Unamjua milionea mfuta viatu(shoeshine)

Unamjua milionea mfuta viatu(shoeshine)

MT255

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2012
Posts
3,728
Reaction score
4,999
Kijana muuza mayai milionea kwa kazi ya kufuta viatu vumbi Kwa brash,taulo ata mikono kiatu chako lazma kingaree ufikapo kwenye Airport za madiba mtu peke wakungarisha viatu vyako ni Mgaiya Kwa siku anabrash zaidi ya pair 350 Johanesburg 120 Durban 120 Capetown katika hizo airport tatu Mgaiya anawafanyakazi wake 45 na kwa sasa jamaa anaangalia njia zakupata patnership na airport za Usa n Uk.

Jamaa ni mfuta viatu anavaa smart viatu vizuri na aimuumizi kichwa coz anapenda kazi yake na kwa mwaka anaingiza si chini ya rand 2.5m $227,000= tsh 400,000,000 kwa Airport 3 kwakufuta watu viatu tu. Mgaiya akufika hapo kirahisi kabisa kapitia mengi na kafail mara nyingi hii hapa story yake Alianza kufanya kazi airport akiwa kaajiliwa kama mtu wakutoa boarding card za Saairways na baada ya miaka 5 pamoja na kupandishwa cheo cha usupervisor Mgaiya aliachana na kazi airpot na kujiunga na biashara ya familia.

Aliamua kujiingiza katika maswala ya usafirishaji ikiwa ni biashara ya familia na uncle baadae akamwambia aendele na maisha yake kazi yake akaichkua kaka yake wa upande wa mama jamaa akachkua mkopo lakini mambo hayakua poa kabisa vilishindikana akaludi mtaani na kuwa jobless.

Alipoondoka kwenye biashara ya familia alibaki na baadhi ya wateja so akaanza project mpyaa akaatafta wakulima wakawa wanampa mayai na akawa anauza na kupata faida ya $6=10,000 KILA box la mayai BT ilikua biashara ngumu wakulima wakawa wanamdai na akashindwa supply coz saa zingine ata hela ya mafuta ya kupeleka mayai aliku hanaa vikashindikana tena.

Pesa zilipoisha alikua na idea ila hana pesa so akajiingiza kwenye shindano la wajasiliamali la mchanganuo wa biashara na idea yake akawamshindi akashinda $3,100 ndani ya siku mbili. Akaichkua $3,100 anaingiza kwenye biashara ya kupanda miti na baada ya miezi 6 mambo yakawa yaleyale akaishiwa mpaka hela ya kula nikawa shida akarudi kitaa jobless.

Njaa ikamkamata kwelikweli maisha yakawa magumu sana akaamua kujitoa muhanga akaanza ushushine airpot mwaka huo akauza na gari lake ili kupata eneo na kupata mkataba wa biashara yake ilimchukua mwaka mpaka kukubaliwa 2002-2003 akaanza kazi na siku yake ya kwanza alikua ana vifaa so akauza friji lake kununua vifa brush,kiwi,polish na alianza kwakuwekewa viatu vya wateja magotini.


Alikua anaamka saa5:00 alfajiri kuwahi wateja airpot kuwafuta viatu na kurudi saa23:00 familia imelala akiteseka sana ila akiwa na way out baada ya wateja kuwa wengi wakata sehem ipewe jina zuri so jamaa akaita Lere shoeshine baada ya miezi mitano biashara ikanoga na ikachanganya balaa akawa na vijana watano.


Mafanikio aliyopata hapo Capetown akulizika akafungua pia Airport nyingine Jburg na Durban na kuajili vijana zaidi ya 60 now maisha mazuri anamiliki nyumba yake mwenyewe Capetown nzuri mtoto anasoma private school now anafanya shift MOJA TU ya masaa6 uhakika wa 400,000,000 kwa mwaka kwakupangusa TU viatu.


Anasema

“When starting a business in South Africa, you need self-belief,” is his top advice for young entrepreneurs. “All the conditions will never all be favorable at the same time. If you don’t start, you won’t go anywhere — you have to start.” Jamaa now anazichungulia Airport za Angola,Kenya na Nigeria pia Uk na Usa anatafta patnership kwa harakahara akipata hizo airport Atakua mbali sana.


KAMA ULISHAFAIL NA UWA UNAONA NI MAKOSA YAKO KILA UKIFAIL UNAJIKOSEA SANA KILA KITU KINATOKEA KWA SABABU USIKATE TAMAA KILA UKIANGUKA JIPANGUSE ENDELEA USIKAE ANZA NA ULICHONACHO SASA USIPOANZA NACHO ATA ICHO UNACHOSUBILI UTAKIONA KIDOGO AUTAFANYA KITU NA UTABAKI HAPOHAPO.
 

Attachments

  • 1423947226437.jpg
    1423947226437.jpg
    107.2 KB · Views: 1,319
Hii imenitia moyo sana na kunipa morari nizidi kupambana na nisikate tamaa. Nami nilifanya mengi tu muda uliopita (2013-2014) lakini nilianguka na kupoteza pesa zangu. Sasa napanga kufanya vitu vingine tena na tena, hadi pale nitakapofanikiwa. Ewe Mungu naomba tusaidie watafutaji wote!
 
Huyo kanitia moyo sn kukomaa mpka dam ya mwisho
 
ukiamua kila kitu kinawezekana,fursa zipo nyingi ila zinahtaji utoe aibu ya kuonekana kwa watu.ukishaamua utaziona tu.
Let them wait see and copy.
 
Wajasiliamali wengi waliofanikiwa lazima kuna mahala walifeli then huko kufeli kukawafanya wakaze buti zaidi, labda wenye bahati zao waliokuta wazazi wao wameshawatafunia wao wanameza tu, mfano watoto wa baharesa, mo n.k
 
Wengi wanasahau kuwa kuwa milionea lazima uwe na Milion dollars etc
Huyu anakalibia huko ila bado
 
Hongera zake. Ila mimi na principle moja work hard and save while u r still young and energetic especially at your early twenties to mid thirties hii ndiyo njia pekee itakayokutoa. Usidharau kaz. Pia usiruhus hela yako itoke kisengesenge nimemsoma sana warren buffet. Akiba ninayo kwa kubeba boksi tu kibongobongo piga ua naweza kuwa top elfu kumi
 
Wengi wanasahau kuwa kuwa milionea lazima uwe na Milion dollars etc
Huyu anakalibia huko ila bado

Hujui real Definition. Kuwa milionea wa dola maana yake una assett worth minimum dola milioni moja ambazo zinakuingizia return ya at least asilimia nane ya dola milioni moja kwa mwaka baada ya kodi. Mfano nikiwa na hisa za 1 million dollar tayari mimi ni milionea au nikiwa na biashara ina worth hiyo amount tayari mimi ni milionea. Hawaongelei cash bali wanaongelea asset zinazotengeneza cash. Huyu jamaa ana biashara worth million dollars ndo maana an return ya milioni mia nne kwa mwaka. Kwa hesabu za haraka haraka biashara yake inaweza ikawa na thamani ya dola milioni nne mpaka sita iwapo ataamua kuiuza hii leo.
 
Hii ni moja kati ya nyuzi bora kabisa JF. Ukiisoma unajikuta unapata nguvu mpya ya kuboresha kile unachokifanya. Sintoshangaa jamaa akipaki Vogue na kwenda kufuta wateja wake viatu....
Big up mleta uzi, big up mjasiriamali.
 
Fursa zipo nyingi sana tatizo ni sisi kutokuwa na akili ya kijasiriamali zaidi ya kufikiria tu kuajiriwa.
 
Back
Top Bottom