Unapotoka kusaliti (kuchepuka), unapokutana na mwenza wako hivi unajisikiaje?

Binafsi nilijaribu kuchepuka ( dhambi kwa mujibu wa imani yangu, na nimetubia hii dhambi sitoirudia tena hadi nakufa).

Huwa anajua nikibanwa na majukumu sana na muda ukiwa umeenda huwa nachukua hotel napumzika na huwa nampa taarifa, ni mwanamke na mama aliyetokea kuniamini sana kama mimi ninavyomuamini.

Sasa usiku mmoja sikuridi na nikawa nimepiga mechi ya nje ( demu wa kuota huko duniani ), wakati narudi home asubuhi, nikamuona mchumba anapita njia ya juu sijui alikuwa anaenda madukani, ikabidi mie nipite njia ya chini kumkwepa, nikakosa kabisa confidence ya kukutana nae wala hata kumsalimia uso kwa uso ( sijui aliona au hakuniona )...

Nikafika home nikaoga, nikawasha laptop nikaanza kupitia mambo mawili matatu, akarudi wala hakuniuliza kitu, akaniandalia chai akaniwekea mezani nae akaja kukaa pale tukaanza kupiga story mbali mbali huku tunakula ( moyoni mwangu nikawa nasema huyu kama akijua nilichofanya usiku wa leo sijui itakuwaje hapa, na cha ajabu mapenzi yake kwangu ndio yakazidi kweli kweli, utani mwingi, cheko nyingi na furaha iliyotamalaki moyoni mwake, ndio nikawa nakosa kabisa amani nikawa nafumba fumba macho kama usingizi vile umenipitia ili nimkimbie nikalale, kabla ya kunipa ruhusu ya kwenda kulala, anapotaka kutoka huwa lazima tupige magoti kidogo tuombe kwa pamoja ndio aendelee na issue zingine.. na kwenye kuomba ukawa mtihani mkubwa zaidi...

Kwa wengine mlipokutana na mazingira haya mlikuwa katika hali gani na mliweza kumudu vipi?

Kuna watu wa ajabu sana....yaani mchumba tu ndiyo unakosa amani? duh nyie ndiyo mnajiuaga mkikataliwa......mimi mara nyingi nikitoka kuchepuka ....niifika nyumbani moja kwa moja namgegeda wife bila kuchelewa...na ndiyo tabia yangu niliyoizoea miaka nenda rudi
 
Looh
Kuna watu wa ajabu sana....yaani mchumba tu ndiyo unakosa amani? duh nyie ndiyo mnajiuaga mkikataliwa......mimi mara nyingi nikitoka kuchepuka ....niifika nyumbani moja kwa moja namgegeda wife bila kuchelewa...na ndiyo tabia yangu niliyoizoea miaka nenda rudi
 
Kwakweli sitokaa nisahau kilichotokea mwaka jana. Niliandamwa na mapigo na mojawapo kubwa kabisa pigo la kwanza ni kujua mume wangu wa miaka kumi alikua ananicheat. Nilimwamini sana toka uchumba hadi ndoa. Yaani na yeye alikua anajua jinsi ninavyomwamini so akatake advantage. Nilifaham baada ya mchepuko kunipigia kimakosa...uchungu nilioupata hauelezeki. Nina miaka 30s lakini uzito uliporomoka mpaka 47 kg. Nilipata pressure ya kushuka mpaka nilikua nashindwa kutembea kwa kizunguzungu na kuishiwa nguvu. Nilikua nilitaka niondoke, kikwazo kikaja sikua na kazi. Mpaka leo sijakaa sawa.wanawake na wanaume mnaochepuka mnaumiza sana sana wenzi wenu. Hata kama mtasameheana na kuamua kuendelea, ndoa kamwe haitakua kama mwanzo hata ufanye nini. Hamjui tuuu. Hiki kitu kinanitesa hadi leo nikikumbuka jinsi nilivyokua najitahidi kutimiza majukunu yangu kama mke,mama na mlezi wa familia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom