Unataka kuachana na uzinzi? Soma hapa

Unataka kuachana na uzinzi? Soma hapa

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,023
Reaction score
36,865
Watu uliofanya nao uzinzi, nafsi zao hubakia ndani yako kwa kazi maalum. Soma hii:
  1. Ili kututesa.
  2. Kuja katika ndoto, na kushiriki uzinzi na sisi.
  3. Kutuzuia tusioe au kuolewa.
  4. Kutuvurugia amani na upendo kwenye mahusiano mengine au ndoa.
  5. Kujichua kupitia nafsi zao.
  6. Kutufanya tuwe makahaba kwa kutamani kulala na kila mwanaume/mwanamke mpya mbele ya macho yetu.
Siku ya leo nitakupa mwongozo wa maombi utakao tumia kujitenga na kila nafsi ya mtu yeyote iliyo ndani yako inayozuia na kuharibu maisha yako—usiingie kwenye ndoa, inayozuia usipate mahusiano na usiolewe wala kuoa, inayofanya uendelee na uzinzi na ukahaba, inayofanya ujichue mara kwa mara.

Kuna nafsi za watu wengi zinaishi ndani ya mtu kumtesa kulingana na watu aliowahi kushiriki nao uzinzi. Kila aliyeshiriki uzinzi na wewe, nafsi yake hubaki ndani yako kukutesa na wakati mwingine kukuzuia usipate mume/mke mwingine, ili abaki yeye tu katika ulimwengu wa roho.

Akiwa ni mwanaume mmoja, basi kunakuwa na nafsi moja.
Wakiwa ni wawili, basi kunakuwa na nafsi mbili.
Wakiwa watano, basi kunakuwa na nafsi tano zikishindanda ndani ya mtu, na mara nyingi zinamsumbua hata usiku kwa kumbukumbu za matukio, na mara nyingi zinamsumbua kwa kuja katika ndoto kushiriki naye tendo, n.k.

Leo tutajitenga nazo.
Kila unayemkumbuka, jitenge naye.
Kata mawasiliano.
Kataa nafsi yake inayoishi ndani yako.
Kataa ile roho (spirit) inayoishi kwako.

Simamia hii mistari, soma kwa umakini:
  • Mithali 3:32–33
  • 1 Wakorinto 6:15–19
Nafsi zetu zikishashiriki uzinzi tu, zinakuwa chafu kwa kushambuliwa na kila adui wa kuzimu, wakidhania tumeshaungwa nao kuwa kitu kimoja. Zinakuja ndani yetu kutaka ushirika, maana zilikuwa na ushirika na fulani uliyelala naye.

Wakati mwingine, kama wale ulio lala nao walikuwa na nafsi zinazoishi ndani yao, basi unapolala nao, zile nafsi pia huja ndani yako. Ukiunganisha na ya kwake, basi linakuwa jeshi kubwa.

Ushuhuda:
Rafiki mmoja alikuwa na mahusiano na binti mmoja, walilala pamoja sana na kushiriki uchafu... Itaendelea.
 
Ni kweli kabisa ..
Hata ndoa nyingi na mahusiano yao kutodumu ni sababu ya Roho ya Uzinzi ya wale walioshiriki nao Zinaa...

Niongeze na neno kutoka
Zaburi 51...
Kuomba Toba na Rehema kwa kumaanisha zaidi...
 
Zaburi 51..
Bonge moja la neno!

Zaburi 51​


Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima.

 
Mithali 3:32–33
Bonge moja la neno.

30 Usishindane na mtu bila sababu,
Ikiwa hakukudhuru kwa lolote.


31 Usimhusudu mtu mwenye ujeuri,
Wala usiichague mojawapo ya njia zake.


32 Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA,
Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.


33 Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu,
Bali huibariki maskani ya mwenye haki.


 
  • Thanks
Reactions: _ly
Back
Top Bottom