Unasemaje kuhusu India na Unyanyasaji wa Watanzania

Senator jr

JF-Expert Member
Apr 3, 2016
367
495
Kuwa Mwaafrika nchini India: Tunaonekana kama mashetani

_______________________________

Mwaka mmoja wa masomo nchini India umekuwa mgumu kwa Zaharaddeen Muhammed, 27. Anasoma shahada ya pili kemia kwenye chuo kikuu cha Noida International [University]. Kwa ni nchini Nigeria.

Anasema watu wa huko humuona tofauti na asiyeweza kuaminiwa. “Ninaongea kihindi na mara nyingi hucheka. Lakini ninapowapa watoto wa majirani biskuti, hawakubali,” alisema kwenye kongamano la Africa-India Solidarity huko New Delhi.

Anasema baada ya mwaka mmoja, ndoto yake kubwa bado hajaitimiza: kualikwa kwenye harusi ya Kihindi. "Sijawahi kwenda nyumbani kwa mhindi yeyote kama rafiki. Hakuna aliyewahi kunitembelea,” anasema Zaharaddeen.

Mapema mwaka huu, mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania alipigwa na kuvuliwa nguo hadharani huko Bangalore na kundi la watu wenye hasira waliokuwa wanalipiza kisasi cha ajali iliyosababishwa na mwanafunzi wa Somalia asiyemjua kabisa.

Zaharaddeen aliongelea tukio hilo la Bangalore: "Alikuwa akitembea tu hapo [mwanafunzi wa Tanzania]. Ingeweza kutokea kwa mtu yeyote kati yetu.” Hata kupata vyumba vya kupanga wakati mwingine huwa mtihani kwa watu weusi nchini India.

Rohtas, dalali wa nyumba anasema huambiwa na wamiliki wa nyumba kuwa asiwaoneshe watu weusi sababu huaminiwa kuwa wanafanya biashara za madawa ya kulevya na shughuli zingine za kihalifu.

Mwanafunzi mmoja wa kike alidai kuwa si wenye nyumba tu wenye imani hiyo: “Wauzaji wa maduka huangalia fedha ninazowapa kuhakikisha kama sio feki,” anasema. "Ni dharau na si haki. Sisi ni watu wenye furaha na wachangamfu. Lakini India tunajikuta tukiwa na hasira tu.” Kwa upande wa Ibrahim Djiji Adam, 25 mwanafunzi wa biashara kutoka Libya anasema: Mara nyingi tunaonekana kama mashetani, wauza unga au changudoa.” Chanzo: Al Jazeera #Regrann MIMI NAWACHUKIA SANA WAHINDI,NI WABAGUZI MNO,WANAWANYANYASA SANA WAAFRIKA NA WABONGO HUKO NCHINI KWAO,ILA WAO WAKIJA HUKU TUNAISH NAO VZR NA WAKO HURU KWA KILA KITU..HIKI KITU NI CHA MDA MREFU SANA NA SERIKALI IPO KIMYA AS IF HAKUNA UBALOZI WA TANZANIA HUKO INDIA...THIS Z UNFAIR KWAKWEL..MIM NINGEKUWA RAIS NINGEFUKUZA WAHINDI WOOTE KWENY HII NCHI!
 
Daah, niliingia supermarket moja pale Mumbai, nikashangaa jamaa ameinuka mlangoni alipokuwa akawa ananifuata kila row ninayoivuka, just kuangalia kama nitaficha kitu. Jamaa washenzi sana
 
Daah, niliingia supermarket moja pale Mumbai, nikashangaa jamaa ameinuka mlangoni alipokuwa akawa ananifuata kila row ninayoivuka, just kuangalia kama nitaficha kitu. Jamaa washenzi sana
Lakini cha ajabu huku kwetu ndio Waajiri wetu poor Tanzanians Daah yaani tunawaona ka Miungu
 
Back
Top Bottom