sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,989
- 4,162
Waungwana wa humu, hapa nina wazo la kijinga tu hapa. Lakini ndio JF ilivyo hata ukiwa na pumba watu wataisoma tu. Mfano mimi nimewaza niandike kila atakayepitia uzi huu utaje kwanza Umri wako na mali ulizonazo hadi kufikia umri wako. Au kama ulishazipoteza kwa ujinga wako au bahati mbaya.
Kwangu mimi naanza hivi japo sijafanikiwa sana katika maisha kwa jinsi nilivyojipangia kuwa.
Nina umri wa miaka 42.
Nina mke na watoto watatu, japo nishakuwaga na michepuko, ila nishaipiga chini.
Nina kaduka ka mtaani kadogo japo kananiingizia kakipato kwa kula mboga na ugali.
Nina kagari kadogo ka kirikuu nilikaagizaga Japan.
Nina pikipiki ya kijapan used inanisadia visafari vyangu vya hapa na pale.
Nishawahi kununua pikipiki pia za kichina kama Fekon na Sanlg.
Nimefanikiwa kujenga nyumba ambayo thamani yake imefika 32Mln.
Nina vitu vya nyumbani vingi tu kama set ya kochi za mbao za kizamani za mninga, vitanda kama vinne vya mbao, TV Samsung 32"flat panel HD, Sony 5.1 channel home theatre, Jiko la umeme na gas, fridge Juba la kikorea, ving'amuzi vya dstv vitatu, Azam kimoja na madish yake, nina dish kubwa la nchi 6, vifaa vya kazi kama grinder, drill sander, nina simu ya sumsung, ipad ya apple, laptop toshiba, printer ya samsung laserjet, na vingine vingi vidogo dogo kama blender, juice dispencer nk.
Huu ni ujinga wangu ninaojisikia kuandika kwa leo. Hebu tuletee na wakwako pia ili tujilinganishe mafanikio yako hadi katika umri ulio nao.
Maana wengine umri mdogo wana mali za mamilioni wengine umri mkubwa wana mali za maelfu na wengine hawana kabisa hela zinaishia kula.
Kwa kifupi mafanikio yangu yametokana na ubahili wangu, sinywi pombe wala kula bata. Hata pamba za bei mbaya za dukani sivai kwa sababu sina pesa za kufanya hayo, la sivyo nitachekwa. Nakomaa sana kwenye kazi lakini napata vihela vidogo sana.
Natamani niweze kujenga ghorofa lenye swimming pool na kuendesha magari kama range rover au wagon yoyote kali. Natamani nipate mchongo utakaonipa pesa nika enjoy utalii sehemu mbali mbali ninazotaka duniani. Maana maisha ni mafupi alafu duniani kuna raha sana.