Elections 2010 Unamuunga mkono Dr. Slaa kugombea URAIS mwaka 2010? Jiandikishe hapa

ndiyo na tuhakikishe hawaibi kura,hivi chama chenye wanachama 4m ukilitoa kundi la lowasa na rostam ambao tunajua kabisa hawatampa kura unabaki na watu 1m tutamshindwa huyu mkwere anaetukana watu kwa ofisi isiyozalisha mali anawatukana wazalishaji? hebut twende mbele ikibidi tu petition mahakamani hatuwezi kuwa na uchaguzi wa urais wa JK Kikwete vs Mtikila halafu kikwete atakwambia kashinda kwa kishindo
 
[
QUOTE=Sikonge;900806] Siyo lazima uchangie kila kitu. Nilivyoona unajadili swala la Muungano nikafikiri una upeo mkubwa sana ila ghafla yakaanza ya Karume alikuwa hajui kusoma, hajui Kiingereza (Mmalawi na baharia huyoo hajui Kiingereza) na maswala mengine, nimeanza kukufahamu kwa ukaribu. Endelea kujifunua. Ila jambo moja tu ni kuwa kama Wanaotaka UHURU wa Zanzibar watu wenyewe ndiyo kama nyie, basi kweli naweza kukubaliana na Nyerere kuwa "nyie watu jamjakomaa kujitawala". Hebu onyesheni kukua basi kidogo hata kwenye majadiliano ya kawaida kabisa.
Kama ulikuwa na shida ya kujadili mada ya muungano ungekuja kule, unchokionyesha hapa ni kuwa ukweli umekuchukuza, siwezi kukusaidia. Aliyesema kuwa Karume hajuwi kingereza si mimi ni Prof. Shivji, ambaye silingani naye hasa na masula ya wapi Karume alitokea yalizuka ndani ya mjadala wenyewe na sikuyaleta mimi, nakushangaa unamsemea Dr. Slaa hapa JF wakati yeye ni memba, na ameshasema kuwa hana mpango wa kugombea urais, wanaompakazia ni CCM wanaotaka kuwachanganya wapiga kura wake. Labda wewe na hao wenzako hapo juu unaowaorodhesha ndiyo hao CCM wenyewe aliowasema Dr. Slaa. Mimi nimeleta mzaha tu kwa kuwa hii thread imekaa kimzaha mzaha, provided, kuwa msimamo wa Dr. Slaa unajuulikana na hakuna anayeshughulika tena.
Nafikiri huu mjadala wako unafanana na majadiliano hayo uliyoweka kwenye hiyo picha.
 
Mimi nimeleta mzaha tu kwa kuwa hii thread imekaa kimzaha mzaha,

Duh, watu wengine bwana - ni mizaha kama hii iliyomweka JK madarakani. Kumpa Kikwete miaka mitano kulikuwa ni mzaha wa mwaka lakini kumwongeza Jakaya miaka mingine mitano kutakuwa ndio mzaha wa karne. Hata hivyo ndivyo Watanzania wengi walivyo - watu wa mzaha mzaha !

Na mimi Mag3 niongezeni kwenye listi ya wanaomtaka Dr. Slaa agombee - Dr. Slaa tosha ! Kugombea Ubunge ni wazo zuri lakini kugombea Uraisi ni jambo zuri zaidi na Wahenga walisema good is never enough where better is possible.

Baada ya kujiandikisha what next?

Tutatuma petition kwa Dr. Slaa afikirie upya uamuzi wake wa kutogombea. Ninachojua na nilicho na hakika nacho ni kuwa jina Mag3 linawakilisha watu si haba.
 
Mkuu Sikonge

tafadhali ongeza jina langu Tai Ngwilizi kwenye list

ni muhimu kwa Dr. Slaa kugombea mwaka huu, uwezekano wa kushindwa hasa vijijini upo ndio,lakini watu wengi watakuwa wamefunguliwa macho. itakuwa nguvu ya kutosha kuwafanya wananchi wa vijijini waamke na kuiangalia CCM na Kikwete kwa mtazamo tofauti jambo ambalo litaupa nguvu upinzani.Slaa kusubiri hadi 2015 inaweza kuwa sio suluhisho kwa sababu inawapa CCM miaka mitano ambayo wanaweza kutumia kumwangusha kisiasa. Sasa ndio wakati wa kutumia kilicho mkononi kuipinga CCM

na kama Slaa akishinda...kwa nini asiweze kuwa rais? Kama Kikwete, washauri wake, wasaidizi wake, mawaziri wake na wabunge wake wameweza kuwa madarakani basi hata Slaa anaweza!
 
Hongera Dr. kwa kugundua mapema mpango wa sisiem lakini waache waendelee wewe endelea na mipango yako.
 
Mtu akifanya vizuri katika kazi yake hupandishwa cheo. Ni ukweli usiopingika kuwa, huwezi kumwacha mtu huyo na kumpandisha cheo mtu mwingine asiyefanya vizuri kama hakuna sababu za chuki. Kama Dr Slaa amefanya vizuri kwenye uongozi wa chama chake na ubunge, sasa anahitaji kupandishwa cheo. Manufaa ya utendaji mzuri yaliyofurahiwa na watu wa jimbo lake sasa yaweze kufurahiwa na taifa zima 100%.

Woga sio mzuri. Kusitasita au kuwa na mashaka si vizuri. Tujipe moyo na tumpe moyo Dr Slaa kwamba tupo nyuma yake kupigania ukombozi wa taifa letu. Inawezekana Kikwete akawa ndiye raisi wa kwanza kutawala awamu moja Tanzania na vilevile anaweza kuwa ni raisi wa mwisho kutoka ccm kutawla Tanzania. Hata hivyo inawezekana mwaka pekee wa mapinduzi ukawa ni 2010 na tukiacha kuongoza mapambano ya ukombozi mwaka huu, CCM atajiimarisha zaidi na haitawezekana tena kumwondoa.

Uwezo wa kumwondoa katika uongozi upo, sababu zipo, sasa tunahitaji nia ya watu kuunga mkono hoja ili Dr Slaa atiwe moyo wa kuongoza mapambano ya ukombozi wa nchi kutoka katika mikono dhalimu na fisadi inayonyonya damu ya watu wake. Tusiogope ..ndege mjanja hunaswa na tundu bovu, CCM sasa wamenaswa na tundu bovu, wanaanza kuwehuka na kutapatapa. Kilichobaki ni kwenda kumshika yule ndege aliyenasa, kumkaanga kwa mafuta yake na kumla.

Tusiogope tuwe imara tukapiganie nchi yetu. Tuwe na moyo mkuu ....
Count sn2139
 
Hongera Dr. kwa kugundua mapema mpango wa sisiem lakini waache waendelee wewe endelea na mipango yako.

LUteni,

Leo umenisikitisha sana kwa michango yako, Kwanza kama Dr amejua mipango ya CCM na wewe unamsupport hutakiwi kusema hadharani kwani unapeleka signal kwa hao wanaomtega kuwa amegundua. Pili wewe unaonekana mambo haya ni mageni kabisa, ili mtu agombee uraisi ina bidi yeye mwenyewe akubari na aingie kwenye nomination.

Alichofanya sikonge hapa ni kumwonesha Dr slaa kuwa kama atafikiria kugombea basi ajue kuwa kuna watu wengi wanamsupport na siyo kwamba wanamlazimishaagombee. sasa unaanza kutoa siri kama unazijua kweli au kuropoka kuhusu mambo ya Chadema!. Unaweza ku google na kuona vitu vingi vya aina hii vikifanyika duniani. Hata huyo socialist wako uliyemweka kwenye avatar yaka kama siyo wakina Harry Reid kumwambia kuwa wanamsupport pengine asingetia mguu kwenye kinyanganyiro.

Muda mweingiene sio lazima kutoa siri za chama ili uonekane kuwa ni mtu wandani.

Slaa anaweza kuvuna wagombea 100 kama akisimama kwenye urais au akaenda bungeni na wagombea wengine 15 akiamua kugombea
 
Hizi ni kampeni zisizo na kichwa wala miguu, mtu mwenyewe hataki, halafu tunapoteza muda kijiandikisha majina, then tunajiita greater thinker, how?
 
Hizi ni kampeni zisizo na kichwa wala miguu, mtu mwenyewe hataki, halafu tunapoteza muda kijiandikisha majina, then tunajiita greater thinker, how?
Ulitakiwa ujuandikishe jina lako tu na au ujiondoe kimya kimya kwenye thread. Huoni umepoteza muda zaidi kwenye kuandika maneno hayo zaidi ya jina tu? Wiki lijalo, hao watakaokuwa wamejiandikisha, ntawaomba Mods wamtumie RASMI kwenye email yake ingawa nafahamu kuwa na yeye yuko hapahapa. Ungelisoma juu Mag3 na Shalom walivyochangia, ndiyo ungelielewa maana ya hii kitu. Kuna siku moja Mungu atakujalia na wewe uelewe.
 
Wanajamvi samahani naomba nitoke kidogo kwenye mada hii, mimi nauliza tu kuna uhalali gani kwa mkuu wa mkoa kumfukuza mbunge mkutanoni na kumtishia kumuweka rumande? maana jana nimeona kwenye taarifa ya habari ya TBC1 Shekiffu (Mkuu wa mkoa wa Manyara), akimtisha na kumfukuza kwenye mkutano mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka!
 
Back
Top Bottom