CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,387
- 6,481
Mshana wewe uwe unalala. Naona umepost saa 10: 48 usiku! I salute you!Kuna jibu moja rahisi sana kwenye hili swali nalo ni kwa ajili ya ulinzi binafsi (pengine na familia)...lakini si kweli hata kidogo! Silaha unayo miliki ni kifo binafsi na si ulinzi binafsi , haina tija kwako haikusaidii kwa asilimia unazofikiri inakupa kujiamini kusiko halisi
Kama wewe ni mwamini wa Mungu mmoja unayeamini uwezo na ulinzi wako kwenye maisha yako kubeba silaha ni kujichanganya kiimani kwamba sasa unaamini katika ulinzi wa Mungu au silaha?
Silaha haina matokeo mema silaha chake ni kujeruhi kuua na kuangamiza, ni sahihi Kabisa kwamba tunapaswa kujihami tunapaswa kujilinda lakini kamwe si kwa mtindo huo wa kubeba silaha nzito nzito , kwani umekuwa askari wewe? Kwani ni mwanajeshi wewe? Your mind is the most lethal weapon and your faith to the Almighty creator
Silaha ni kwa ajili ya wasiojiamini silaha ni kwa ajili ya wasio waamini, silaha ni kwa ajili ya wenye rohombaya dhulmati na wanaoogopa kifo! Silaha ni kwa ajili ya maadui...kama unajiamini kama unaamini katika ulinzi wa Mungu kama huna roho mbaya sio dhulmati na huna maadui huna haja ya kubeba silaha
Wengi wamekufa wakiacha silaha zao bila kuzitumia hata siku moja...silaha ni biashara silaha ni uchumi wa watu ili wao waweze kuishi inabidi wauze silaha? Na ili wauze vizuri inabidi wakuandae kisaikolojia na wakuandalie mazingira ya woga na kutojiamini ili tu umiliki silaha ...ni aina fulani ya kucheza na akili za watu
Naamini kati yetu tutakaosoma hapa tuna berreta zetu kwenye makabati full loaded! Lakini mbona umeendelea kuugua? Mbona kuna mazingira mengi tu umeepushiwa kifo bila ya msaada wa hilo lichuma lako ulilolinunua kwa bei ghali sana?
Mrudie Mola wako ukatubu na kuungama, kwa kutokuwa na imani thabiti juu ya ulinzi wake...! Maisha yako na mustakabali wako viko mikononi mwake na sio kwenye bunduki lako , ni yeye ajuaye kutoka kwako na kuingia wako sio bastola iliyoko kabatini chuma kisichosema
[emoji15] [emoji15] [emoji15] Eti hata fulani naye a nazo mbili?[emoji23] [emoji23] za nini?[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Mungu wetu tunayemwamini ndio kila kitu kwenye maisha yetu
Ngamani ndiyo nini? Hapo umenitoa kapa!Ndio muda ambao narejea ngamani
Hahaahaha kwani hujazoea maigizo yetu mkuu bado???Hivi ule uhakiki wa silaha kwa wakazi wa Dar uliishia wapi maana nilimuona mkuu wa Kaya peke yake akiwa anahakikiwa au movie ilikuwa inaendelea. [emoji41] [emoji41] [emoji41]
upo vizuri sanaKwa anaeamini uwepo wa Mungu ni kweli kwamba kumtegemea Mungu ni jambo muhimu sana. Binadamu tuna matatizo mengi sana tunayopambana nayo katika maisha yetu. Kuna maradhi, maadui wetu wanaopatikana kutokana na sababu mbalimbali n.k. Wakati tunapopatwa na maradhi hatukai na kusema Mungu atatusaidia bila kwenda hospitali kupata matibabu (dawa).Vilevile katika kukabiliana na maadui hatupaswi kukaa tu na kusema Mungu yupo atatulinda bila kuchukua hatua stahiki. Ndiyo maana tunajenga nyumba, tunaweka milango na mageti na vifaa vingine vinavyotusaidia kwenye masuala ya usalama kama security lights, CCTV cameras n.k. Na hivi kwa hakika vimesaidia au kuokoa wengi. Kitu muhimu kwa anaeamini uwepo wa Mungu ni kujua kuwa pamoja na hayo yote hapo juu lakini hayawezi kufanikiwa bila nguvu ya Mungu.
Nitoe mfano mmoja kutoka kwenye biblia. Kwa wasomaji wa biblia mnaelewa kisa cha Daudi (mwisraeli) aliyemuua mfilisti Goliathi kwa kutumia kombeo (sling) na mawe. Huyu Daudi alikwenda na kombeo na mawe ili kupambana na mfilisiti Goliathi ambaye alikuwa ni jitu kubwa na lenye nguvu sana lakini Daudi akiwa na silaha hiyo na mawe yake mfukoni alimwomba Mungu wake na kisha akaingia vitani na akaweza kumshinda adui yake Goliathi. Yaani Mungu aliweza kubariki silaha (kombeo na mawe) aliyokuwa nayo Daudi.
Ukiangalia huo mfano utaona kwamba kuwa na silaha kama bunduki (kombeo) na risasi ( mawe) siyo jambo baya na haimaanishi kuwa umiliki wake unaashiria kutomtegemea Mungu. Kitu muhimu ni kwamba umiliki wa hizo silaha uwe ni kwa kufuata sheria, silaha zitumike kwa malengo halali (kujilinda) na pia umiliki wa silaha usitufanye kuwa na kiburi na kudhani kuwa kwa vile tuna bunduki hizo basi Mungu hana nafasi tena juu ya maisha yetu na hizo silaha zetu. Hayo ndiyo mawazo yangu.
hizo ni ajali tu kama zilivyo ajali nyingine. watu wasipomiliki silaha madhara ni makubwa zaidi! tafakari vizuri kama hoja yako umeitoa moyoni.Haya ndio madhara ya kukaa na silaha ndani
1.Jamaa mmoja hapa Dar aliwakurupusha majambazi waliotaka kuiba kwa jirani yake kwa kupiga risasi tatu juu
Siku iliyofuata usiku wa saa mbili jamaa walimvamia jamaa akiwa kakaa sebuleni na kumtoboa macho mbele ya familia yake
2. Jamaa mwingine yeye alipishana lugha na mkewe usiku wakiwa wamelala jamaa akatishia kumpiga mkewe risasi, ni katika purukushani za kupokonyana silaha jamaa alimpiga ya tumboni mkewe na kufa muda mfupi baadae, mpaka leo yupo segerea
3. Hii niliishuhudia live tulienda kumtembelea jamaa yetu siku moja jumapili mchana , tukiwa tumekaa sebuleni akatoka chumbani mwanae wa kiume wa umri wa miaka 5 hivi kaelekeza bastola kwa baba yake
Mwanzoni tulidhani ni toy lakini kumwangalia jamaa alivyotoa macho ya woga tukajua kuna hatari
Mtoto akawa anamwambia babaake Dad hands up wote tulikuwa kimya
Aliyeokoa jahazi ni mdada wa kazi aliyekuja kwa nyuma na kuikamata silaha na kuelekezea juu ambapo ili fire[emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134]
Kumbe jamaa analala na ile silaha na kuiweka tayari kwa kupiga ila asubuhi huirudisha kabatini lakini siku hiyo akapitiwa, siku iliyofuata jumatatu jamaa aliipeleka police ikauzwe
Tunapaswa kujihami tunapaswa kujilinda lakini ulinzi wetu Usiwe chanzo cha maafa na matatizo
Tunajenga nyumba na kuziwekea ulinzi mkali mpaka zinageuka gereza la kifo badala ya nyumba
Tunakuwa na silaha za hatari ndani ya nyumba kwa ajili ya kujilinda lakini ni silaha hizo hizo hutuletea maafa wenyewe
Tunakuwa na mazindiko mbalimbali na mahirizi makubwa yanayotufanya tuingie kwenye maagano yenye madhara makubwa halafu Tunakufa na malaria
Bado ulinzi wa Kimungu ndio ulinzi bora kuliko mwingine wowote ule..vyovyote iwavyo usisahau Mungu ndo mweza wa yote na vyote
Ni kweli mkuu. Tena ajali alizotolea mfano Mshana Jr ni zile ambazo kwa kiasi kikubwa zimetokana na aidha uzembe au matumizi mabaya ya silaha. Hiyo ya jamaa kumtishia mke wake kwa bastola ni matumizi mabaya ya silaha kama ilivyo matumizi mabaya ya barabara kwa madereva. Na kwa upande wa mfano wa mtoto aliyetoka chumbani na bastola hadi sebuleni huo ni uzembe wa mmiliki ambao hautakiwi.hizo ni ajali tu kama zilivyo ajali nyingine. watu wasipomiliki silaha madhara ni makubwa zaidi! tafakari vizuri kama hoja yako umeitoa moyoni.