BOL, kwa mfano radio, na ukakuta imenyofolewa, una haki ya kuwadai bandari. Na watakulipa. Je, hii ina ukweli gani?

Kwa suala la ushuru wa TRA, mbona kuna wengine kama kina Next Level wanadai wanatumia CIF yako unless kuna dalili za wewe kutaka kudanganya? Na hiyo bei wanayoitaka wao inaamuliwa vipi? Je, wana table za bei kwa kila aina ya gari? Kama sio, basi wao wanazitoa wapi hizo bei?

Na kama TRA wanapanga bei randomly kiasi hicho, inamaana watu wawili mnaweza kuagiza gari mbili zinazofanana kabisa halafu mkapangiwa bei tofauti? Kama ndio hivi, sasa huu sio uhuni tunaotakiwa tuutolee macho badala ya kukubali kwamba ndio utaratibu sahihi? Je, nikiagiza starlet CIF $3,000 wakiniambia ni $30,000 kwa sababu tu sura yangu mbaya inabidi nikubali tu imekula kwangu?

Ukweli hasa wa hii dhana ya TRA kujipangia bei uko wapi? Maana wengine wanasema hawafanyi hivyo wengine wanasema wanafanya? Na kama wanafanya hivyo, je, hii sio aina fulani ya ufisadi na wizi? Na, mbona watu (hasa madalali) wanalichukulia kama kitu cha kawaida?

We come back on this.....nikotight kidogo na ''mabox'' ya bongo!
 
Waheshimiwa,

Kwa sehemu nakubaliana na maelezo ya kuagiza gari kwa njia ya mtandao kuwa ni gharama nafuu lakini kuna hasara zake. Waswahili wanasema rahisi ghali!!

Nilipata uzoefu mwaka 2005 baada ya kuagiza gari toka Japan kwa kupitia agent mmoja hapo Dar kwa makubaliano kwamba gari langu nitalipata baada ya mwezi mmoja kwa gharama ya 2,500 USD wenyewe wanaita CIF(Cost Including Freight).

Aina ya gari niliyotaka ilikuwa ni Mark II Baloon mettalic Blue, Manual Transmission,Petrol Engine,4 doors, PW na iwe ni 4 cylinders. Baada ya jamaa kumlipa ile pesa ilichukua miezi 2 mpaka gari hiyo kufika Bandari ya Dsm. Kama hiyo haitoshi tulivoenda kuikagua ile gari kwa ajili ya Clearence ilikuwa haina vigezo karibu vote nilivyotaka!

Kweli ilikuwa ni Baloon metallic Blue safi inawaka. Lakini ikawa ni Automatic Transmission, Diesel engine na kibaya zaidi ikawa ni 6 cylinders. Kidogo nishawishike kuikubali lakini nikaona itanisumbua baadaye.Pale pale Agent nikamwambia hiyo haikuwa gari niliyokuwa nimeagiza. Na kwa vile nilikuwa nimesubiri kwa miezi 2 nikamwambia sina muda wa kuendelea kusubiri gari tena bora arudishe hela yangu nitafute gari sehemu nyingine.

Unajua aliniambiaje? Nisubiri mpaka gari hiyo ipate mnunuzi ndipo arudishe hela yangu! Aliniambia nimpe 1 week ya kufanya logistics za kuindoa bandarini na kutafuta soko. Believe me it took me another 1 month ya kusubiri mpaka nikaamua kuwatumia polisi ili kumshinikiza jamaa aweze ku-refund pesa yangu. Hata hivyo jamaa alikubali mbele ya polisi na akaanza kunilipa kidogo kidogo mara leo milioni 1, kesho laki 5, mara laki 3 mpaka nikawa bored stiff.Hiyo nayo ilichukua kama mwezi na zaidi. Kwa hiyo jumla ya muda wote ikawa kama miezi 4 na zaidi.

Uamuzi niliochukua baada ya hapo ilikuwa kwenda kwenye show room za Bongo nikachagua gari niliyotaka nikalipa hela yangu na kuondoka na mashine. Niliona kuagiza gari toka Japan au Arabuni ni upuuzi na kupoteza muda.

Conclusion yangu ni kuwa,be careful na hawa watu wanaojifanya ni agents wa kuagiza magari au kukuletea gari baada ya kui-pick kwenye mtandao mara nyingi ni matapeli na wababaishaji. Kuna jamaa zangu wengi wamewahi kulizwa kwa mtindo huu wa kumtumia mtu akuletee gari. Kuna rafiki yangu aliletewa gari ikiwa ina chemsha kama unapika maharagwe na kwenye mtandao ilikuwa inaonekana bomba na bandari ilipofika ni exactly kama ilivokuwa inaonekana kweny mtandao,lakini inachemsha!!

Kwa hiyo jamaani be careful. Kama una hela yako ni afadhali ukanunue gari yako kwenye show room zetu za Bongo unaweza kupata gari nzuri tu na ukaepuka usumbufu na gharama za kipuuzi zisizo za lazima.

Wakatabahu,

makoye.
 
Mkuu asante kwa hili. Hapa penye nyukundu mimi mbona sijaelewa. Maana nilileta gari toka UK sikuambiwa hili au ni kwa ajili ya magari yanayoagizwa toka Japan?

magari toka uk yanatakiwa yawe na MOT iliyo valid.
 
Dullymo,
ebu tusaidie kuhusu tradecarview Maana hawa watu wanauza magari kwa bei poa sana na kuna makampuni mengi saana, sasa hayo ambayo wameyawekea lable kwamba ni ya kitapeli ni yapi???????????? Msaada kaka.

kwenye mtandao wa tradecarview bonyeza kisanduku cha help hapo utaona neno la black list bonyeza utayaona hayo makampuni.
 
Asante wachangiaji Wote Raha ipo hapa kwangu Niliagiza Gari 3 aina ya Mitsibishi Grandis Cheriot 2 za 99 iliobaki 98 ajabu zile za 99 nimelipa Mil3.2 kwa kila moja ila ya 98 niliandikiwa ktk accesmnt ya kulipa 2.6 Hivi hawa jamaa wanafuata vigezo gani? Sielewi
 
Inaelekea wewe si mtaalam sasa katika ili CIF sio COST INCLUDING FREIGHT bali ni COST INSURANCE FREIGHT- umenipata nipo katika fani hii zaidi ya miaka 12.
 
Back
Top Bottom