Elections 2010 Unamuunga mkono Dr. Slaa kugombea URAIS mwaka 2010? Jiandikishe hapa


Mkuu, hili halikuniuma kabisa. Mie pia napenda sana mizaha ila tofautisha nyakati. Hii kitu si MZAHA kabisa na tumepania. Itakuwa vema kama na wewe mtani wangu Mzenji ukajiunga kama unaona jamaa anatufaa. Tusipopigania mabadiliko wenyewe mnafikiri nani atafanya? Kumbuka hata Nuhu alipoanza kujenga Mashua yake, watu walimcheka, ila gharika ilipofika....... Kutokana na hali ilivyo kwa sasa, hakuna kipindi kizuri kama hiki kuwashughulikia viongozi wetu na tukimaliza basi turudi kwenye kuushughulikia Muungano wetu.

Hongera Dr. kwa kugundua mapema mpango wa sisiem lakini waache waendelee wewe endelea na mipango yako.

50Cent anasema ..... "GET RICH (DR SLAA) or DIE TRYIN"
 

Kilembwe, bila samahani. Kuna thread ya huo ugomvi wa Sendeka na RC. tayari. Itafute na uulize swali lako huko. Hapa ni kujiandikisha tu kwenye listi. Vipi wewe pia hutuungi mkono?
 
Kama Dr. Slaa agombee urais wa JF mimi naona anafaa sana...nchi si lelemama nyie...Obama keshaota mvi tele kwa stress.

Ni kweli nchi si lele mama lakina Dr Slaa is much better than JK na wengi watakaojitokeza sisi em. Kama ni mvi tayari anazo na ukiota mvi kwa ajili ya taifa lako huna cha kujutia.
 
Ingependeza Kama Dr Slaa na Chadema vingewin Urais mwaka huu. Lakini sioni Mkakati.
 
Ingependeza Kama Dr Slaa na Chadema vingewin Urais mwaka huu. Lakini sioni Mkakati.

Ndiyo mkakati wenyewe huu. Kikwete hataki kura za WAFANYAKAZI sasa kama kuna muda wa mtu kugombea kumuondoa Rais wa CCM ni huu. Pia inaweza kutokea Kikwete akasusa kugombea na Dr. Slaa hajajiandaa, hapo tutajuta kwa kutokujiandaa. Sasa Mkuu, uko na sisi kwenye listi? Tunakaribia 50 sasa kwa siku moja tu.
 
Mnisamehe kama nitaonekana niko tpfauti, simshauri agombee urais, maana ``c.c.m`` mbinu zao ni kali sana, sio lahisi kuwaondoa, hivyo basi nashauri agombee ubunge ili aendelee kuibua uozo na ufisadi unaofanywa nchini.
 
Kaitaba,
Kuna jamaa alimwambia maneno kama hayo Obama, na Obama hakurudi kwa jamaa tena kuchukua ushauri. Hapa hatupo kurudi nyuma.
Yeye Dr Slaa na akili zake achanganye na za kwetu. Ila tukiwa wengi, kuna uwezekano tukazizidi za kwake na akaamuwa kugombea. Njooni kwa wingi ili afahamu watu kiasi gani wanamuhitaji. Kama ubunge kashafanya sana kwa mafanikio makubwa. Muda umefika aongeze hatua moja mbele
 
Mkuu wangu Sikonge tatizo si kujiandikisha tu haichukui hata sekunde kumi kuandika jina lazima ufikirie kwanza kwanini unajiandikisha, ikiwezekana na sababu kama wengine wanavyofanya, ujue hata kutojiandikisha na kutoa sababu inakupatia wewe uliyeleta hii poll uelewa zaidi kuliko kutegemea one sided ambayo inaweza isikupe picha halisi, but all in all we are sailing in the same boat but different floors.
 
Luteni,

Kuna wengi sana walimwambia Obama asigombee. Angeliwasikiliza basi angeliula wa chuya. Ilipotokea kuwa USA kuna matatizo ya Uchumi, Wazungu wenyewe wakaanza kuangalia ni nani ana akili kuweza kusafisha hii hali na si nani ataweza kwenda kurusha mabomu Uarabuni.
Inawezekana sisi hatuko sawa, ila wewe unapendekeza nini? Si uanzishe thread yako na sisi tuje tuone mawazo yako yakoje? Au ndiyo unaleta ya John Mashaka na Dr. Shayo sijui? Shayo yeye ni kuja kukashfu tu maoni ya John Mashaka, ila yeye hata siku moja haanzishi yake. Huo ni uvivu wa kufikiri. Unachokiogopa hasa ninini? At the end of the day WE HAVE NOTHING TO LOOSE.

NYONGEZA: Mbona Kikwete anajulikana kuwa atagombea? Inamaana akitangaza atakuwa kapoteza mvuto? Kampeni inabidi zianze mapema. USA huwa wanaanza mapema na hakiharibiki kitu.
 
Shalom

Maneno yako yana uzito fulani, najua huwa tupo pamoja wakati mwingi katika mipango ya Chadema, uzuri wangu sijui ndiyo ubaya kwa wengine huwa sijui kujificha, umesema tunawapa signal sisiem, unajua hata kumfanya mpinzani wako ajue kuwa unajua mbinu zake nayo ni mbinu tosha ataanza kubabaika kama wanavyofanya sasa wameshindwa kubashiri ni nani atasimama kwa tiketi ya Chadema wengi wanahisi SAS, Six, Slaa nk tuwaache wawe kwenye suspense hadi siku ya siku, binafsi nafikiri ni mbinu nzuri tusubiri siku atakapotangazwa ataleta mshindo, wewe chukulia mfano wa wagombea wa CUF kila mtu anawajua siku akitangazwa hawatakuwa na impact/mvuto wowote kwa walengwa. Shalom
 
46. Pasco
 

...Mbu na wanawe wote!
 
Sikonge quote me right am not against the move am pro Slaa and Chadema for so long time and nobody can change me about it and I think most of the members know that na sisemi kuwa akiteuliwa kugombea sitampigia kampeni ila ninachosema let him be free to decide, kama ulivyosema hata tukijiandikisha elfu kumi leo, kesho akakataa we have nothing to lose but why begin losing today. Ndiyo najua kwamba most of politicians sometimes NO means YES and vice versa yeye mwenyewe Dr. kasema NO sasa sijui tuilazimishe iwe YES, ofcourse am confused help me.

Kuhusu suala la kuanzisha thread yangu ili uje kutoa maoni nafikiri hapo Sikonge umepotoka kidogo you didnt mean it, nini tofauti ya wewe kuanzisha thread hii na mimi kuja kutoa maoni and vice versa, au una maana mimi nianzishe ili wewe uje kutoa maoni wakati huohuo wewe ukianzisha mimi nisijekutoa maoni anyway tuyaache hayo hayatatusaidia tu focus kwenye mada yenyewe lengo langu kuu ni Chadema ishinde si mtu mmoja ashinde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…