Unapotelea wapi umakini wa vyombo/vyanzo vyetu vya habari?

Unapotelea wapi umakini wa vyombo/vyanzo vyetu vya habari?

Joined
Nov 9, 2014
Posts
5
Reaction score
1
Vyombo vya habari ni sehemu na kiungo muhimu kwenye jamii, katika kufundisha, kuelimisha na hata kuonya juu ya mambo yanayoendelea katika jamii husika.

Hapa nchini Tanzania, kama nchi zingine tunavyo vyombo vya habari kama Vituo vya Runinga, Magazeti, Redio n.k

Moja ya habari, Leo, katika gaziti la MTANZANIA - 9.02.2015 imesema na ninanukuu "Membe adaiwa kutetea mtandao wa kifisadi". Ukisoma habari hiyo, inasema Mh. Membe, akihutubia waumini wa kanisa la Wasabato nchini, alimsafisha Ndugu Maswi, Katibu Mkuu aliyesimamishwa Wizara ya Nishati na Madini, ambaye hivi karibuni amehusishwa na kashfa ya sakata la Tegeta ESCROW Account, gazeti hilo linasema Ndugu Membe amemsafisha Ndugu Maswi kuwa ni Mtu safi.

Kauli hii, na zingine nyingi ambazo zimenukuliwa na gazeti hilo zilizosemwa na wasomi wetu, wa taifa hili zinanishangaza sana na kunifanya nishangae umakini na weledi wa mwandishi huyo, lakini pia umakini wa wasomi wetu katika kuzungumzia na kuchambua mambo.

Mh. Benard Membe, alisema hivi, naomba niweke sahihi, kauli hiyo iliyopotoshwa na mwandishi Huyo, nanukuu " Serikalini wapo waumini wengi Wasabato wakiwamo Ndugu. Wassira, Sefue, Masaju, Maswi na wengine. Hivyo kuonyesha kuwa ni dhehebu kubwa na muhimu hapa nchini". Hii ni katika kutambua umuhimu wa Dini/Dhehebu na jinsi inavyokuza waumini wake katika kutetea na kuendeleza Ustawi na Misingi wa/ya Taifa.

Aidha alisema "tangu amekuwa kiongozi hajawahi kusikia mgogoro wa kidini kwa wasabato ama kati yao wenyewe au na dini nyingine. Hivyo hii ni ishara tosha kuwa dini hii inapenda AMANI".

Hiyo ndio kauli ya Mh. Benard Kamilius Membe.

Tunafahamu, mipango na mikakati yenye mbinu chafu na siasa za majitaka, iliyoandaliwa na inayoendelea kuandaliwa na Baadhi ya Ndugu wanaokisaka kiti cha Urais kwa hila na fitna nyingi wakitumia mbinu zao nyepesi sana, hafifu sana na zisizo na chembe ya akili. Tunawaambia, Mh. Membe, hachafuliki. Ngumu sana kumchafua mtu ambaye hachafuliki na hawawezi, ndio maana wanatafuta mambo mepesi mepesi kumchafua. HACHAFULIKI. Wanaohoji uadilifu wa Mh Membe, waulize, TUTAJIBU. Msiwe wavivu kufikiria kiasi hicho.

Na sisi tunawauliza, Waambieni uadilifu wenu watanzania. Msirudie mambo yaleyale kila siku na kutumia nguvu nyingi kutuaminisha UONGO. Ikulu haingiliki kwa UONGO, KUUNGA UNGA na UZUSHI.
 
Back
Top Bottom