Unapomuonea wivu mwanandoa wa mwenzako !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Unapomuonea wivu mwanandoa wa mwenzako !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Ni jana tu hiki kituko kimetokea

Nakiita kituko kwa kuwa hakijaleta maana kwangu

Hapa sitajadili u-hovyo wa wivu wenyewe kwa kuwa ni mada ngumu kueleweka kwa wengi

Dada huyu ambae ndo kamuonea wivu mume wa rafikie,alikuwa na mahusiano naye kwa muda wa mwaka mpaka pale kadhia hii ilipotokea

Kadhia yenyewe ni kuwa,dada huyu alipigwa chini na mume wa shogaake ambae walikuwa wanamahusiano ya siri kitendo kilichofanya mwenye mume asijue kwa muda wote huo wa mwaka mmoja

Timbwili lilikuja kusanuka baada ya huyo mume wa shoga yake kuanzisha mahusiano na rafiki yao mwingine kitendo kilichomfanya ashindwe kuvumilia na kwenda kumweleza shoga ake aache kutembea na mume wa mtu,lakini baada ya kutokusikilizwa ilibidi amfate shoga yake[mwenye mume] na kumweleza kuwa shoga yao anamahusiano na mumewe
mwenye mume hakukurupuka na alimwambia atafanya uchunguzi kwanza

Tatizo lilikuja pale yule dada ambae alikuwa ni hawara wa kwanza wa huyo mume wa shoga yao kuona siku zinaenda na shoga ake [mke wa jamaa]] hachukui hatua haraka kukomesha mahusiano hayo,aliamua kwenda kumtisha jamaa kuwa kama hataachana na shoga yake atamwambia mkewe,jamaa akamwambia kuwa hata akienda kumwambia mkewe hatamuamini kwani anamjua mkewe sio mtu wa kukurupuka na atahakikisha mkewe hagundui

Kuona hivo huyu hawara wa zamani alikwenda kuleta vurugu nyumbani kwa shoga yake ambae ni hawara mpya wa jamaa,kama mnavyojua uswazi,baada ya muda mfupi watu walijaa na kuwakuta wamevurugana vibaya sana,uongozi wa mtaa ulipofika eneo la tukio na kutuliza ugomvi ilibidi waanze kuhojiwa kisa cha ugomvi ndipo .muanzisha fujo[hawara wa zamani] alipoeleza kila kitu na alipoulizwa kisa cha kupigania mume wa mtu hakua na jibu la moja kwa moja,alipobanwa ilibidi aeleze ukweli juu ya mahusiano yake na mume huyo wa shoga yao na akadai eti alikua anaona wivu kwa shoga yake kula vinono alivyokuwa anapewa yeye na mume huyo wa shoga yake

Pia akadai eti anampenda sana huyo mume wa shoga yake!!!!!!!

Khaaaaaaaaa!!!!!!!!!

Hapo ndipo nilipostaajabu sana wakati huo nikipewa story hii na jirani ambae mmoja kati ya wahusika wa ugomvi ule ni girlfriend wake

Ndipo aliponiuliza kulikoni mtu amuonee wivu mume wamtu,

Kwakeli sikuwa na jibu na mpaka sasa sina jibu zaidi ya kumuona huyu mwanamke wa ajabu sana

Hii inawezekanaje???????????????????????????????
 
Wanasema muovu akiokoka anakuwa ana upako mkali kuliko hata mlokole wa siku zote!
 
Kuna maana sana ya watu wa kale kusema watu waoane wakiwa bikra, hii mara ushakuwa wa Hasani na Ema, unatalikiwa na Athumani ndio unakuja kutulia na Brayani? Tabu tupu, katika hizo experience zote kuna sehemu moyo unaweza kuwa umeuacha huko.

Afu ndio unamkuta naye kaoa? CHochote chaweza kutokea, ndio unawaacha watu midomo wazi, ilikuwaje?

Your brain is very smart.....
 
Jamaa atakuwa mtoaji mzuri wa matunzo na inawezekana mkewe kukicha ni story za mumewe kwa mashoga zake..leo nimeletewa hiki wkend ntapelekwa wapi sijui!!!!!

Else mkewe ni mjeuri na kiburi na anawasimulia wenzake on how stiff she is sasa wao wanacheza na gap as wanajua jamaa anakosa nini ndani!!!
 
Aisee! Chezeya mume ya mtu! Wivu lazima awe nao sababu amekosa vinono alivyokuwa anapewa!
 
Kuna maana sana ya watu wa kale kusema watu waoane wakiwa bikra, hii mara ushakuwa wa Hasani na Ema, unatalikiwa na Athumani ndio unakuja kutulia na Brayani? Tabu tupu, katika hizo experience zote kuna sehemu moyo unaweza kuwa umeuacha huko.

Afu ndio unamkuta naye kaoa? CHochote chaweza kutokea, ndio unawaacha watu midomo wazi, ilikuwaje?

Wallah!!!

Hii bhange ya leo imekukubali

Khaaaaaa!!!!!!

Mtoto wa kike unatiririka utadhani una PhD!!!!!!!!!!!lol!
 
Aisee! Chezeya mume ya mtu! Wivu lazima awe nao sababu amekosa vinono alivyokuwa anapewa!

Yaani vinono vinakufanya umuonee wivu muke ya mutu kweli???????????????

I cant believe!!!
 
cheating @ work, kazi ipo na haya mahusiano yetu!
 
Kwamba huyo shosti wa awali baada ya "kuachia tonge" akageuka kuwa mlinzi wa ndoa ya mwenzie kwa uchungu wote bila kujali motives behind....

Yeye alidhani analinda chake kumbe analinda cha mwenzake!!!!

Kazi kweli kweli!!!!!
 
Yaani vinono vinakufanya umuonee wivu muke ya mutu kweli???????????????

I cant believe!!!

we fikiria mtu alikuwa akohoi! Akihoa kidogo 'beby jioni usipike ntakupitia twende dodoma hotel kwa dina', umesema unashida na sh ngap? Ok dear hii laki 5 inakutosha? Teh kwanini asilianzishe ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom