Unashindwaje kutengeneza 30,000 kwa siku Dar es Salaam?

Sivan

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
923
1,223
"Inakuwaje wewe Graduate unaishi Dar unashindwa kutengeneza 30,000 kwa kila siku Consistently"

Nimemnukuu jamaa hapa stationary moja nikitoa copy yule kama si Motivesheni Spika itakuwa ni Keyboard Worrior.

NB: Sikuambiwa mimi ni maongezi yao siwafamu.
 
Hela hiyo inatengenezeka ila kwa kazi za kuchosha sana na ambazo wasomi wanaona aibu..

Fungua goli la msosi ama juice sehemu yenye watu wengi uone balaa lake na uzuri wa awamu hii hata Posta unaweza fungua genge na hakuna mgambo wala mtu wa kukugusa.
 
Hela hiyo inatengenezeka ila kwa kazi za kuchosha sana na ambazo wasomi wanaona aibu..

Fungua goli la msosi ama juice sehemu yenye watu wengi uone balaa lake.. na uzuri wa awamu hii hata posta unaweza fungua genge na hakuna mgambo wala mtu wa kukugusa
Alafu Sera ya mgombea urais kusema ataboresha maisha ya watanzania alafu mwisho wa mkutano anaanza kuwaomba wamchangie hela hao hao anaosema ni masikini wameharibiwa maisha na CCM aache kabisa.

Kama ni masikini wa kutupwa hizo hela wanazokuchangia wanatoa wapi.

Lisu acha kupotosha watu
 
Hela hiyo inatengenezeka ila kwa kazi za kuchosha sana na ambazo wasomi wanaona aibu..

Fungua goli la msosi ama juice sehemu yenye watu wengi uone balaa lake.. na uzuri wa awamu hii hata posta unaweza fungua genge na hakuna mgambo wala mtu wa kukugusa
Kaka biashara inayokupa quick income kwa dar ni biashara za kutembeza bidhaa isiyozidi buku jero. Hata ukiwa na goli ila mweke mtu golini wewe mweyewe ingia front sambaza sana bidhaa maeneo ya karibu na goli lako na wale watakao kuja golini wanakutana na mtu mwengine anawapasua kwa kwenda mbele...ukiweka kaubunifu tu katakao kutofautisha hata nukta na wengine basi lazma uwabane mbavu
 
Kuna mwamba kanitukana na kunifanyia matusi kitaani kwangu..nilitaka kufungua cafe ila nikasita..mjuba kaja na turubai tu kalifunga pembezoni mwa stendi..anatengeneza bites za aina mbalimbali maziwa tangawizi na kahawa..anatubutua kishenzi.analugha za maskhara sana wakina mama wote kitaa wanampenda na watoto wadogo wanampenda kishenzi.
 
Back
Top Bottom