Unalifahamu kundi la UB40?

Francis Mawere

JF-Expert Member
Nov 17, 2015
958
830
Ninapoongelea UB40 hapana shaka kwa wewe mpenzi wa burudani ya Muziki utakua unajua anwaongelea wakina nani. Kwa namna moja ama nyingine utakua umekwisha kusikia kibao kama vile “Red Red Wine, I got the Cup” na ule wa Falling in Love with You. Sasa pata kujua nyimbo zote hizo ni kazi za kundi hili la muziki kutoka huko Kusini mwa Birmingham, England. Kundi hili lilikua na vichwa kama vile Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan

Mwanzo wa kundi hili.
Wana kikundi hicho walikua marafiki tangu wakiwa shuleni na Ugumu wa maisha walio kua nao ndio uliosababisha kuunanisha vipaji vyao na kutengeneza kikundi hicho ili kufanya muziki na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini waliokua nao.

Jina la Ub40 lilikuja kutokana na wananchi wa Uingereza kutoa waraka wenye kurasa 40 uliohusu mafao yao ya afya na ajira . hivyo basi kundi hili likaamua lijiite Ub40.
Brian Travers alijiunga na kundi hilo akiwa na zana yake ya Saxophone huku wengine wakija na magitaa. Na mara walianza kubandika mabango katika mitaa ya Uingereza wakitangaza bendi yao.
Wimbo wao wa kwanza ulisikika katika Ukumbi wa The Hare na Hounds Pub Februari 1979 katika shereh za kuzaliwa rafiki yao.
Chrissie Hynde ndiye aliye waona vijana hao wakiimba katika ukumbi mmoja ndipo alipoamua kuwafadhili na kuwapa nafasi ya kurekodi wimbo wao wa kwanza “King/Food for Thought” wimbo ambao ulishika nafasi ya 4 katika chati za muziki nchini humo.
Albamu yao ya kwanza iliitwa “Signing Off” wakimaanisha wanayamaliza malalamiko yao ya ukosefu wa ajira na mafao ya afya. Albamu hii ilizinduliwa rasmi Agosti 1980.
Ikumbukwe kua mnamo mwaka 2010 mahakama ya Uingereza ilitangaza kuwa UB40 imefilisika. Kufilisika kwao kumekuja baada ya wanamuziki wane kina Jimmy Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan kushindwa kulipa madeni yao ya kodi.
Kundi hili ndilo kundi linalotajwa kuwahi kuuza nakala nyingi duniani katika nyanja ya Muziki.

Japo kwa ufupi nmeweza kukupatia historia ya Kundi hili amabalo liliwika mno miaka ya nyuma.

Nimeandika Makala nyingi zihusuzo MAISHA, MUZIKI na MICHEZO Ili kuzisoma zote tafadhali tembelea >>HAPA<<<
 
I like that song, Red Red wine... Ni moja ya vibao Niki play pembeni na red dry wine, nasahu machungu ya maisha...
 
Ni mgao/ruzuku unapewa ukiwa hauna Kazi, ili kupata huo mgao inabidi ujaze form "Unemployment Benefit 40" sasa huo mgao ndio wakaupa jina la utani UB40. Sasa hawa mabwana walikuwa wanavuta huo mgao kipindi wanakutana kuanzisha hilo kundi.

Siku hizi huo mgao unaitwa JSA kwa maana ya Job Seekers Allowance.
 
Ukiingia YouTube search UB40 live at Montreux 2002 uone jamaa wanavyopiga Kazi live kwenye stage. Ni clip ndefu kama SAA Na nusu.
 
Walikua vizuri enzi za Makali yao bob but for now ni sawa na Msondo Ngoma
Unajua ni vizuri kustaafu mapema kuweka Legacy .Tofauti ya Ub40 walikuwa wanaimba wapate pesa, Msondo Ngoma wanaimba Ila wapate pombe Na mademu. Sasa inafika fainali wanajikuta wako nyumba za kupanga Na wanadaiwa kodi. Huku kina Ali Kiba na Mondi ndio hivyo tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom