Unapataje hesabu ya kumlipa fundi tiles?

mugulinde

Member
Jun 7, 2018
52
107
Amani iwe kwenu wanaukumbi.

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mambo mengi anayotujalia katika maisha yetu ya kila siku. Niende kwenye mada moja kwa moja, mwenye ijuzi wa mambo ya ujenzi kwenye kupiga tiles anifafanulie nawezaje kupata hesabu ya gharama ya fundi tiles.

Maeneo yatakayo pigwa tiles ni kama ifuatavyo:. Seating room yenye ukubwa wa sqm 30 Dining sqm 16 Veranda la nje na ngazi zake kushuka chini Sqm 16 room 2 sqm 18

Natanguliza shukrani.
 
Ndio uelewe kuwa ujenzi ni gharama! Ukiskia mtu anaringa na nyumba yake mjini uelewe kuwa sio mchezo
Sahihi kabisa kiongozi, material yamepanda sana nimeshindwa kuweka tiles maeneo kadhaa mfano, jikoni, chooni, master na veranda la kutokea jikoni pamoja na ngazi zake za kushuka ni kama kighorofa flani hivi.

Sent from my Redmi Note 3 using JamiiForums mobile app
 
Yani inakubidi ukaze taft hata 10M ukilianzisha unapiga full gwamba! Finishing ndio utamu wa nyumba yenyewe 😀
 
Wakati nafanya hizi ishu za saidia fundi ilikua tunachaji kwa square meter. Sijui kama bado ni hivyo ila ilikua square meter inaanzia elfu 5.

Hapo sasa zitakuja factors kama kazi ni kubwa sana. Hadhi ya anayetaka kujengewa. Na kama tumewahi kufanya kazi kabla.
 
Chukua jumla ya Sqm za nyumba yako halafu zidisha kwa 5000 au 6000..
Dah! Mungu awabariki sana kwa elimu hii, ndugu zangu, fundi aliniambia eti kila sqm.1 elfu 10,000 nikaona huyu hajielewi, nikamwambia ngoja nikalale kesho kukicha tutaongea.
 
Wakati nafanya hizi ishu za saidia fundi ilikua tunachaji kwa square meter. Sijui kama bado ni hivyo ila ilikua square meter inaanzia elfu 5.

Hapo sasa zitakuja factors kama kazi ni kubwa sana. Hadhi ya anayetaka kujengewa. Na kama tumewahi kufanya kazi kabla.
Castr; uko sahihi, huyu fundi wangu nilianza naye na anakaa site, alipiga plaster moja tamu Sana, tiles akizingua anakosa kazi, alitaka kunipiga, sema bado aliniambia tunaweza kushuka kidogo ila daah!!
 
Finishing ni tamu kweli kweli, ila inatumbua pesa balaa, kupiga plaster, blandering ya kisasa na decoration zake kwenye ukuta wa tv, decoration za nje kwenye kona zote za nyumba na nguzo zake pamoja na Kufunga mkanda/kiuno na schemming Kwa ndani imetafuna 16m
 
Mimi ngumbalu kabisa nisiyejua hesabu.. napimaje Sqm.. hebu mnirahisishie
Sqm, ni sawa na kusema 1 Sqm ambayo ni urefu unakua na meter 1 na upana meter 1, kwa kawaida meter moja ni sawa na urefu wa sentimita 100, yaani rula tatu zile za shuleni uongeze sentimita 10, ndio mita moja.

Kwaiyo Sqm, inakua ni box lenye urefu 1 meter na upana 1 meter.

Sijui umenipata, vipimo vya mtaani meter moja ni inalekeana na hatua kubwa ya mtu mzima.
 
Tiles ni 20,000/- mpaka 40,000/_ per sqm.
Milioni 1.5 mpaka milioni 3.2. inategemea unavyotaka.
Hiyo ni standard, ukitaka urembo inaweza ikawa zaidi. Kwa hiyo hapo aliposema kila kitu ni milioni 3 yupo sawa.
kuna cement na vigaragazo vinigne.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom