Unamlindaje mwanao na mtandao

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mwaka jana kwenye wiki ya TEKNOHAMA neno kuu lililotumika ni MKINGE MTOTO NA MITANDAO ,mambo mengi sana yalijadiliwa kwenye wiki hiyo ya TEKNOHAMA huu ni mwaka mpya sasa nimejaribu kuangalia kuona jinsi wazazi wanavyozingatia hili la kukinga watoto wao na mitandao .

Wengi ninaowaona kuongea nao au kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na Mitandao wamewekeza sana katika vitu kama programu za kurekodi kila kitu ambacho motto wake anachofanya kwenye mtandao kwa wakati Fulani yaani kuhifadhi taarifa zote .

Wengine ni kuweka muda maalumu wa kutumia kompyuta kuingilia kwenye mtandao huku yeye mzazi akiwa pembeni kuona mtoto wake anachofanya ili kujaribu kumfundisha haya na yale .

Kundi lingine ni lile linalokataza watoto wao kutumia kitu kinachoitwa kompyuta kabisa majumbani mwao mpaka watoto wao wafikie umri Fulani lakini hawa watoto inawezekana wakatumia kompyuta hizo mashuleni mwao au kwa rafiki zao au mitaani tu .

Na la mwisho ni hili ambalo limeamua kununua michezo ya kompyuta kwa ajili ya watoto wao watumie muda mwingi katika kucheza michezo hiyo kwenye kompyuta zao .

Kwenye makundi yote hayo pia inategemeana na hali ya kiuchumi ya mzazi husika sio hilo tu na hata watoto hao wako kwenye mazingira gani ili kuweza kupata nafasi ya kutumia vifaa hivyo au hata kuviona vikifanya kazi naamini wengi watakuwa ni wale wa maisha ya kati na juu .

Juzi nilikutana tena na mmoja wa wazazi hawa yeye amempa mtoto wake wa miaka 16 kila kitu kuanzia kompyuta iliyounganishwa kwenye mtandao muda wote simu na vifaa vingine kwa ajili ya matumizi yake .

Mzazi alianza kuona mtoto wake mambo yanabadilika kidogo akaamua kumwomba password yake ya anuani ya barua pepe ili aweze kuona kile anachoandikiana na wenzake ,mtoto kuona hivyo akawa anafuta kila anaposoma .

Yule mzazi akaamua kuforwad barua pepe zote zinazoingia kwenye anuani ya mtoto wake kwenda kwenye anuani yake bila mtoto Yule kujua pia kujiunganisha kwenye simu yake ya mkono ili aweze kusikiliza mazungumzo pindi mtoto wake anapoongea kwenye simu .

Nilijaribu kuangalia kwa mfano watu alio nao kwenye mtandao wa facebook niligundua majina kama 3 hivi lakini moja ndio nilikuwa nalijua ni la mtu wa miaka zaidi ya 45 aliyekuwa anajaribu kupata mawasiliano ya mtoto wa miaka 18 kwa kumbembeleza
…..
Suala la kumkinga mwanao na matishio mbalimbali ya mtandao ni zaidi ya kuhifadhi mazungumzo anayoyafanya kutumia kompyuta na vifaa vingine vya mawasiliano kama ukirekodi ya nyumbani anaweza kutumia yashuleni kwao kwa raha zake kwa mfano au anaweza kwenda kwa jirani au anaweza kwenda kwenye mgahawa wa mtando na kufanya shuguli zake .

Je wewe kama mzazi unafanya nini kumdhibiti mtoto wako na matumizi ya kompyuta haswa anapotembelea mitandao mbalimbali duniani ? kama hatembelei akiwa nyumbani kwako anatembelea shuleni tu je unajua sera ya TEKNOHAMA ya shule anayosoma mtoto wako umewahi kuisoma na kukubaliana na kitu kilichoandikwa humo .

Niliwahi kutembelea shule moja mjini arusha ( Arusha Modern ) Hii shule haina Sera ya TEKNOHAMA kwenye chumba chao cha kompyuta wanafunzi wanaweza kufanya chochote wanachotaka kwenye kompyuta hizo kuanzia kutembelea mitandao mbalimbali , kushusha vitu na kuwasiliana na wenzao popote walipo huu ni mfano halisi wa mambo yanayoendelea nyuma ya pazia , kwahiyo kama mzazi ni muhimu kujua sera ya Teknohama ya shule anayosoma mtoto wako uchukuwe uisome na kuweka sahihi kukubaliana na kile kilichomo ndani .

Kuhusu kutumia program za kuhifadhi kila anachofanya mtoto wako kwenye kompyuta na mitandao hii kwangu sioni kama ni njia bora unaweza kumfanya mtoto wako awe muaga asiwe huru kufanya anachotaka yeye na ni ngumu sana kwa yeye kujifunza baadhi ya vitu kama akitambua anafuatiliwa kuheshimu uhuru na masuala binafsi ya mtoto wako ni muhimu sana lakini pia angalia na umri wa mtoto wako kabla hujaamua kumhusisha sana na masuala au matumizi ya kompyuta .

Siku hizi kuna mitandao jamii kama facebook , tagged, hi5 na mengine mingi tu kama umeweka programu za kuzima au kufunga mitandao michafu mtoto wako asiangalie basi anaweza kuingia kwenye mitandao jamii kama facebook na hi5 akakutana na wahalifu humo ndani wakawasiliana na kubadilishana habari zingine mwisho wa siku mtoto anaweza kuumizwa .

Ni muhimu sana kuangalia wale watu ambao mtoto wako anawasiliana nao kwenye facebook na mitandao mengine ya jamii ambayo imezagaa duniani ,kujua wale anaowasiliana nao kwa njia ya barua pepe na wengine wengi na kama kuna chochote unapenda kumfundisha mtoto wako au kumkataza uanzie na hapo lakini angalia usiingilie uhuru wake wa kuwasiliana wala kuvunja haki zake zingine .

Hili ni jukumu la Wazazi na walezi huko majumbani kwa kushirikiana na walimu mashuleni ,wahudumu wa migahawa ya mtandao pamoja na wadau wengine kutengeneza njia mbalimbali zinazoweza kusaidia pande mbalimbali kwenye suala hili

Haya ni mawazo yangu tu wewe kama mzazi na walimu mashuleni muna mengi zaidi .
 
shy unaandika mada za maana sana, zenye fikra endelevu katika maswala ya tekno kwa ujumla. lakini wenzangu mbona michango ya mawazo patupu? mathalan hili swala la kulinda watoto wasiathirike na yanayopatikana kwenye wavuti (internet).

kwa sisi wana JF kukaa kwetu kimya ina maana athari hizi hazituhusu? au ni kwasababu tuna uelewa mdogo? au hatuna interest? sote kwa njia moja au nyingine tuna uhusiano na watoto, lakini inashangaza kuona mada nzuri kama hii inakosa michango ya wana JF, siwalaumu ni hoja tu.
 
Back
Top Bottom