Uzi wa kwanza jf naupinga kwa 110% kuna baadhi ya mambo yakijulikana kabla ya ndoa haki ya nan hupat mke/mme na yakijulikana baada ya ndoa hayana effect maisha yatasonga kama kawa. Mfano mimi nina dada yangu ameolewa na mchaga mbahili kinyama, unajua ubahili? Yan ni katika kiwango cha standarg gauge. Dada yangu mdogo akaapa na nyumban wakamsapot kama hatokuja kuolewa na mchaga labda achanganyikiwe hayo maneno akawa anamwambia kila mwanaume aliekua anamfuata fuata, katika pita pita akapata bf wa kichaga ila jamaa hakua mbahili ila kwa msimamo wa sista na nyumbani yule jamaa hata mlangon kwa wakwe asingekanyaga, ikabidi awe msiri kwanza, Tulikuja kujua baada ya yeye na wazaz wake kuja kutuambia na jamaa sio mbahili hata chembe. Ndo mana mda mwingne nasema haya masuala ya kumbatiza mtu tabia kutokana na kabila lake ndo maana halisi ya uchawi. Haya niambie angeweka mambo yote wazi ungemuoa wewe broo, au shda yako tukose mahali? Ngoja niishie hapo natumia nokia ya batan nisije nikatoka sugu ya vidole bure.