Thad
JF-Expert Member
- Mar 14, 2017
- 13,367
- 31,532
Wasalaam wanajf!
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu kutafuta marafiki,wachumba na wenza mitandaoni kila kukicha. Hivyo ni vyema tukakumbushana mambo mbalimbali yanayojitokeza kabla,wakati na baada ya kutafuta mtandaoni.
SABABU:
Watu wengi wamekuwa wakiwashangaa watu wanaotafuta marafiki,wachumba au wenza mitandaoni. Jamii imejenga mtazamo hasi kwa watafutaji hawa wakisahau kuwa kuna sababu mbalimbali zinazopelekea watu kutumia mitandao kwa utafutaji huo. Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea:-
a) Kubanwa sana na kazi (u busy)
Kuna watu ambao muda wao mwingi wanautumia kufanya kazi kiasi kwamba hawapati nafasi ya kujichanganya na watu wanaowazunguka kama marafiki na majirani. Hivyo ni rahisi kwao kutumia muda mfupi kama saa moja kuwasiliana na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali mitandaoni. Lakini pia ni rahisi kuwasiliana na kufanya kazi kwa wakati mmoja.
b)Mazingira ya ugenini.
Wakati mwingine mazingira ya ugenini huwafanya watu wajione wapweke na hivyo huamua kutumia mitandao kupata marafiki kirahisi sana. Mfano,mmoja kati ya marafiki zangu alikiri kuwa aliamua kutumia mtandao wa badoo alipokuwa nchini China kwasababu ya upweke aliokuwa nao.
c)Hulka ya kutojichanganya.
Kuna watu hawapendi mitoko wala sio watu wa kujichanganya na jamii. Hivyo watu hawa hukosa marafiki/wachumba au wenza kutoka katika jamii inayowazunguka badala yake ni rahisi kwake kupata marafiki wa kubadilishana nao mawazo akiwa ndani kwake.
d)Udomo zege
Kuna watu hutafuta wachumba na wenza mitandaoni kwa kuwa hawana ujasiri wa kumfuata mtu na kumtongoza/kumwambia kuwa anampenda ana kwa ana. Hivyo kupitia mtandao ni mambo yanakuwa rahisi zaidi. Hii pia imerahisisha sana kwa wanawake kupata wachumba/wenza pale anapokuwa anahitaji.
FAIDA
Kuna faida nyingi sana za kutafuta marafiki/wachumba/wenza mitandaoni. Hizi ni baadhi tu ya faida hizo:-
i)Kupata watu wangi kwa wakati mmoja.
Mtandaoni ni sehemu pekee unayoweza kupata marafiki au wachumba wengi kwa wakati mmoja. Hivyo ni rahisi sana kuchekecha na kupata marafiki au mchumba um/watakao.
ii)Kupata marafiki/wachumba /mwenza kutoka sehemu yoyote ile duniani.
Mitandao inatoa wigo mpana wa kupata marafiki kutoka sehemu mbalimbali na wenye hadhi mbalimbali kuliko hao wanaokuzunguka. Nakiri kuwa kupitia mitandao nimepata marafiki ambao katika mazingira yanayonizunguka kamwe nisingewaza kukutana nao. Mara nyingi rafiki zangu ninaoishi nao, huniuliza nimefahamiana vipi na hao marafiki kwani mazingira yao na yangu na hadhi zao hazituruhusu kukutana kirahisi.
iii)Kupata mawazo mapya.
Wakati mwingine marafiki wanaotuzunguka, wanakuwa na mawazo sawa na yetu. Hivyo marafiki kutoka mitandaoni huwa na mawazo mapya na pengine yenye kutoa changamoto. Kwa sisi wajasiriamali tunajua umuhimu wa kuwa na wazo jipya kila iitwapo leo.
CHANGAMOTO
Penye faida hapakosi changamoto.Baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika utafutaji wa marafiki/wachumba /wenza mitandaoni ni pamoja na:-
1.Uongo
Watu hudanganya sana mitandaoni,hudanganya umri,kazi wanazofanya,hali zao kimahusiano (marital status),urefu, uzito n.k. Wengine hutuma hata picha zisizo zao. Hivyo unapotafuta kuwa makini sana.
2.Utapeli na wizi
Kuna watu hutumia sana mianya hiyo kutapeli na kuibia watu mali zao. Hii imenikuta mara mbili. Nilitapeliwa na watu niliokutana nao mitandaoni.
3.Kupoteza muda
Wakati mwingine huu utafutaji hupelekea kupoteza muda mwingi kuwasiliana na watu. Hii ni kutokana na kuwa na watu wengi mno wa kuwasiliana nao.
Hizo ni baadhi tu ya sababu,faida na changamoto za utafutaji wa marafiki/wachumba/wenza mitandaoni. Karibuni muongezee nyingine.....