Unamkumbuka Dk. Leakey Abdallah?

Chagua mmoja anayeweza kuelezea mpira Kati ya hawa
Tigana Lukinja
Eddo Kumwembe
Dokta Leakey
George Ambangile
Mbwaduke
MAYAI Tembele
Ally Kamwe
Wilson Oruma
Kashushu
 
Chagua mmoja anayeweza kuelezea mpira Kati ya hawa
Tigana Lukinja
Eddo Kumwembe
Dokta Leakey
George Ambangile
Mbwaduke
MAYAI Tembele
Ally Kamwe
Wilson Oruma
Kashushu
Kwa bahati mbaya umemruka Amri Kiemba..... huyu mwamba ukiondoa kupenda kucheka anaujua mpira in and out na anajua kuuelezea kwa jicho la mchezaji, jicho la ukocha na jicho la kichambuzi na jicho la ushabiki

Katika hao ulio wataja ntakwenda na Tigana Lukinja kisha Tembele

Edo ni mzuri sana na hana mpinzani kwenye kuandika malaka za kimichezo kuliko kuchambua live

Ambagile anajua sana kushawishi hoja zake na ana details nyingi za ku Google lakini zimejaa sana nadharia nyingi kama walivyo akina Hans, Goef rea, Farahn, Njenge

Kashasha sio mchambuzi mzuri ila ni mtamu sana kuelezea kitaalamu majina ya matukio na mipigo na formation wakati na baada ya mechi

Dr Leaky ni mtaalamu zaidi wa kuhadithia matukio na historia ya visa vya wachezaji makocha mashabiki viwanja, uhasama wa timu nk nk
 
Azam wamuajiri huyo jamaa, kichwa sana anachambua vema toka niko shule ya msingi
 
Huyu alikuwa DR kweli

anamambo mawili muhimu kwenye uchambuzi

(1)hakuna taifa asilolijua kwa mpira na mpira wenyewe (kuchambua

(2)Historia za kitawala kwenye mataifa hayo mawili yanayokuwa kwenye ratiba ya mtanange sikuhiyo

mfano ,sikuhiyo wacheze ureno na Angola au ureno na msumbiji au ureno na Hispania

Kama kesho yake unamtihani wa histori ,acha kufungua daftari nenda kaangalie mechi majibu yoye utapata kwake.....kwasasa Yuko wapi cjui
 
Mkuu wewe kweli unamjua vizuri sana DR Leaky

Ni mzuri mmno kuelezea matukio na historia za timu husika
 
Chagua mmoja anayeweza kuelezea mpira Kati ya hawa
Tigana Lukinja
Eddo Kumwembe
Dokta Leakey
George Ambangile
Mbwaduke
MAYAI Tembele
Ally Kamwe
Wilson Oruma
Kashushu
Wilson Oruma nae watu wanamuona ni mchambuzi? Duh
 
Mkuu wewe kweli unamjua vizuri sana DR Leaky

Ni mzuri mmno kuelezea matukio na historia za timu husika
namfahamu ndo muhindi pekee pia rafudhi ya kiswahili na English sanifu na anasikika huchoki msikiliza .......wengine Hawa wakizungumza unaona mbona kama puani kunakamasi na nyingine mdomoni ....
 
Dr Riki Abdallah bado anaendelea na biashara yake ya utalii ( kuwindisha).
Dr Riki ni mdogo wa Kapteni Aziz Abdallah Rubani maarufu wa zamani wa ATC.
Dr Riki Abdallah ni Mzaliwa wa wilaya ya Kibondo, kwenye jimbo la uchaguzi la Muhambwe, kijiji cha mpakani cha Mabamba.
Bado anaishi Dsm.
 
Dr Leaky ni mtaalamu zaidi wa kuhadithia matukio na historia ya visa vya wachezaji makocha mashabiki viwanja, uhasama wa timu nk nk
Mpira kwa sehemu kubwa ni kuandika Historia na kurudia Historia. Watunza stats ndio Hawa hawa watunza historia.. Je unaamini hayafahamu ya Tactical analysis ?
 
Mpira kwa sehemu kubwa ni kuandika Historia na kurudia Historia. Watunza stats ndio Hawa hawa watunza historia.. Je unaamini hayafahamu ya Tactical analysis ?
Mkuu mfano ikiwa inacheza Brazil Vs Argentina halafu wachambuzi wakawa ni Lukinja na Dr Leaky

Lukinja atatumia muda wake wote kuelezea game kwa angle ya ubora wa wachezaji, mifumo nk

Dr Leaky pamoja na kufanya analysis lakini atatumia muda mwingi kueleza visa na vituko vya uhasama wa nchi hizi mbili na drama zao na mambo mengi yanayo ihusu hiyo game nje na ndani ya uwanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…